Kumbe haya ndio miongoni mwa yanayofichwa!

Acha kutumia neno UCHAGUZI, na vitu vya kipuuzi,wakiita nchi zinazofanya chaguzi TZ, utaiweka???? Yaani Israeli wao wauite uchaguzi na wetu eti uitwe uchaguzi?!! Nyumbu wanaingia kwenye chumba cha kupigia kura wananyakua ballot boxes, wanakimbia nazo tena kwa msaada wa walinzi wao¡! Wanaya najisi halafu yanarudishwa tena ndani na zoezi linaendelea!!!!
Nimecheka sana...Uingereza waite uchaguzi na Tanzania tuite uchaguzi, definitions zake zitakuwa tofauti kabisa
 
Other risks to East Africa’s second-biggest economy include “delays or little progress in improving fiscal management” and rushed public investments that may not have a high rate of return, according to a copy of the IMF report that was seen by Bloomberg.
Kwa kiswahili ni umbumbu wa uendeshaji wa uchumi
 
MKURUPUKAJI yuko busy kuficha UKURUPUKAJI wake unavyozorotesha uchumi wa nchi.

Tulisema siye humu haya matumizi ya pesa nyingi za walipa kodi hayana vipaumbele kwa Watanzania na ROI ni ndogo percentage ndogo sana kwenye uchumi wa nchi. Sasa YAMETIMIA! Ili kuficha failures zake hata namba ANAZIFICHA! Ukaguzi wa matumizi unaotakiwa kufanywa na CAG Assad KAUGOMEA!

Other risks to East Africa’s second-biggest economy include “delays or little progress in improving fiscal management” and rushed public investments that may not have a high rate of return, according to a copy of the IMF report that was seen by Bloomberg.
 
Stop this crazy person before it’s too late. Let him retire peacefully to his home village. He is a DISGRACE to our beloved Nation and UNFIT to lead.

Magufuli goverment is founded on a bed rock of lies, bigotry and hate. It has lived on lies all these 3+ years and is now sinking in sewer filled pools of lies. They are not only lying to their enemies (Mabeberu), friends and well wishers but also to themselves and each other.

Other Tanzania goverments were not perfect but this one of Dr. Magufuli and his associates are talking us to the lowest levels of rot. On the whole many Tanzanians for now have far more faith in lies and dinals preached by Magufuli and his CCM cronies than in the ideal development tried to be imposed on them
 
Hapa natoa saluti.

Heshima mkuu.

Sasa hivi hivyo viwanda alivyokuwa anaimba hana habari kabisa navyo. Mji wa "Dege" Kigamboni, hata kama kulikuwa na makosa ilistahili yasahihishwe nyumba ziendelee kujengwa, sasa yametelekezwa na kuwa magofu!

Mandhari ya Dar Es Salaam yalianza kubadilika na kuwa na mwonekano wa mji wa kimataifa baada ya ile minara mitatu kuchomoza juu. Yeye aliona hilo sio jambo la maana kulifanya.

SGR na ndege ni mambo mazuri kuyafanya kama taifa, lakini yanataka kuwa na mipango itakayofanya mambo hayo yanafanyika bila kuathiri sehemu nyingine za uchumi. Hii SGR itakapofika Morogoro, sijui itachukua mda gani kufika Dodoma, na hatimae Mwanza na Rwanda! Sitashangaa akiifanya hii kuwa sababu yake kuendelea kukaa madarakani hata ikichukua miaka 30! Museveni na Kagame wamekwishaonyesha njia.

Udhaifu wake mkubwa ni kutofuata taratibu zilizowekwa katika kila jambo analorukia, na matokeo yake ni kuvuruga tu na kupoteza pesa kama ilivyotokea kwa korosho. Hili ni tatizo litakarogharimu sana uhai wa taifa letu. Na mbaya zaidi hataki kusikiliza maoni ya wengine. Yeye anajua kila kitu, kwa vile 'wanyonge' wake walishamweleza kila kitu wanachotaka (hata kama wanasingiziwa)! Yeye anatekeleza tu bila kujua athari zinazofuata katika utekelezaji huo.

Njia za Reli za zamani zinafufuriwa? Kweli tutaiona tena reli ikitoka Tanga hadi Arusha kwenye miaka hii ya karibuni? Pesa ya kazi hii imetoka wapi, na ni nani aliyeidhinisha? Of course ni yeye, kwani bunge katika macho yake ni kupoteza mda, kama ilivyokuwa kwa Stiegler''s gorge na ujenzi wa mji wa Mtumba!

