Kumbe Katiba ya Tanzania Haitumiki Zanzibar! - Pinda akiri Utata!. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kumbe Katiba ya Tanzania Haitumiki Zanzibar! - Pinda akiri Utata!.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pascal Mayalla, Jul 1, 2010.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Jul 1, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,573
  Likes Received: 18,464
  Trophy Points: 280
  Wanabodi,

  Katika kipindi cha maswali na majibu ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu bungeni asubihi hii, imedhihirika kumbe Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, haitumiki Zanzibar hata katika uchaguzi wa Wabunge wa Bunge la Muungano!

  Tanabahi hiyo, imetolewa na swali toka kwa Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Hamad Rashid Mohamed, na kuuliza kwa nini Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeipa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEK), uwakala wa kuendesha uchaguzi wa rais na wabunge, lakini ZEC inatumia sheria ya uchaguzi ya Zanzibar badala ya ile ya Muungano?. Mhe. Hamad Rashid akauliza endapo kutatokea kesi ya uchaguzi ya ubunge wa Muungano, kesi hii itaamuliwa kwa sheria gani?.

  My Take.
  Kumbe zaidi ya zile kero za muungano zilizokuwepo, bado kero zinazidi kuibuliwa kila kukicha, hivi kuna tatizo gani kwa Tanzania na Zanzibar kuufumua huu muungano na kuufuma upya tukianzia na katiba mpya sio tuu, kuunda muungano thabiti, imara na madhubuti bali pia kutengeneza level playing ground kwenye medani za siasa?.

  Waziri Mkuu Pinda alikiri hilo ni tatizo na ufumbuzi wake utapatikana endapo kutatokea kesi ya uchaguzi ambayo haijawahi kutokea, atasubiri busara za mahakama kwenye hili.
   
 2. Obuntu

  Obuntu JF-Expert Member

  #2
  Jul 1, 2010
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 512
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Pinda is not serious!

  Tatizo lipo - Ufumbuzi wake mpaka itokee kesi - na uamuzi wa kesi utategemea busara za mahakama!
   
 3. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #3
  Jul 1, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Du! bongo bana, sasa huko mahakamani si wanasema mambo ya siasa ni bungeni, huyu mkuu anatwambia tena otherwise. Inakuwaje Lol.................
   
 4. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #4
  Jul 1, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Nimelisikia swali, lilikuwa la akili sana na inaonyesha kweli kuna problem kubwa ya Kikatiba kwenye suala hili. Inaelekea CUF wana orodha ndefu ya matatizo ya kikatiba katika set up ya Muungano na wanatyoa issues kidogo kidogo. Nawashauri wangeandaa dossier kuhusiana na matatizo haya ya kikatiba ambayo wataitumia kupush agenda ya kuandikwa kwa katiba mpya
   
 5. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #5
  Jul 1, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  the question is, Mahakama ipi? hii hii inayoburuzwa na ccm?
   
 6. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #6
  Jul 1, 2010
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,920
  Likes Received: 2,069
  Trophy Points: 280
  Halafu tunasema tunae waziri mkuu!
  Busara ya mahakama ni kutokuingilia/kutoamua mambo ya kisiasa hivyo ishu hii ikitokea mahakama itairudisha bungeni kama ilivyofanya kwenye ishu ya mgombea binafsi!
   
 7. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #7
  Jul 1, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Mwanasheria Mkuu wa JMT alikuwepo huko Bungeni au hakuwepo? Swali kama hilo Waziri Mkuu hakutakiwa KABISA kujaribu kulijibu!! Siyo kila swali analoulizwa afikiria analo jawabu.
   
 8. W

  WildCard JF-Expert Member

  #8
  Jul 1, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Kila Jimbo Zanzibar lina MUWAKILISHI na MBUNGE. Na majimbo yenyewe hata watu 5000 kwa jimbo hayana!
   
 9. W

  WildCard JF-Expert Member

  #9
  Jul 1, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Hii wameiiga ile "PMQ" ya kila Jumatano kule Uingereza. Majibu yote anayatoa WM tu. AG hakuwepo leo lakini hata angekuwepo asingejibu.
   
 10. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #10
  Jul 1, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,573
  Likes Received: 18,464
  Trophy Points: 280
  .
  Q&A ni ya PM tuu. Ila pia Pinda, amekiri kuwa hili ni gumu, wanachoweza kufanya, ni kusubiri siku Wizara ya Sheria na Katiba itakapowasilisha makadiria yake, kambi ya upinzani iliweke kwenye maoni ya upinzani.

  Tukubali tusikubali, structure ya Muungano wetu ina matatizo. Zanzibar ni jeuri, inatumia jeuri ya uwepo wa katiba yake kuendesha kila kitu Zanzibar kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar hata kwenye mambo ya Muungano. Ukizama sana kwenye hili, unaweza kuta kumbe hao wabunge wa Zanzibar sio legitimate MP kwa sababu hawakuchaguliwa kwa mujibu wa Katiba ya JMT. Kimfumo, Katiba ya JMT ndio sheria mama, na Katiba ya Zanzibar ni subrdinate tuu, sasa hii ZEC imepata wapi mamlaka sio tuu ya kuitumia sheria ya Uchaguzi ya ZEK kwa wabunge wa Muungano, bali pia kui-sideline/ignore Sheria ya Uchaguzi ya NEC.

  Natamani kuina hand-over note YA NEC iliyodelegate powers kwa ZEC kuendesha uchaguzi wa rais na wabunge kama wakala wa NEC.
  Sijapata kusikia wakala anaepaswa kutekeleza majukumu ya asliyemtuma kwa kujiundia sheria zake!.

  Tukizama sana humu, tutarudi kule kule kwenye malumbano ya uhalali (legality) ya huu Muungano wetu.
   
 11. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #11
  Jul 1, 2010
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,684
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160

  Mh. Rashid naye si mbunge wa JMT? sasa yeye mwenyewe hatma yake ni ipi?. Ninavyoelewa kule ZNZ kuna Wawakilishi ambao nadhani ndio wabunge halali wa huko. Hawa wabunge wanaokwenda DOM kama MH. Rashid wanaweza kujikuta hawana pa kwenda maana maamuzi mengi kuhusu kero za muungano huwa yanatolewa na Baraza la Wawakilishi!!
   
 12. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #12
  Jul 1, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Hivi hii serikali ya CCM ina matatizo gani, kwanini hawataki kuwa pro-active?
  Yaani kweli PM anakiri na kusema solution itatokea pale tatizo litakapotokea!!! Huu muungano ni zimwi tusilolijua litatula mpaka twishe!!!

  Shame on the government!!
   
Loading...