Pulchra Animo
JF-Expert Member
- Jun 16, 2016
- 3,398
- 2,990
- Thread starter
- #81
Ubaya unakumbukwa kuliko wema
My friend, that’s an oversimplified view of human behavior. Hakuna general formula inayoweza kuelezea behavior ya kila mwanadamu kwa usahihi, muda wote.
Mara nyingi binadamu akikuambia haki imetendeka sio lazima amaanishe kwamba haki imetendeka kweli. Anachomaanisha ni kwamba maslahi yake binafsi hayajaumizwa na hatua iliyochukuliwa. Pia, binadamu akikuambia fulani ni mbaya haina maana kwamba huyo fulani ni mbaya kweli.
Zipo scenarios nyingi za watu wanaohesabiwa ubaya kwa kutenda haki. Fikiria, kwa mfano, mwajiri aliyemfukuza mfanyakazi wake kwa sababu ya performance issues. Huyo mwajiri anaweza kuwa alifuata taratibu zote zinazohusika, lakini mfanyakazi hawezi kumuona huyo mwajiri wake kuwa alitenda haki; lazima atamuhesabia ubaya! Hata hakimu anayemhukumu mtu kwenda jela kwa kosa alilolitenda kweli, naye anahesabiwa ubaya.
Kwa kifupi, hawa watu waliohesabiwa ubaya kwa kutenda haki hawana uwezekano wa kupata msaada wa aina yoyote kutoka kwa wale walioumiziwa maslahi yao binafsi, hata kama wangepatwa na shida ya aina gani. They became enemies of the others just because they did what was just and equitable!