Kumbe JamiiForums asilimia 99.9 ni watumishi wa Serikali

kitokololoo

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
704
813
Bisha ubishavyo ila huo ndyo ukweli hili limejidhihirisha baada ya mshahara wa watumishi wa serikali kuchelewa kuingia kila Uzi humu ilikuwa ni kilio cha mishahara...

Kuna Uzi hapa wakuulizia mshahara umefikisha 35k viewers hahaha hii inaonyesha wengi hujifanya watu wenye pesa walojiajiri kumbe si kweli wengi watumishi humu.

Maisha tunategemea wafanyabiasha na wafanyakazi hutegemeana biashara huchanganya tarehe za mishahara tusizomeane humu..

Lakini ndugu zangu watumishi nanyi mjifunze kuweka kaakiba ili hii aibu isiwakumbe tena pia kipindi cha mvua jitahidini basi ata kulima ka heka ka moja ka mahindi na vimaharage au ata mpunga ili inapotokea kama hivi unabandika Maharage unampa mama mia tano tu anaenda koboa mpunga mambo yanakuwa poa kabisa sasa pia lima ka bustani ata tuta moja ka mboga mboga huta juta tarehe kama hizi utaishi vzr tu na vilio vitapungua pindi mshahara ukichelewa haupati kadhia hii

Halafu baada ya Leo kupata mshahara waliokuwa wanalialia mshahara humu kila mtu atageuka kuwa si wafanyakazi tena kila mtu mfanyabiashara tena mwenye mamilioni hyo ndyo jf

Nawakumbusha tu Leo tarehe 24 mpk mwezi ujao tena tarehe 24 pia kuna sikukuu apo katikati ya mwezi june tumieni vzr.

By mkulima mfanyakazi from mbeya.
 
Unabisha nini kaka na kuna ushahidi upo Uzi umefikisha 37k viewers na comment Karibu 1000 huko watu wakidai mshahara umechelewa

Na ww nimeona comment yako unalia njaa
 
Kwani mtumishi hawezi kuwa, "good life"

Shombo za humu ni kichefuchefu si bora wao wana hakika ya kuingiza kila mwezi aliyejiajiri mteja wake mkuu ni muajiriwa, ni mshenzi tu ndo atamchekelea mwenzie
 
Wamekukosea nini?
Maisha kutegemeana, mwenyewe unasubiria watumishi hao hao waje kwenye biashara yako ya mazao.
 
Baada ya mshahara kutoka leo, kuanzia kesho hadi tarehe 19 juni kila mwanaJF ni mfanyabiashara mkubwa ambaye mtaji wake unaanzia Milioni 100.

Ikifika kuanzia tarehe 20 hadi 25 juni tunafilisika ghafla. Ukiijua JF wala hupati taabu
 
Watumishi wengi wanapata taabu wengine unasikia Mkuu wa wilaya kawasaidia kuchukua ATM Card huko walikokopa ni kazi sana mtu hawezi kuishi siku sita mbele mshahara ukichelewa ni shida mtindo mmoja...
 
Kila mwana jf ni mfanyabiasha tena mwenye mtaji wa mamilioni hiyo ndyo jf kilichonishangaza mm why Uzi wa kuulizia mshahara umekuwa na viewers wengi na comment kibao nilichogundua wengi wanadanganya humu yani ingekuwa tunatumia real id tungekimbiana humu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom