Ben Bella
JF-Expert Member
- Dec 3, 2019
- 529
- 1,856
Wakuu, naomba niende moja kwa moja kwenye mada.
Jana usiku nilitembelewa na mpenzi wangu nyumbani Kwangu mtaa wa Majengo, Dodoma.
Huyu mdada ni PS (Private Secretary) wa kigogo mmoja hivi wa wizara nyeti ya serikali hapa jijini Dodoma.
Wakati tumengia kitandani, akaanza kunisimulia stori ya kufurahisha sana ambayo imetokea hivi majuzi tu hapo ofisini kwao.
Stori yenyewe ilikuwa hivi;
Yeye (mpenzi wangu) alikuwa anampelekea boss wake (top official) wa wizara mafaili kadhaa ambayo ilibidi yasainiwe.
Alipofika ofisini kwa huyo kigogo alisukuma mlango akaingia ndani. Alimkuta boss wake yuko busy na simu ya mkononi akiwa anaangalia video.
Yule dada (PS) alinyooka direct hadi kwenye meza ya boss kitendo ambacho kilimshtua yule kigogo na kusababisha aiweke pembeni ile simu ili yule dada asiweze kuiona ile video. Kwa bahati mbaya hakuweza kuzima sauti mara moja na ndipo yule mpenzi wangu alipogundua kwamba sauti iliyokuwa inasikika toka kwenye huyo simu ilikuwa ni ya Tundu Lissu.
Aliweka mafaili mezani na kuondoka hapo ofisini haraka sana. Aliniambia kwamba hakuwa amemsimulia mtu yeyote isipokuwa mimi.
Nilistaajabu sana ila nilijifunza kwamba kumbe kuna vigogo wa serikali wanaofuatilia harakati za wagombea wa upinzani kama Tundu Lissu.