Kumbe Kanali wa Jeshi ni cheo kikubwa kuliko cheo cha IGP

FisadiKuu

JF-Expert Member
Nov 19, 2015
8,108
13,346
Habari wanabodi,

Nimeshangazwa kuona Kanali (Mpambe wa Rais) akipigiwa saluti na IGP Sirro pamoja na Kamishna Mkuu wa Magereza..

Je, hii ina maana Cheo cha Kanali ni cheo kikubwa sana kuliko cheo cha IGP pamoja na makamishna wote wa vyombo vingine vya dola ukitoa JWTZ?

Na Je, cheo kikubwa kabisa cha Polisi ni sawa na cheo gani cha kijeshi?
 
Labda kulikuwa na wanasiasa eneo hilo ambao kisheria watapigiwa saluti wabunge mawaziri n.k.
 
FisadiKuu,

Siyo kweli, umeona vibaya. Angalia vizuri wakati Mh. Rais anasalimiana na wageni kwa kupeana mikono kabla hajamfikia IGP Sirro. Kushoto kwa Sirro alikuwepo Mabeyo; baada ya Mabeyo kumpigia saluti Mh. Rais, na Rais akasogea kwa Sirro. Wakati Sirro anapiga saluti muda huohuo, yule Kanali wa Jeshi alikuwa amempigia boss wake (Mabeyo) saluti. Hivyo, mkono wa kulia wa Kanali ukaendana na saluti ya Sirro akimpigia Rais. Ukiangalia vibaya unaweza sema ni kweli Sirro kampigia Kanali saluti lakini sivyo.

Sorry, nilikuwepo ndiyo maana nakuelewesha hivyo.
 
nilikuwa makini sana hapo mleta mada hukuona vizuri raisi alipofika kwa IGP ndo IGP akatoa saluti lakini mpambe hakutoa saluti isipokuwa rais alipokuwa kwa mkuu wa majeshi mpambe wa rais nae alitoa saluti kwa mkuu wa majeshi
Safi. Kumbe na wewe umeona? Nadhani tulikuwa wote pale sema hatujuani.
 
Mtu anayeweza kuamuru vituo vidogo vifungwe au visifungwe kweli anampigia Kanali saluti? Si mchezo.
 
Miaka fulani tulifanya battle humu JF. Jibu la mwisho na ninaloliamini ni kuwa vyeo vya jeshi fulani havina hadhi katika jeshi lingine. Mfano kufananisha Polisi na Jeshi la Wananchi. Kila jeshi lina different ways of recruitment, kupanda vyeo, mafunzo n.k.

Kuna mdau alitamatisha humu kuwa mtu wa Jeshi A halazimishwi kupiga saluti kwa mkubwa wa Jeshi B, na endapo atafanya hivyo, anafanya tu kwa heshima na kwa kuamua.
 
Sina uhakika kama observation yako iko sahihi.

Naomba link ya hiyo video nikatazame ndo nirudi kutoa comment nyingine
Kanali yuko na Rais full time. Akipigiwa salute Rais kama huangalii sawasawa au una malengo ya kutuondoa kwenye mada za kijinga za Kigogo, ndio zinakuja threads kama hizi.
 
Back
Top Bottom