Kumbe hii ndiyo maana ya "Kazi Iendelee"?

Wakati akiingia madarakani, Rais wa awamu ya 6 alitambulisha kauli mbiu yake kuwa kazi iendelee bila kusema ni kazi ipi hiyo, je ni ile iliyofanywa na awamu ya 4 na kuja kusitishwa na awamu ya 5 au ni ile iliyofanywa na awamu ya 5 iendelezwe.

Kadiri muda unavyo kwenda nimeanza kuelewa ni kazi gani mama alisema iendelee, katika uzi huu nitaonesha baadhi ya kazi hizo.

1. Ujenzi wa bandari ya Bagamoyo, baada ya Dr Magufuli kunusa harufu ya ufisadi na utapeli katika mradi huo, aliamua kusitisha kazi hiyo, mama ameonesha interest ya kuruhusu mradi huo uendelee "Kazi iendelee"

2. Mradi wa Gas Mtwara na Lindi pia ulimulikwa na mzee Magufuli na alisema wazi kuwa haridhishwi na mikataba ya hovyo katika mradi huo, serikali ya awamu ya 6 imealika makampuni kama Shell ambayo yatatumia Bilioni 73 kuendeleza mradi huo "Kazi iendelee"

3. Rais Magufuli alipo ingia alipiga marufuku korosho kusafirishwa kwa njia ya barabara kwenda bandari ya Dar, badala yake, meli zilienda bandari ya Mtwara kuzifuata, mwaka huu shehena ya korosho inasafirishwa kwenda bandari ya Dar na sio Mtwara tena "Kazi iendelee"

4. Mzee Magufuli alizuia viongozi na maafisa mbalimbali wa serikali kusafiri nje ya nchi bila kibali maalumu, yeye mwenyewe akiwa kielelezo, sahivi safari za nje zimerudi kwa kasi ya kimbunga jobo. "Kazi iendelee"

5. Mzee Magufuli alipambana na hujuma za wasaliti waliokuwa wakilichezea shirika la Umeme Tanzania na kujipatia faida kwa kuuza majenereta, na kukodisha mitambo ya umeme, na kuuza nishati ya dizeli na petroli kwa watumiaji, alipambana na waliokuwa wakihujumu kwa kufungua maji yamwagike ktk mabwawa ya uzalishaji umeme ili ionekane umeme wa maji hautoshi kutokana na kina kupungua, katika kipindi chake hakukuwa na kelele za kupungua kina cha maji ktk mabwawa yetu.

Miezi michache baada ya kifo chake, maji yameamua kupungua ktk mabwawa ya uzalishaji umeme "Kazi iendelee'

6. Mzee alizuia makinikia kusafirishwa nje ya nchi, Waziri mkuu amesha ruhusu siku chache baada ya kifo cha JPM "Kazi iendelee"

Mimi naamini kazi inayo endelea ni ile iliyokuwa imesimamishwa na JPM, na baada ya kifo chake inaendelea maana hakuna kikwazo tena. "Kazi iendelee"

By Gwajima wa JamiiForums.
Na pia usisahau, watu wajinga kama wewe wameruhusiwa tena kuandika mawazo yao bila kutishiwa.....kazi iendelee
 
Hahahaaaaaaaaaaaaa
 
Back
Top Bottom