Kumbe hakuna chama kinaitwa CCM, CHADEMA, CUF, ACT Wazalendo wala NCCR Mageuzi?

Tulimumu

JF-Expert Member
Mar 11, 2013
14,304
12,965
Malisa GJ

Juzi TAMISEMI walitoa taarifa kuwa moja ya sababu za wagombea wa vyama vya upinzani kuenguliwa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa kwa 98% na kubakia 2% tu ni pamoja na kujaza kimakosa fomu za kugombea.

Moja ya makosa ambayo TAMISEMI waliyaainisha ni wagombea kujaza vifupisho vya majina ya vyama vyao badala ya majina kamili kama yalivyosajiliwa ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa.

TAMISEMI ilisema hakuna chama kinachoitwa CHADEMA bali kuna Chama cha Demokrasia na Maendeleo. Kwahiyo mgombea aliyejaza fomu yake akaandika CHADEMA automatically alikua amepoteza sifa. Vivyohivyo kwa wagombea wa ACT Wazalendo, NCCR Mageuzi, CUF na vyama vingine.

Lakini katika hali ya kushangaza hakuna mgombea hata mmoja wa CCM aliyekutwa na kosa la kujaza chama chake kwa kifupi. Yani kati ya wagombea karibu laki moja wa CCM nchi nzima hakuna hata mmoja aliyeandika CCM, bali wote waliandika Chama cha Mapinduzi. Sijui walipewa semina elekezi au wote walikua "magenius" wakajua namna ya kujaza fomu zao.

Anyway, hiyo sio hoja kwa leo. Hoja nayotaka kueleza ni ile aliyoeleza kaka yangu Dotto Bulendu kuhusu mkanganyiko wa majina ya vyama vya siasa. Dotto anasema Tume ya taifa ya uchaguzi (NEC) inavitambua vyama kwa majina ya ufupisho. Na hata kwenye document rasmi za Tume kama karatasi za kupigia kura utaona wametumia majina ya ufupisho kama CCM, CHADEMA, ACT wazalendo, CUF etc.

Sasa Comrade Bulendu anauliza, inawezekanaje taasisi mbili za serikali zitofautiane katika jambo moja? Yani NEC wanatambua kuna chama kinaitwa CHADEMA lakini TAMISEMI hawatambui hiko chama. Na wanasema hakuna chama kilichosajiliwa kinachoitwa CHADEMA au CUF au CCM. Kwa kifupi vyama hivyo havipo.

Je Kanuni za uchaguzi mkuu zinazoandaliwa na NEC na zile za uchaguzi wa Serikali za mitaa zinazoandaliwa na TAMISEMI zinapingana?

Je, sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 1992 inasemaje? Je ni kweli kwamba hakuna chama kinachoitwa CHADEMA au CCM au CUF au TLP?

Kama chaguzi za serikali za mitaa za miaka ya nyuma (2014, 2009, 2004 etc) zilitambua ufupisho wa majina ya vyama, kwanini mwaka huu iwe tofauti?

Halafu TAMISEMI inakaataaje kutambua vifupisho wakati yenyewe ni kifupisho?
 
Maajabu ya ujingaujinga wa ccm nikutudhalilisha watanzania wote yakuwa hatuna akili wala uelewa.

Tunaonekana mbumbumbu kwa vihoja vya viroja.

Aibu sana.
Majina CCM, Chadema,CUF na ACT ni majina halali kabisa yako kisheria kwenye katiba zao kifungu Cha kwanza Cha katiba zao .Jina ambalo haliko kwenye katiba ya Chama chochote ni jina ACT WAZALENDO Hilo jina haliko kwa msajili Kama jina liwe la kifupi au kirefu la Chama chochote.Jina la kifupi linalotambuliwa na msajili ni ACT sio ACT Wazalendo

Kwa mtu akiandika CCM au akiandika Chama Cha mapinfuzi Yuko sahihi au akiandika chadema au akaandika Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Yuko sahihi
 
Tuseme unakubaliana na hoja ya kukosea kujaza fomu-yaani unaandika CCM badala ya Chama Cha Mapinduzi. Ujazaji wa fomu zozote una maelekezo labda kiwe ni kitu kilicho wazi. Fomu zilitakiwa zionyeshe "Jina la Chama ...(andika kwa kirefu)". Unayo ona na kuyasikia ni mazingahombwe yanayo dhihirisha nia mbaya ya watawala.
 
