Kumbe JK alikuwa na mpango wa kurudia aliyoyafanya 2005? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kumbe JK alikuwa na mpango wa kurudia aliyoyafanya 2005?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by MwanaHaki, Nov 3, 2010.

 1. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #1
  Nov 3, 2010
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Wakati wa Mkutano Mkuu wa CCM pale Chimwaga, Dodoma, wakati wa kupiga kura za kumteua mgombea wa Urais kupitia chama hicho kwa Uchaguzi Mkuu wa 2005, baadhi ya wajumbe waliokuwapo kwenye Ukumbi wa Chimwaga walisikika wakisema, baada ya zoezi hilo kukamilika, kwamba, ilikuwa kana kwamba kulikuwa na "jinamizi" lililopita, na kuwapumbaza watu wote waliokuwapo pale, kiasi kwamba, hata wale waliopanga kuwachagua wagombea wengine walijikuta wakiweka "tick" kwa Kikwete, hatimaye wakibaki na alama za mshangao na kujiuliza: Tumefanya nini?

  Sitaandika ninachokijua, lakini nimepata habari hizo, na kwamba mgombea huyo alitahadharishwa kutorudia aliyoyafanya 2005, la sivyo ingetokea vita kubwa ya kidini ambayo ingeleta maafa makubwa sana.

  Nani aliyemtahadharisha sitamtaja pia. Lakini ni mambo mazito.

  Afadhali amesikia ushauri huo, la sivyo, hivi sasa wengi wetu tungekuwa "wakimbizi", huku tukiwa tumechomewa nyumba zetu, mali zetu, magari yetu, na kadhalika.

  Allahu Akbar!

  Mungu ni Mkubwa!

  Bwana Yetu Asifiwe!

  -> Mwana wa Haki
   
Loading...