Kumbe Dowans ya United Arab Emirates siyo Costa Rica!- (Document) You decide

Hii sasa ni kizunguzungu.... Sasa hiyo Dowans HOldings SA ilisajiliwa wapi? Ilisajiliwa Costa Rica au United Arab Emirates (incorporated under the laws of UAE). Na kama hiyo SA kama tunavyoelezwa siyo kifupi cha South Africa bali Sociedad Associaone... au kitu km hicho sasa itasajiliwa vipi UAE?
Ukweli ni kwamba ishu nzima ya Dowans ni utapeli mtupu na si vingine! Na hii wengi wetu tulihisi na tulipata dalili nyingi but now its RAINING!! :A S 13:
 
Hivi pinda kaiona hii thread? Au je anaijua hiyo docs pls mkjj wape mwanahalisi waitoe hiyo docs ili tumsikie pinda
 
Hii ndiyo Tanzania....'nchi ya amani na utulivu'

Mafisadi wanajizungushia maneno na kukoleza akili za watanzania kama watakavyo...
Na tunaye Rais, Waziri mkuu, waziri wa mambo ya ndani, Nishati na madini, na watendaji wengine.....ndiyo serikali....!
nadhani afadhali tujisemee tu wazi kuwa HAKUNA UONGOZI TZ....ndiyo maana haya yote yanafanyika...ina 'tuna amani na utulivu' tusiulize lolote, tunayataka wenyewe! na haya ni machache tu maana nchi hii ina wizara takriban 30 an ushee, na kila wizara 'ulaji uliopo, ni kila waziri analijua lake...JK kwatu!!

akiibuka mtu akaanza kuwaeleza watanzania walio usingizini mambo haya anaitwa mchochezi, mhaini.
 
Hii sasa ni kizunguzungu.... Sasa hiyo Dowans HOldings SA ilisajiliwa wapi? Ilisajiliwa Costa Rica au United Arab Emirates (incorporated under the laws of UAE). Na kama hiyo SA kama tunavyoelezwa siyo kifupi cha South Africa bali Sociedad Associaone... au kitu km hicho sasa itasajiliwa vipi UAE?
Ukweli ni kwamba ishu nzima ya Dowans ni utapeli mtupu na si vingine! Na hii wengi wetu tulihisi na tulipata dalili nyingi but now its RAINING!! :A S 13:

bado kidogo tu atakuja pinda na machozi analia akisema dowans ni ishu ya usalama wa taifa.
 
Sura ya swala la Dowans Tanzania kwa kweli ni moja ya mfano wa nguvu sana kwa udhaifu wa power ya wananchi. Watanzania kweli tumekuwa tuna sua sua na kungoja eti someone else atatusadia kutatua haya maswala yetu. CCM sio chama cha huruma wala kusijisikia vibaya hata mara moja. Tumeona comments za Kikwete na ccm crew kutoona ubaya wa Dowans na mikataba mingine ya ccm. Hasara ya ccm Tanzania ni kubwa zaidi wakiendelea kukaa Ikulu.

Uongo wa Kikwete na ccm hata mara moja hautabadilika kuwa ukweli. CCM ni sawa na ugonjwa wa TB
 
bado kidogo tu atakuja pinda na machozi analia akisema dowans ni ishu ya usalama wa taifa.

Suala linalohusu mafisadi na ufisadi linahusu Usalama wa taifa. Suala linalohusu CCM na sera zake linahusus amani na utulivu. Suala linalohusu umasikini wa wananchi ni kuwachonganisha wananchi na serikali, suala linalohusu rasilimali za tiafa ni uchochezi unaopelekea kumwaga damu.
 
Technology kwani nani kazuia kusiwepo umeme Tanzania? Serikali nzima ni CCM - Rais wao, sera zao, sheria zao viongozi wao, watendaji wao kila kitu chao. Wanashindwa nini kutatuta tatizo? Kama tatizo ni umeme tu kinawashinda kitu gani kulitatua unless ni viongozi waoga, wasiojiamini na wasio na uthubutu wa kuchukua hatua zinazopaswa.

Mwanakijiji umemvua nguo Technology kabisa ameonekana anakiwango cha juu kabisa cha Ujinga! Bora angenyamaza tu,inasikitisha sana unatumia jina zuri la Tecnology wakati wewe mwenyewe ni Mbumbu kabisa
 
Hii nchi sijui tunaelekea wapi. Wamesahau kutatua matatizo ya aina hii na mengine mengi mengi yanayowatatiza wananchi badala yake wanaangalia namna ya kumdhibiti Dr. Slaa na chadema. Shame on them.
 
Na bado wapo Watanzania wenzetu wengi wa kawaida kabisa ambao wanaumizwa na haya yanayotendwa na serikali hii lakini wanajitokeza kufua mbele kuitetea serikali ya CCM na kujibu kwa kebehi wale watu wanaojitoa kwa hali na mali na akili zao kutujulisha Watz yanayojiri ili tuzinduke. Lazima tumerogwa sisi Watanzania,maana wenzetu wote hawako hivi.
 
Kuna tatizo lipi Dowans ikiwepo UAE, Costa Rica, Tanzania na kwingine kokote?
 
:A S 13::A S 13::A S 13: MMkijiji unataka kuleta uchochezi katika serikali yetu kwanini kila siku unakuja na madocument yasiyo na mbele wala nyuma???:A S 13::A S 13:
 
Mwanakijiji, naomba kutoa wasiwasi wangu juu ya uhalisia wa document hii (isije ikawa umepewa fake document ili uonekane hauko makini, unakumbuka kilichotokea kwa Dr Slaa Shinyanga juu ya kifo cha Balele???).

Kabla sijatoa mchango wangu naomba kwanza kuthibitishiwa uhalali (Authenticity) wa hii attachment, nachelea kusema kuwa ni fake kwani bila hivyo basi wale wote walioshiriki kuiwakilisha Tanesco kwenye case ya ICC na wakashindwa watangazwe kuwa ni incompetent na wasiruhusiwe kufanya kazi za uwakili.. WAFUTIWE LESENI ZAO ZA UWAKILI NA WAFILISIWE
 
:A S 13::A S 13::A S 13: MMkijiji unataka kuleta uchochezi katika serikali yetu kwanini kila siku unakuja na madocument yasiyo na mbele wala nyuma???:A S 13::A S 13:

Muulize uliye naye kwenye Avatar yako!
 
Back
Top Bottom