Kumbe dunia inajua viongozi wetu hodari kwa maneno? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kumbe dunia inajua viongozi wetu hodari kwa maneno?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Apr 1, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Apr 1, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  KATIKA kile kinachoonekana kama jibu la kwa nini Tanzania ni nchi maskini licha ya rasilimali nyingi ilizonazo tena miaka 50 baada ya uhuru, wataalamu wa masuala ya uchumi kutoka China na Vietnam wamesema, umaskini unaoikabili nchi yetu unatokana, pamoja na mambo mengine, viongozi kuwa na maneno mengi kuliko vitendo.


  Wakichangia mada mbele ya Rais Jakaya Kikwete ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mkutano wa 17 wa mwaka wa Taasisi ya Utafiti wa Kuondoa Umaskini Tanzania (Repoa), jijini Dar es Salaam juzi, wachumi hao ambao walikuwa wamealikwa kueleza uzoefu wao katika masuala ya kuondoa umaskini, walisema Tanzania haikupaswa kuwa nchi inayotegemea misaada kutoka kwa wahisani, bali ilipaswa kuwa inajitegemea.

  Akitoa uzoefu wake, Profesa Do DucDinh wa Taasisi ya Kimataifa ya Uchumi ya Vietnam, mbali na kukosoa mchakato mzima wa ubinafsishaji uliofanywa na Serikali ya Awamu ya Tatu ambao ulibinafsisha na kuua viwanda vingi vya msingi, alisema inasikitisha kuona

  Tanzania ina kila rasilimali lakini ni maskini wa kutupwa.

  Akizungumza huku Rais Kikwete akimsikiliza kwa umakini mkubwa, mtaalamu huyo alisema Tanzania imebinafsisha viwanda kiholela na matokeo yake viwanda vingi vimekufa na kuongeza kuwa, nchini Vietnam suala la ubinafsishaji lilifanywa kwa umakini na Serikali sasa inamiliki viwanda vingi ambavyo vinatoa ajira.

  Alitoa mfano kwa kusema kuwa, pamoja na kwamba Vietnam ni nchi ambayo haina kilimo cha korosho, inavyo viwanda vingi vinavyobangua korosho vikiwa vinapata malighafi kutoka nchi mbalimbali duniani ikiwamo Tanzania, huku akiishangaa Tanzania ambayo inalima korosho lakini imebinafsisha viwanda vya kubangua zao hilo ambavyo vingi vimekufa.


  Huku akihoji inakuwaje nchi inabinafsisha viwanda vinavyoongeza thamani ya mazao ya kilimo ambacho kinategemewa na asilimia 80 ya wananchi, mtaalamu huyo alionya kuwa, iwapo Tanzania inayo nia ya dhati ya kupunguza umaskini wa wananchi wake, basi haina budi kujipanga na kuikuza sekta ya kilimo kwa vitendo.

  Kwa upande wake, Profesa Li Xiaoyung wa Kituo cha Kimataifa cha Kuondoa Umaskini cha Beijing alisema maisha magumu yanayolalamikiwa na wananchi yanatokana na mfumuko wa bei, hasa wa vyakula na kutoa mfano wa ugali ambao ni chakula kikuu lakini bei ya unga ni kubwa kiasi cha wananchi wengine kushindwa kuimudu. Alisema alipokuja Tanzania mwaka jana alikuta kilo moja ya mchele ikiuzwa Sh1,200 lakini ameshangaa kukuta kilo moja ya bidhaa hiyo ikiuzwa Sh2,500 hivi sasa na kusema huo ni mfumuko wa ajabu.

  Mtaalamu huyo alisema mfumuko huo kwenye bidhaa za chakula ndiyo unaowasababishia wananchi umaskini kwa sababu ni bidhaa wanazozihitaji kwa matumizi ya kila siku, huku akisema sekta za mawasiliano na madini ambazo Serikali inatilia mkazo haziwezi kuwaondolea Watanzania umaskini kama kilimo hakitapewa kipaumbele.

  Kauli za wataalamu hao ni nzito na ndiyo maana tumelazimika kuzitilia msisitizo kwa kuzirudia kinagaubaga katika safu hii. Tunasema hivyo kwa sababu dhana na nadharia za maendeleo na za kufuta umaskini ambazo viongozi wetu walizirudufya kutoka katika sera za Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani (IMF), hazikutukwamua katika umaskini kwa kuwa hazikufaa kutumika katika mazingira tuliyomo. Bahati mbaya viongozi wetu walikosa ujasiri wa kuzikataa kwa hofu ya kunyimwa misaada ambayo hakika imetushika mateka kwa miaka 50 sasa tangu tupate uhuru.

