Kumbe JK alikuwa anampinga Lowassa kimya kimya? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kumbe JK alikuwa anampinga Lowassa kimya kimya?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Lunyungu, Jul 12, 2009.

 1. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #1
  Jul 12, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Date::7/11/2009

  Kikwete apinga hoteli kujengwa mbugani

  Na Peter Edson

  RAIS Jakaya Kikwete amepinga hoja ya aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowasa aliyoitoa bngeni enzi za uongozi wake ya kutaka zijengwe hotel nyingi maeneo ya hifadhi za taifa.

  Badala yake Rais Kikwete ameiagiza Wizara ya Maliasili na Utalii kuhakikisha kuwa inadhibiti ujenzi holela wa hoteli katika maeneo ya mbuga za wanyama.

  Akizungumza wakaki wa uzinduzi wa hoteli ya kitalii ya Bilila Kempinsk yenye hadhi ya nyota tano katika mbuga ya wanyama ya Serengeti, Rais Kikwete alisema kama kutakuwepo na ujenzi holela wa hotel katika mbuga baadaye kunaweza kuleta athari kwa wanyama.

  “Tunahitaji hoteli nzuri za kitalii zenye sifa na siyo kila mtu aje mbugani kujenga hoteli. Haitaleta maana yeyote, hivyo nawagiza ninyi Tanapa (Shirika la Hifadhi la Taifa) na wizara husika kusimamia vyema jambo hili,” alisema Kikwete.


  Mwaka 2007, Lowasa aliwahi kulieleza bunge kuwa serikali inakusudia kuanza kujenga hotel kwa wingi katika maeneo ya mbuhgani kwa lengo la kuvutia watalii kutokana na ukosefu wa hoteli zenye hadhi nchini.


  Alisema sekta ya utalii ni eneo muhimu katika ukuaji wa uchumi hapa nchini kwani katika kipindi cha mwaka 2007/2008 sekta hiyo iliweza kuchangia pato la taifa kwa asilimia 17.2 na kuingiza fedha za kigeni kwa asilimia 25, jambo ambalo halikuwahi kutokea huko nyuma.

  Alisema kukamilika kwa hotel hiyo ni sehemu ya kutangaza utalii katika mbuga ya Serengeti nje ya nchi, hivyo ni vema wamiliki na wafanyakazi katika hotel hiyo wakafanya kazi kwa uaminifu ili kuvutia zaidi wawekezaji.

  “Tutapokea watalii wengi katika hoteli hii, lakini hata sisi tumepata ajira kutokana na kukamilika kwa hoteli hii, msiiharibu, ipendeni ili nayo iendelee kuwalea,” alisema Rais Kikwete.
  Alisema hivi sasa Serikali ipo katika mchakato wa kupunguza kiwango cha malipo kwa hati ya kusafiria kwa watalii kutoka asilimia 100 hadi kufikia 50 kwa mtalii mmoja, lengo likiwa ni kuondoa vikwanzo vinavyosababisha kupungua kwa watalii nchini hasa katika kipuindi hiki cha kuyumba kwa uchumi duniani.


  Mwananchi Tanzania Newspaper(MCL)
   
  Last edited by a moderator: Jul 13, 2009
 2. b

  bnhai JF-Expert Member

  #2
  Jul 12, 2009
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 2,207
  Likes Received: 1,373
  Trophy Points: 280
  Hapo nadhani namna mwandishi alivyoiframe tu. Suala la ujenzi wa hoteli lilikuwa na upinzani muda mrefu hata huyo JK naye ametaka utafiti ufanyike kabla ya ujenzi. Kwahiyo hiyo ni stahili ya uandishi wetu
   
  Last edited by a moderator: Jul 13, 2009
 3. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #3
  Jul 12, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Lakini upinzani wa wakati JK alikuwa kimya kama Rais mbona hakusema lolote hadi sasa anapo enda kuifungua hii , ambayo inasemekana ana mkono wake na labda tajiri kasema hakuna hotels zaidi ili kumpa nafasi kuwa bingwa mbugani , na mshindani pekee ndipo kauli zinatoka ?Bado nadhani kuna sense ndani yake maana JK daima huwa hasemi kwa uwazi .
   
 4. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #4
  Jul 12, 2009
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Ni mbinu za kuzuia competition tu na faida binafsi. Si porini si mjini mbona Mengi walimnyima Kilimanjaro? It is a chain and if you connect dots utajua nini kinawendelea.
   
 5. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #5
  Jul 12, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  I buy your story 220% but again why go public against mshikaji wake ? Si kwamba pia ni kampeni hizi na kuwapoza wadanyika kwamba Jamaa anajali ?
   
 6. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #6
  Jul 12, 2009
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,855
  Likes Received: 2,430
  Trophy Points: 280

  ....hiii ndio ile hoteli tuliyosemaga hapa kuwa bwana mkubwa ana ubia ...serengeti...!!

  conflicts of interest hapo...mzee hiyo kuzuia hotel kujengwa mbugani ameona leo...
   
 7. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #7
  Jul 12, 2009
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0

  Hotel ya Bilila Kempinsk imeshajengwa na sasa anazuia nyingine kujengwa ili kuipa Hotel hii impya ambayo tetesi zinasema ana ubia nayo isipate ushindani.
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  Jul 12, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,361
  Likes Received: 6,380
  Trophy Points: 280
  anapinga kujengwa hoteli Serengeti wakati akifungua hoteli iliyojengwa humo? Je zikitaka kujengwa hoteli kama za ubora wa hiyo aliyoifungua atakuwa na matatizo nayo?
   