Wako sahihi kabisa ndio maana hata ukijiita Mtanzania unakuwa umekosea ,wenzetu wa Zanzibar huwa hawafanyi hilo kosa,Kama unatoka bara wewe ni Mtanganyika na Kama unatoka visiwani wewe ni Mzanzibar,hakuna nchi inayoitwa Tanzania kama ambavyo hakuma chama kinachoitwa CCM,CHADEMA,CUF ,ACT ,NCCR NK.
Kwahiyo ukitaka kujitambulisha Mtanzania andika jina lililokamilika Tanganyika Zanzibar nia ya umoja
 
Naona malisa mchaga amekuja kuhanikiza chama cha kwao kwenye mbege

State agent
 
Uongo wake wote umejaa happy ukipoweka ACT wazalendo .Tume ya uchaguzi haojawahi chapisha karatasi ya kupigia kura wakati wowote yenye jina kuwa mgombea anatoka Chama Cha ACT wazalendo.Karatadi zote za kura hueleza wazi mgombea anatoka Chama Cha ACT.

Hawajawahi chapisha fomu yoyoye inayosema mgombea ni wa ACT wazalendo hakuna Chama chenye jina Hilo.Tume wanakijua Chama kinachoitwa kifupi ACT na siyo ACT wazalendo .Hilo la ACT wazalendo ni uongo wake wewe mleta mada,na bulendu wako
 
Karatasi ya za kupigia kura uchaguzi uliopita hizo hapo .Hakuna chama kilichoorodheshwa kinachoitwa ACT wazalendo .Chama ambacho kilitoa wagombea wake kinaitwa ACT.Ondoeni uongo wenu wa kusema chaguzi zilizopita tume ilichapisha karatasi za kura zenye jina la ACT WAZALENDO

1573210407661.png


hapo ni zanziba 2015

1573210473232.png

hapa ni Tanzaia bara 2015
 
Hivi kwani mgombea kuandika kifupisho kunamkoseshaje sifa ya kugombea ?
Inamkosesha tu kama kaandika kifupi cha jina ambalo haliko kwa msajili wa vyama vya siasa.Mfano msajili ana jina la chama kifupi ni ACT halafu mjaza fomu akiandika anagombea kupitia chama kinaitwa ACT WAZALENDO anatupwa nje ni sawa na mtu aandike kwenye fomu anagombea chama kinaitwa CUF LIPUMBA au CUF SEIF wakati msajili ana jina lenye jina la kifupi la CUF anatupwa nje
 
kama kulikuwa na sharti kwenye fomu la kuandika jina kirefu ACT watakuwa ndio walioumia zaidi sababu kule wamejaa ma ustaadhi kuandika kirefu JINA La chama yaani waandike ALLIANCE FOR CHANGE AND TRANSPARENCY

Sidhani kama hili ma ustaadhi wa ACT wanaliweza fomu zote lazima ziwe ziliharibika

CCM sio shida anaandika tu chap chap chama cha mapinduzi kafunga kazi
 
Tuseme unakubaliana na hoja ya kukosea kujaza fomu-yaani unaandika CCM badala ya Chama Cha Mapinduzi. Ujazaji wa fomu zozote una maelekezo labda kiwe ni kitu kilicho wazi. Fomu zilitakiwa zionyeshe "Jina la Chama ...(andika kwa kirefu)". Unayo ona na kuyasikia ni mazingahombwe yanayo dhihirisha nia mbaya ya watawala.
Mambo ya kijinga hayo kwa nini kanuni isiruhusu mgombea aliyekosea aenda ofisini arekebishe kabla orodha rasmi ya
ya wagombea haijatolewa
 
Mambo ya kijinga hayo kwa nini kanuni isiruhusu mgombea aliyekosea aenda ofisini arekebishe kabla orodha rasmi ya
ya wagombea haijatolewa
Vyote hivyo ni vigingi ambavyo hutegemei watu wastaraabu waviweke. Hakuna uwazi kabisa. Hiyo ndio CCM yetu, ya Polepole na Magu.
 
Back
Top Bottom