  Sisi tunadhani wataalamu hawa wa uchumi wanastahili pongezi za dhati kwa kutufumbua macho na kutoa majibu kuhusu kwa nini nchi yetu bado ni maskini wa kutupwa licha ya utajiri mkubwa ilionao. Ni kweli viongozi wetu ni hodari zaidi kwa porojo kuliko vitendo na changamoto inayotukabili sasa kama taifa ni kuhakikisha tunapata viongozi wenye dhamira na uwezo wa kutukwamua katika umaskini na kutufikisha tunakotaka kwenda.

  Kumbe dunia inajua viongozi wetu hodari kwa maneno?
   
 2. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #2
  Apr 1, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  maji yakimwagika yanaweza kuzoleka?

   
 3. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #3
  Apr 1, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Watu tumesema san juu ya haya mambo lakini viongozi wetu hawaelewi somo nana sasa kiwanda cha urafiki nacho ndio nimekufa hivyo

  Kiukweli huwezi kubinafsisha viwanda ambavyo ndivyo vinavyo ongeza dhamani ya mazao,unauzaje viwanda ambao vimekuwa vikisaidia kuprocess raw materials na kupata goods na mwisho wa siku kuuza nje na kupata fedha za kigeni,haingii akilini kabisa,yaani mwl nyerere wakati ana anzisha viwanda hivi tumemwona ni mjinga kabisa,tusingelalama juu ya ajira ya vijana kama kweli viwanda vyetu vingekuwa vinafanya kazi

  Sielewi ni kwanini lakini hii nchi tajiri inahitaji kiongozi atakae jitolea kwa moyo kwa manufaa ya umma na kuweka mbari matakwa ya watu wa ulaya
  Umasikini wetu ni wa kujitakia na umeletwa na viongozi walio uza viwanda vyetu
   
 4. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #4
  Apr 1, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  10% zinatuangamiza na kukosa ubunifu wa jinsi ya kuendeleza viwanda hivi.
   
 5. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #5
  Apr 1, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Sikubaliani nawe kabisa ktk hili,hapa maji yanazoleka kwani viwanda vipo tunaviona ila wahusika wamebadirisha matumizi,kwa hiyo tunamwitaji kiongozi atakae rudisha viwanda hivyo mikononi mwa serikali pasi kumwangalia mtu usoni

  Rafiki yangu ukitaka kujua kuwa inawezekana hebu tumwazime nchi hii rais wa china na aiongoze kwa sheria za china,kila kitu kitakuwa sawa.tatizo la viongozi wetu wameweka mbere urafiki,jamaa na undugu na hii inawia ngumu kusimamia malengo ya serikali
   
 6. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #6
  Apr 1, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Kongosho
  Ubunifu tunao tatizo ni uzarendo haupo na kama uzarendo haupo lazima utakimbilia 10%
  Nenda pale morogoro kiwanda cha tumbaku kimeuzwa kwa bei ya chee sana tena san,wameuza mpaka nyumba za wafanyakazi bei chee kabisa na kiwanda kinaingiza pesa ya kufa mtu,wahusika pale mshahara unaanzia mil 12 kwa mabosi na kuwa bana walalahoi pesa mingi inaenda usa
  Pale tumbaku kuna eng fungo ni mbunifu wa hali ya juu,amekibadirisha kiwanda kwa kuweka design za ajabu pale
  Uzarendo hakuna,viongozi wanafanya mambo kama nchi si yao
   
 7. SALOK

  SALOK JF-Expert Member

  #7
  Apr 1, 2012
  Joined: Sep 20, 2011
  Messages: 2,681
  Likes Received: 870
  Trophy Points: 280
  Tanzania kuna kiongozi mmoja tu ambaye si vuvuzela, huyu anaweza kuwa tabibu mzuri wa gonjwa hili linaloikabili nchi hii, kwani ni mtu wa vitendo zaidi kuliko maneno! Amebobea ktk fani husika hivyo anakidhi vigezo vya kuikwamua nchi kutoka ktk janga hili la kujitakia! Hivyo ni wakati wa watanzania kumpatia mgonjwa wao (tz) daktari stahili kwa ugonjwa unaomsumbua! Vinginevyo hatutafanikiwa kamwe! Kwani wengine wote ni mavuvuzela hasa wa chama kile na kileee..!!
   
 8. G

  GABE100 Member

  #8
  Apr 1, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  na wao wlikuwa wanapoteza muda wao kumweleza kikwete. uwezo wa jk kutekeleza mambo ya kimaendeleo ni mdogo kama sio hamna kabisa
   
Loading...