 9. b

  bnhai JF-Expert Member

  #9
  Jul 12, 2009
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 2,207
  Likes Received: 1,373
  Trophy Points: 280
  Mengi alishindwa kushindana si kwamba alinyimwa. Yapo mahoteli mengine huko, sidhani kama njia hiyo inatosha kuzuia competition
   
 10. I

  Ipole JF-Expert Member

  #10
  Jul 12, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 296
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mzee Mwanakijiji mwanzo nilikuona kama mtu mwenye busara lakini sasa naanza kupata mashaka kidogo kwamba ndiye mwanakijiji huyu huyu aliyekuwa anatuletea hadithi za kuvutia au mwingine. Katika hali ya kawaida kwa binadamu yeyote mwenye busara hivi tunahitaji kweli kuwa na Hotel nyingi katika mbuga za kuhifadhi wanyama? Mimi sidhani JK kwa kusema hivyo alikuwa anafanya makosa.
   
 11. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #11
  Jul 12, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  JK hafanyi makosa haya leo lakini wakati kaingia madarakani na mshikaji wake Lowasa ndiyo walio komaa na ujenzi wa mahoteli na uwanja wa ndege .Haya hakuyaona ama kaona baada ya Hotel yake kuisha ? Now Mwanakijiji hapa kakosa busara wapi ? Soma tena bandiko lake na utajua kwamba kaweka alama ya kuuliza na hajasema watu wakajenge huko hoteli .
   
 12. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #12
  Jul 12, 2009
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mkuu,
  Tutegemee nini kutoka kwako pale unapotaka kulazimisha hoja juu ya JK dhidi ya Lowasa?
  Kauli ya JK haipingani kwa namna yeyote na hiyo kauli ya Lowasa.
  Lowasa amesema zijengwe hoteli nyingi na JK amesisitiza zisijengwe kiholela ni lazima ziwe na ubora wa hali juu zitazovutia watalii. Kwa maana hiyo basi hata zikijengwa 1000 lakini zikiwa nzuri kama Bilila, RUXAAA!!!!!
   
 13. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #13
  Jul 12, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Ipole,
  Ni lini mheshimiwa rais alipotambua kwamba kuna hatari ya kujenga hoteli nyingi katika mbuga za wanyama? Baada ya hoteli ya rafiki yake kumalizika? Na kwa nini?
   
 14. M

  Makabe Member

  #14
  Jul 12, 2009
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  JK amekuwa na maono ya mbali. Hakunahaja ya kujengwa kwa hoteli nyingi mbugani mfano wa hiyo aliyoifungua, ni vema ukabuniwa utaratibu wa kuwa na hoteli za mfuto ambazo si kama zao huku marekani na ulaya. wenzetu wanataka vitu tofauti. kuwajengea mahoteli kama yaliyoko kwao si kuwavutia bali kuwfukuza
   
 15. M

  Mkandara Verified User

  #15
  Jul 12, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Ipole,
  Nadhani Mwanakijiji alichosema ni kwamba kama JK alikuwa akipinga iweje yeye alikwenda kufungua Hotel iliyopo ktk mbuga hizo hizo..Kama imewezekana moja itashindikana vipi kufunguliwa ya pili au tatu zenye ubora kama huo au zaidi..
   
 16. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #16
  Jul 12, 2009
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Kaazi kwer kwer
   
 17. M

  Mundu JF-Expert Member

  #17
  Jul 12, 2009
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,719
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Wandugu kwenye siasa au ungwini hakuna aliye sahihi na ambaye si sahihi, kilichopo ni kujenga hoja na kuitetea hoja.

  Kikwete amewahi kutofautiana kikauli na Lowassa mara nyingi, mojawapo ikiwa ni ile ya "Mamilioni ya Jakaya". Lowassa alitaka watendaji wa Benki wasilete urasimu wa kutoa fedha zile, na Kikwete akasema Fedha zile ni Mikopo, na taratibu zote za kibenki za kugawa mikopo nafuu zifuatwe, na hakuna kugawa fedha kiholela holela. Ni hoja tu, na jinsi mtu anapoweza kuzijenga na kukubalika.

  Na wakati mwingine mwenye kisu kikali ndiye mla nyama, na JK ana kisu cha Urais, na mara nyingi yeye husema mwishoni.
   
 18. M

  Mkandara Verified User

  #18
  Jul 12, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Sawa mkuu, lakini matokeo ya hizo mabillioni ya Kikwete mbona ziligawawiwa kiholela!
  Alichopinga mwanzo na kikatendeka kile kile alichopinga ndio kupinga gani huko, wakati mwenye last say ni yeye sii Lowassa..
   
 19. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #19
  Jul 12, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Binafsi sioni kama JK anapingana na aliyosema Lowassa. Kwanza Lowassa alisema mwaka 2007 ambao ni muda mrefu na huenda tayari hotel zinaanza kuwa nyingi kiasi cha JK kuona kuna haja ya kufanya control.

  Mwandishi kaongeza chumvi labda ili kuuza magazeti lakini sioni hii habari inaendana na kichwa cha habari, naona mwandishi ana create a storm in a tea cup.
   
 20. MwalimuZawadi

  MwalimuZawadi JF-Expert Member

  #20
  Jul 13, 2009
  Joined: Sep 1, 2007
  Messages: 643
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Wakuu tatizo la Tanzania si nani kasema nini lini na wapi. Cha msingi ni nani kafanya nini lini na wapi. Maneno ya hawa woooote JK na genge lake yamekuwa na utata mara nyingi sana. Kitakachosemwa kinaweza kumaanisha kitu kingine kabisa au ni mtego wa kumyaka ngedere mwingine aliye mbali!!!
   
Loading...