Kumbe Dr Asha Rose Migiro ni chaguo la Kikwete! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kumbe Dr Asha Rose Migiro ni chaguo la Kikwete!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ngongo, Jan 25, 2012.

 1. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #1
  Jan 25, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Lazima nikiri wazi hizi ni "habari za mitaani". Leo nilikuwa katikati ya mji napata chakula cha mchana katika mgahawa maarufu Alshababu au kwa wasomali ndani ya vyumba vya uwanja wa michezo Sheikh Amri Abeid.Nimekaa katika meza yenye watu wanne siwajui hata mmoja isipokuwa navutiwa na mazungumzo yao.

  Mazungumzo yao yamejikita katika uchaguzi wa mwaka 2015.Wote wanakubaliana uchaguzi wa mgombea wa CCM tayari umeshaanza tangu mwaka 2011 najikuta nikijikaribisha mwenyewe bila kukaribishwa,nauliza ni kitu gani kimewaaminisha uchaguzi ndani ya CCM umeshaanza wote wanacheka mmoja anajibu unasikia Bwana hizi kelele za kuvuana gamba unafikiri ni nini kama siyo mkakati wa kumtafuta mgombea au wewe huko dunia ipi ?.Najianda kutoa majibu naambiwa na Kijana mwingine tulia Mzee unajua Kikwete mjanja sana anajua kundi la mapacha watatu lina nguvu kubwa sana na linaweza kuzuia chaguo lake ahaa naingilia kati kwani chaguo la Kikwete ni nani ?.Mzee mpaka leo hujui chaguo la Kikwete we mtanzania kweli kwa taarifa yako Dr Asha Rose Migiro Rais wako 2015.

  Mkakati wa Mwenyekiti wa CCM ni kupendekeza mgombea mwanamke "Safari hii ni mwanamke".Upo Mzee wataangaliwa wanawake wenye uzoefu mkubwa.

  [1] Anna Makinda Spika wa bunge la JMT,huyu atagaragazwa kwa skando la posho.Suala la posho kwa taarifa yako Rais analijua na alishalikubali kaamua kuliacha lilivyo ili kumuondolea sifa Makinda.Nauliza wapi mmepata hizi habari [Naomba source].Mimi mbunge wangu kanimbia kila kitu,vikao vya wabunge wa CCM suala la posho lilishapitishwa siku nyingi Mama wa watu kaachiwa kikapu.Hivi vikao vya CDM Magogoni nia yake kubwa ni kumdhalilisha spika asivyojua kazi yake vizuri.

  [2] Professor Tibaijuka Waziri wa Ardhi,huyu atagaragazwa na waZanzibar au hujasikia alivyoshutumiwa na waZanzibar Tanzania kujiongezea mipaka ya eneo la Bahari kuu.Mzee huu ni mkakati wa Kikwete kamtuma Jussu kupayuka maksudi auanataka kujifanya hujui Jussu alipewa ubunge na Kikwete hawa ni marafiki wakubwa wana mikakati yao siku mkishtuka Dr wake kashakalia kiti cha magogoni.

  [3] Dr Asha Rose Migiro Naibu katibu mkuu UN,huyu atapeta hana kashfa wimbo sasa ni zamu ya kina mama utaimbwa waTanzania kama kawaida yenu mtaupokea na kuongezea madoido.Mzee kwa taarifa yako huyu Mama kaambiwa ni lazima arejee nyumbani haraka wajumbe na warasimu wa CCM wamzoee mapema siku ngoma ikipigwa msijesema alikuwa wapi siku zote.Namalizia juice baridi tunaagana na hawa marafiki zangu wapya nafurahi uTanzania wangu namkumbuka Nyerere lugha ya kiswahili imetuunganisha waTanzania.Marafiki zangu wapya hatukuulizana dini wala makabila yetu.

  Mungu Ibariki Tanzania Mungu Ibariki Afrika na watu wake.
   
 2. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #2
  Jan 25, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Tanzania kuongozwa na Mwanamke!!! Sijui.

  Sio kama hawawezi bali mila za kiafrika zinakataa na wananchi wengi mpaka leo bado wanazo.

  Tuvute subra tuone.
   
 3. Root

  Root JF-Expert Member

  #3
  Jan 25, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 26,242
  Likes Received: 12,962
  Trophy Points: 280
  Hiyo ni kweli
   
 4. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #4
  Jan 25, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Mkuu Barubaru.

  Ni kweli lakini Tanzania kila kitu kinawezekana kikiwezeshwa ndiyo maana Anna Makinda ni Spika wa bunghe letu.


   
 5. M

  MAMENGAZI JF-Expert Member

  #5
  Jan 25, 2012
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 781
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Kama ni kweli basi watakua wamefanya kama wakati wanamchagua spika wa bunge, ili kumchomoa Six, wakaja na wimbo wa safari hii mwanamke, na kwa wimbo huu basi kuna mwanaume anaetaka kuchomolewa hapa. Hebu tusubiri
   
 6. k

  kuzou JF-Expert Member

  #6
  Jan 25, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 200
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  watu wanajifunza uraisi tanzania hivi hatuna ready made president jamani
   
 7. F

  Froida JF-Expert Member

  #7
  Jan 25, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Ajiandae tuu ni haki yake atakutana na majembe mengine ,Kama CCM wanadhani wanahati miliki ya kutawala milele ni hapo wakati utakapofika kwa sasa tujenge maudhui ya kuunda katiba yetu
   
 8. Kaliua urambo

  Kaliua urambo JF-Expert Member

  #8
  Jan 25, 2012
  Joined: Apr 21, 2009
  Messages: 606
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35

  njoo utusikilize na sisi tupo hamsini na sisi tunajua chaguo la watanzania
   
 9. Jagermaster

  Jagermaster JF-Expert Member

  #9
  Jan 25, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 656
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hii ipeleke Chitchat huko haina hadhi ya jukwaa hili
   
 10. g

  greenstar JF-Expert Member

  #10
  Jan 25, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 390
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  just a dream.....No ready made president? Wait for strong propaganda to be aired by wavuamagamba......vs......chandimu a.k.a CDM.
   
 11. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #11
  Jan 25, 2012
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 280
  jk anajua...na analijua hili tena vizuri sana kuwa ''asha-rose'' hawezi wa rais wa nchi hii....
   
 12. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #12
  Jan 25, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Mkuu Jagermaster,

  Ikitokea ikawa hivyo utaipeleka wapi ?.Haya ni mazungumzo ya mitaani lakini ukiyatakari kuna jambo zito ndani yake ndiyo maana hata mimi nikawa radhi kusikiliza na kuchangia.   
 13. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #13
  Jan 25, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Mkuu Kaliua urambo,

  Mnaweza mkawa hamsini au hata mia lakini akili zenu zikawa zero.


   
 14. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #14
  Jan 25, 2012
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
 15. spencer

  spencer JF-Expert Member

  #15
  Jan 25, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 2,792
  Likes Received: 1,337
  Trophy Points: 280
  Hivi nyie mnaomzungumzia huyu Asha-Rose Migiro mnajua asili yake ni nchi ipi?
  Je amekana uraia wa nchi yake lini?
   
 16. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #16
  Jan 25, 2012
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Kama hadhiti vile!

  Anyway tupe authority ya hao vijana ulikuwa unajadiliana nao kwanza alafu niambie kwanini nisiseme wewe hoja yako hapa juu ya Mapacha na magamba wala si lolote na si Rose Migiro!?
   
 17. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #17
  Jan 25, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Mkuu Spencer tafadhali tujuze uraia wake si wengine tunajua ni mTanzania mpare wa Mwanga.

   
 18. m

  masabuda Member

  #18
  Jan 25, 2012
  Joined: Dec 16, 2011
  Messages: 76
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ni mwisilamu mwenzake
   
 19. Kaliua urambo

  Kaliua urambo JF-Expert Member

  #19
  Jan 25, 2012
  Joined: Apr 21, 2009
  Messages: 606
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  kwa hiyo hao wanne wanaakili mia kwa sababu mnakula hotel moja,usisikilize maneno ya kahawani mkuu
   
 20. K

  Kisinga Member

  #20
  Jan 25, 2012
  Joined: Jan 18, 2012
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kila Mtanzania ana haki ya kugombea bila kujali huyu ni mwanamke au mwanaume, Katiba imeweka wazi haya mambo na hakuna mwenyehati miliki na urais wa nchi hii
   
Loading...