Kumbe Hadi Huku Poland Wanamjua Rais Magufuli

Metsada

JF-Expert Member
Mar 19, 2013
1,456
866
Wadau Nimekaa Mahali Fulani Hapa Mtaa wa Poznańska Street Katika Mji wa Warsaw Poland, Yani Wazungu Fulani Nikawaskia Wanazungumzia Tanzania Kwamba Hivi Sasa Ina Rais Mzuri Ambaye Anasimamia Vizuri Uwajibikaji Katika Masuala ya Fedha za Umma na Kuanzisha Elimu Bure.

Nikapata Hamu ya Kuwasogelea na Kuwauliza Iweje Wanaizungumzia Tanzania Hivyo, Wanaijua? Nikajibiwa Kwamba Wao (wako 9 wamekaa meza moja) wana kikundi chao walifika TZ mwezi April kwa ajili ya utalii na kwamba walipata fursa ya kuitembelea TZ na pia kutengeneza urafiki na baadhi ya watu na kwamba walifurahi kuona TZ inapiga hatua.

Kumbuka hawa hawakutembelea TZ nzima ila wanasema walienda Zenji, Kilimanjaro, Arusha na Serengeti. Kiukweli wanaisifu sana Tanzania pamoja na Rais JPM. Nimefurahi kuona Nchi yangu inazungumzwa vizuri na baadhi ya watu hapa Poland.
 
Je waliijua Tanzania kabla? Ili kuweza kutoa huo ulinganifu wa uongozi...
Wanasema wanafahamu Rais huyo alichaguliwa 2015 na kwamba anafanya kazi nzuri - wamezungumzia sana hili la udhibiti wa matumizi ya fedha za umma. Kwa upande wangu naona wanachosema ni kweli Mkuu. Mianya ya wizi wa fedha za umma imedhibitiwa kwa asilimia kubwa sana Kiongozi
 
Nabii hakubaliki nyumbani kwao. Vipi lile ongezeko la tozo sijui kodi ktk sekta ya utalii ilifutwa? Je hawa na wale Waisrael kadhaa hakuona gharama kubwa kama nao walilipia gharama iliyolalamikiwa tukaambiwa tutakosa watalii. Nauliza nipate majibu sijui muendelezo na matokeo ya lile saga.
 
Hapana Mkuu hawakulalamikia hayo maswala. Labda kama waliongea baada ya mimi kuondoka maana watu wa huku huwa wako careful na comments zao hasa wanapozungumzia Nchi nyingine - hawaropoki hovyo na kuponda. Wao huzungumzia mazuri zaidi.. kwa uzoefu wangu
 
Wadau Nimekaa Mahali Fulani Hapa Mtaa wa Poznańska Street Katika Mji wa Warsaw Poland, Yani Wazungu Fulani Nikawaskia Wanazungumzia Tanzania Kwamba Hivi Sasa Ina Rais Mzuri Ambaye Anasimamia Vizuri Uwajibikaji Katika Masuala ya Fedha za Umma na Kuanzisha Elimu Bure. Nikapata Hamu ya Kuwasogelea na Kuwauliza Iweje Wanaizungumzia Tanzania Hivyo, Wanaijua? Nikajibiwa Kwamba Wao (wako 9 wamekaa meza moja) wana kikundi chao walifika TZ mwezi April kwa ajili ya utalii na kwamba walipata fursa ya kuitembelea TZ na pia kutengeneza urafiki na baadhi ya watu na kwamba walifurahi kuona TZ inapiga hatua. Kumbuka hawa hawakutembelea TZ nzima ila wanasema walienda Zenji, Kilimanjaro, Arusha na Serengeti. Kiukweli wanaisifu sana Tanzania pamoja na Rais JPM. Nimefurahi kuona Nchi yangu inazungumzwa vizuri na baadhi ya watu hapa Poland.

Mimi Niko poland mwaka Wa 10 sasa hakuna mtaa kama huo

Hao wazungu watakuwa wale Wa pale Lumumba
 
Wewe hujui huko nyuma Tanzania ilikuwa inazungumziwa vizuri kila sehemu hata kama tulikuwa maskini.

Hawa viongozi wenu wameiharibu nchi yetu halafu mnajidanganya kujitekenya.

Magufuli kaua uchumi, nchi itaenda mbele vipi?
 
Wadau Nimekaa Mahali Fulani Hapa Mtaa wa Poznańska Street Katika Mji wa Warsaw Poland, Yani Wazungu Fulani Nikawaskia Wanazungumzia Tanzania Kwamba Hivi Sasa Ina Rais Mzuri Ambaye Anasimamia Vizuri Uwajibikaji Katika Masuala ya Fedha za Umma na Kuanzisha Elimu Bure. Nikapata Hamu ya Kuwasogelea na Kuwauliza Iweje Wanaizungumzia Tanzania Hivyo, Wanaijua? Nikajibiwa Kwamba Wao (wako 9 wamekaa meza moja) wana kikundi chao walifika TZ mwezi April kwa ajili ya utalii na kwamba walipata fursa ya kuitembelea TZ na pia kutengeneza urafiki na baadhi ya watu na kwamba walifurahi kuona TZ inapiga hatua. Kumbuka hawa hawakutembelea TZ nzima ila wanasema walienda Zenji, Kilimanjaro, Arusha na Serengeti. Kiukweli wanaisifu sana Tanzania pamoja na Rais JPM. Nimefurahi kuona Nchi yangu inazungumzwa vizuri na baadhi ya watu hapa Poland.
Fanyeni kazi ili msifiwe kama mnataka sifa ila sio mfanye ujinga alafu mtake sifa nzuri hao wazungu wana akili na sio ma bogus kama nyie
 
Hao walifika only attractive zone/areas sisi tunaoishi uswazi ndo tunajua kuwa hali ya maisha Tanzania ni ngumu mno. Mtu anakuja kukopa robo ya unga dukani huku anakupigia magoti kuwa maisha yake yako hatiani.
Watu wanakimbia familia kisa kodi ya nyumba.
Weeeee tz kuna maisha magumu kama kuzimu na kwasasa hakuna dalili ya nuru mbele kwa watu wengi.
Acha uCCM wako Magufuli kaiharibu Tanzania, licha ya mazuri aliyayafanya.
Mimi ni civil servant, najua maisha duni ya watumishi wa umma.
Pia ni mfanyabiashara mdogo, najua jinsi hali ngumu inayowakabili wafanyabiashara.
 
Fanyeni kazi ili msifiwe kama mnataka sifa ila sio mfanye ujinga alafu mtake sifa nzuri hao wazungu wana akili na sio ma bogus kama nyie
Labda kama hujawai kuishi Ulaya ... hata huku ma bogus kama wewe wapo wengi sana - watu mnaopenda kusikia mabaya tu, kusikia maafa tu, kusikia udhalilishaji tu - that's what you like to hear.
 
Unajua kila mtaa Poland?
Ndio hapo sasa.. yani watu wengine ni majanga. Hawajui why google maps ziliundwa- mtu unaweza ukaishi mji fulani hapa Europe na bado ukapotea kwa train (hii hutokea hata kwa wazaliwa wa hapa)...
 
Mimi Niko poland mwaka Wa 10 sasa hakuna mtaa kama huo

Hao wazungu watakuwa wale Wa pale Lumumba
M1-05.JPG

Poznańska Street
 
Back
Top Bottom