Jumong S
JF-Expert Member
- Jul 3, 2013
- 7,295
- 10,467
Watu ni wengi sana!Pembeni lilipaki Hummer kubwa jekundu. Majukwaa makubwa kabisa na maspika yasiyopungua 50 yanaashiria uwepo wa Mch mahiri na kijana kabis Gwajima hapa Morogoro!
Waimbaji wakubwa nchini Flora Mbasha,John Lissu na wengine wanasifu kwa bidii sana! Baada ya sifa Mch anaalikwa na anaanza kuhubiri sana kuhusu uchawi. Ameelezea aina za misukule na kwa nini hakumrudisha Amina Chifupa. Amepiga mkwara sana na kusema leo wanarudishiwa uhai.
Kweliii
Baada ya mahubiri anaomba kwa bidii na kuita njoooo. Watu kadhaa wanaanguka chini, wengine wanatembea kama wanyama, wengi wanakimbia kwenda mbele, baadhi ya watu wanakimbia kuogopa mikiki mikiki! Wanaoitwa misukule baaadhi wanatoa shuhuda walikokuwa wamefichwa!
Lakini nikajiuliza maswali kadhaa:
1. Mchungaji mbona anautajiri mkubwa sana?
2. Hawa misukule ni halisi na je, ndugu zao watawapokea ikiwa watajua kweli ni wao (maana kuna mmoja kadai alichukuliwa na mpangaji wao miaka 5 ilopita)
3. Hii injili inaelekea wapi? Sio kwamba hapa tunapigwa changa la macho?
4. Kwa uchunguzi mdogo, wengi wanaoenda wanapelekwa na kushangaa misukule, je jamaa anatumia nguvu za Kristu kweli aliye hai?
Please, mwenye historia kidogo ya huyu mchungaji atujuze.
Asanteni.
Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums