Kumbe hata viongozi wa juu wa ccm wanajua kuwa kushika dola 2015 ni ndoto

Dr Slaa ni kikwazo kikubwa cha wizi wa wana ccm, na wana hofu sana kila wakisikia jina hili.
Ndiye mgombea aliyewashangaza wengi kwa kuzunguka nchi nzima akiwa gado.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Hila nyingine za kuwapumbaza watu, hiyo ni saikolojia tu, mnaoneshwa mmefunga kumbe mnachotwa akili zenu. Hivi inayamkinika kweli" kila kundi ndani ya ccm linatumia nguvu zake zote kuweka mgombea urais kwa tiketi ya chama chao; na wakati huo huo eti wanauhakika wa kushindwa. Kumbuka, mamba anapokula mzoga na minofu ya windo lake hutoa machozi, sio ya huzuni bali shangwe na kulilia kupata zaidi.
 
Inapelekana na tafiti zangu, kwa asilimia kubwa naona kuna ukweli toka kwa huyo kada
 
Good analysis, LU-MA-GA. Wewe ni msikilizaji mzuri, pia una tabia ya kuchukua summary.
 
Huyo kada alisema zaidi kuwa UFISADI LAZIMA UTAKIMALIZA CHAMA MBELE YA WATANZANIA WENYE HASIRA!! kwa sasa CCM wanafikiria kuachana na hao wagombea waliojitokeza na kuanza kutafuta mgombea asiye na jina halafu wampromote kwa muda uliobaki.Lakini akasema haitawezekana kwani kufanya hivyo kunahitaji mshikamano wa kweli ndani ya chama kitu ambacho hakipo.Huwezi kuamini mwana JF huyo kada alinidokeza kuwa chama kimechangayikiwa hadi walifikia kupendekeza NAPE wamsimamishe maana huyo hana kashfa ya ufisadi this is serious not a joke guys.
 
hiyo ni propaganda ya SISIEM kati ya hao hakuna hata mmoja atakayesimama,watamuweka mtu mwingine tofauti,so usichagulie watu mtu wa kusimamishwa
 
Huyo kada alisema zaidi kuwa UFISADI LAZIMA UTAKIMALIZA CHAMA MBELE YA WATANZANIA WENYE HASIRA!! kwa sasa CCM wanafikiria kuachana na hao wagombea waliojitokeza na kuanza kutafuta mgombea asiye na jina halafu wampromote kwa muda uliobaki.Lakini akasema haitawezekana kwani kufanya hivyo kunahitaji mshikamano wa kweli ndani ya chama kitu ambacho hakipo.Huwezi kuamini mwana JF huyo kada alinidokeza kuwa chama kimechangayikiwa hadi walifikia kupendekeza NAPE wamsimamishe maana huyo hana kashfa ya ufisadi this is serious not a joke guys.

Baeleze kuchanganyikiwa bado hakujafika hatua yake murua itakapofika kila mtu atanyanyua silaha kumpiga mwenzake wakidhani itasaidia...huku wengine tukisonga mbele kuwanyang'anya funguo za jumba letu......Chezea neno la mfalme wewe...Kama sauti tu iliangusha kuta sembuse hao wepesi wanaotegemea kalumanzila?
 
Leo nimeshangaa nilipopokea sms toka kwa kiongozi ndani ya ccm ikisema hivi:
"Tunasikitika kutangaza kifo cha CCM kilichotokea baada ya kuibuka kwa MOVEMENT FOR CHANGE (M4C). Marehemu atazikwa tarehe 31.10.2015.Habari ziwafikie mjomba wa marehemu CUF, Dada wa marehemu TLP, mdogo wa marehemu NCCR, na nyumba ndogo ya marehemu ADC, Pamoja na mafisadi wote wanaohusika na msiba huu popote walipo."
 
Back
Top Bottom