GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 56,516
- 108,791
Katika hali isiyokuwa ya kawaida kabisa nimeshangazwa kusikia kuwa aliyekuwa Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Klabu Bingwa nchini Tanzania ya Simba Sports Club Senzo Mbatha Mazingisa ameenda kuwa Mshauri Elekezi wa Mchakato wa kuelekea katika Mabadiliko ndani ya Klabu ya 'hovyo hovyo' duniani ya Yanga Sports Club.
Kwa Akili ya kawaida tu hivi unawezaje kuacha Kazi ambayo kwa kuwepo Kwako Simba SC kama CEO Wao tena huku Timu yenyewe nayo ikiwa na 'Mafanikio' na inazidi kuelekea katika 'Mafanikio' na unakubali kwenda katika ya Yanga SC ambayo hata tu 10% ya 'Mchakato' wake wa kuelekea katika 'Mafanikio' ya awali waliyonayo Simba SC bado hawajafikia?
Mliosoma sana na 'Werevu' mtanisaidia Kunielekeza hapa hivi kwa Senzo Mbatha Mazingisa aliyekuwa CEO wa Simba SC kuachana na Simba SC na hiyo nafasi na kwenda kuwa tu Mshauri Elekezi wa Yanga Sports Club kuelekea katika 'Mchakato' wake wa 'Mabadiliko' hapa amezidi Kujiongezea CV yake au ndiyo 'ameshaizika' rasmi CV yake 'Kaburini' na kuonekana ni wa hovyo hovyo tu?
Kwa jinsi nchi ya Afrika Kusini ilivyo na 'Maendeleo' sikuwahi Kudhani kuwa nao pia huwa wana 'Wasomi Mapopoma' huku maeneo mengine Afrika.