Hatukatai haya mambo kuwa mazuri, lakini pamoja na uzuri huo, inatakiwa tuwe na taratibu za kuyatekeleza, lisiwe tu jambo la mtu mmoja anayetaka sifa zote kwa kila jambo ndie awe mwamuzi wa kila kitu.

Miradi yote hii, pamoja na bomba la mafuta ya Uganda, na kama gesi nayo ingekuwa inasogea sogea karibu, ikiwa na pamoja na miradi ya umeme wa gesi, - yote haya yalitosha kabisa kukuza uchumi wetu kwa kiasi kikubwa sana kama yangetekelezwa kwa utulivu. GDP yetu ingepanda sana ndani ya mda mfupi na kutuelekeza kwenye uchumi wa kati.
Na kama Bagamoyo nayo ingekuwa njiani------------ hii ingekuwa "Tanzania Mpya" kikwelikweli, na sio ya maneno matupu!

Wawekezaji walikuwa wameanza kumiminika hapa, kwa sababu Tanzania licha ya kuwa na fursa nyingi za uwekezaji, nchi yetu ipo mahali pazuri sana kijiografia. Badala ya kurekebisha matakataka aliyoyaacha Kikwete kwa uangalifu, yeye anataka aonekane hata wazungu wanamwogopa, kama anavyofanya ili waTanzania wamwogope, kama hawamsifu! Hiyo ndio iwe sifa yetu!
Naaam
 
Kwa mfano,ujenzi wa Ikulu ya Chamwino ni wazi umetumia fedha nyingi sana.Ukifika pale Chamwino ukiona tu ule ukuta unaweza kuishiwa pozi na humo ndani ujenzi bado unaendelea.Yaani ukiangali tu kwa nje,unapata picha kuwa ujenzi huo unagharimu fedha nyingi sana.

Ukuta licha ya kuwa mrefu kwenda juu,mzunguko wake ni km za kutosha maana eneo lilichokuliwa ni kuwa mno na huko ndani inaonekane ujenzi bado unaendelea wa baadhi ya majengo/ofisi kwani kuna maeneo ukuta haujafunga maeneo ambayo ni wazi zitakuwa sehemu za mageti na ni katika maeneo haya yaliyo wazi, ndio unaweza kuona japo kidogo na kwa mbali ujenzi unaoendelea humo ndani.

Hii ni mbali na kujenga mji wa serikali hapo Dodoma katika eneo la Mtumba.Miradi imekuwa mingi ya gharama kubwa na inatekelezwa ndani ya muda mfupi badala ya kuifanya kwa awamu huku mapato ya nchi yakiwa hayaendani na haya matumizi makubwa na matokeo yake ni kukopa kwa kiasi kikubwa na kubabdili matumizi ya mafungu kwenye miradi mingine.

Viongozi wa kiafrica ndivo walivo wanaangalia maslai yao. Dodoma ni kisiasa si kiuchumi
 
Hizo project zote hazikuzi pato LA mmoja mmoja ili kuongeza idadi ya walipa kodi.Hio ni miradi ya mikopo Hakuna uwezo wa kurejesha gharama na kuanza kupata faida kwa haraka
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mh.Magufuri mawazo yake angeyaweka kwenye ajenda yao ya CCM ili waanze kufanya hiki ili akiachia uongozi anaefuata anaanza na kingine ila kwa kutaka hiyo miradi mikubwa yote afanye yeye na huku biashara mtaani hakuna kabisa...kitakachokua kinafanyika ni kutembea na Wakuu wa Jeshi na kuwasifia tuu...
 
Mimi heshima kwa mkapa na kikwete imepungua sana, wao ndiyo wametuletea mpuuzi huyu , na wote tunateketea, wao meno nje na mali walizoiba
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Kabisa Mkuu hao mafisadi wawili ndiyo waliotuletea hili balaa kubwa sana nchini.

Mimi heshima kwa mkapa na kikwete imepungua sana, wao ndiyo wametuletea mpuuzi huyu , na wote tunateketea, wao meno nje na mali walizoiba
 
MKURUPUKAJI yuko busy kuficha UKURUPUKAJI wake unavyozorotesha uchumi wa nchi.

Tulisema siye humu haya matumizi ya pesa nyingi za walipa kodi hayana vipaumbele kwa Watanzania na ROI ni ndogo percentage ndogo sana kwenye uchumi wa nchi. Sasa YAMETIMIA! Ili kuficha failures zake hata namba ANAZIFICHA! Ukaguzi wa matumizi unaotakiwa kufanywa na CAG Assad KAUGOMEA!
Huyu mtu sijui huwa ana waza nini kichwani mwake.Kanuni simple kama hizi za uchumi anashindwa kuzielewa na kufanya maamuzi ya ajabu kama haya!Tumekula hasara watanzania!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom