Kumbe hii ndio maana ya neno "Demu" aisee...

zagarinojo

JF-Expert Member
Jul 26, 2020
2,622
2,835
Ingawaji mimi sio msomaji sana wa kamusi ila leo matumizi ya neno "demu"mtaani yamenisukuma kuangalia maana ya neno demu kwenye kamusi.

Nimekuwa nikisikia mara nyingi wanaume/wavulana wakutumia neno "Demu"kama jina la kuwaita wasichana ama mabinti. Taswira iliyonijia ni kwamba neno "Demu"lingekuwa na maana halisi ya msichana au binti mrembo ila haikuwa hivyo

Baada ya kuangalia kwenye kamusi. Maana niliyokutana nayo ni hii

1. Demu ni kitambaa kilichochanika/kupasuka.

3. Demu nguo iliyochakaa iliyokuwa ikitumika kifunika matiti au kufunga kiunoni wakati wa kilimo.

Neno hili limekuwa likitumika kinyume na maana yake na pengine watu wengi wameamini maana yake ni msichana mrembo.

Pia, kuna maneno mengine ambayo nimekutana nayo mahala flani kwenye mitandao ikiwemo JF Ila sijawahi kujua maana yake.

1. Pisi Kali
2. Papuchi
3. Ki Portable
4. Popo Bawa
 
.
InShot_20200927_152000401.jpg
 
Nadhani neno la kiswahili demu limetoholewa kutoka neno la kingereza Dame lenye maana sawa na lady au mke au mjane wa mjeshi.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom