Kumbe Dowans ya United Arab Emirates siyo Costa Rica!- (Document) You decide

kwakweli tumekuchoka na ideas zako unazotumwa na mabwana zako za uchochezi.... tunachohitaji ni umeme....

Kamwambie EL kwamba kwakuwa sasa amerudi ulingoni kupitia mlango wa kamati tena ya mambo ya nje basi awafuate tena wale washikaji zake wa Thailand waje na mvua zao za kubumba wazinyeshe pale mtera then utapata umeme.......
 
Mh hivi kamati ya akina Mwakyembe ilisema nini kuhusu DOWANS? Ilieleza uhalali wa kampuni hii ama wao walijikita katika RICHMONDULI peke yake?????
 
kizungumkuti cha wizi wa kutumia viongozi vibaraka ,mbumbumbu ,wazandiki na waliokosa uzalendo.
 
Tanzania tunachotakiwa ni ku-take stand kwa hawa wezi wa mchana. Nashindwa kuelewa hata wanasheria wetu walioko pale wizara ya sheria hakuna hata mmoja aliweza kutambua huu ujinga. Everything is possible in Tanzania, hata kuwaibia watanzania wakiwa hawako usingizini inawezekana.
 
Kamwambie EL kwamba kwakuwa sasa amerudi ulingoni kupitia mlango wa kamati tena ya mambo ya nje basi awafuate tena wale washikaji zake wa Thailand waje na mvua zao za kubumba wazinyeshe pale mtera then utapata umeme.......
hakuna kitu kama hiki na hawezi ule ulikuwa ni ulaji mwingien tu, shame on these guys!!
 
Tanzania tunachotakiwa ni ku-take stand kwa hawa wezi wa mchana. Nashindwa kuelewa hata wanasheria wetu walioko pale wizara ya sheria hakuna hata mmoja aliweza kutambua huu ujinga. Everything is possible in Tanzania, hata kuwaibia watanzania wakiwa hawako usingizini inawezekana.
wanajua kila kitu na inawezekana wanapata au wameahidiwa fungu hapa
 
Technology kwani nani kazuia kusiwepo umeme Tanzania? Serikali nzima ni CCM - Rais wao-CCM, sera zao- CCM, sheria zao- CCM viongozi wao-CCM, watendaji wao-CCM kila kitu-CCM . Wanashindwa nini kutatuta tatizo? Kama tatizo ni umeme tu kinawashinda kitu gani kulitatua unless ni viongozi waoga, wasiojiamini na wasio na uthubutu wa kuchukua hatua zinazopaswa.

Mwanakijiji naona umemmaliaza huyu anayeijita Technology...sijui ni kwa nini hakutumia avatar yake hata kutoa chembe ya suluhisho la umeme kama watu wake (kama anao huko ccm) wameshindwa... wakati mwingine hawa akina Technology si wa kujibiwa maana inaonekana wanataka nchi iendelee kuliwa mpaka ibaki mifupa... Kwa sasa Tanzania yetu bado ina minofu sehemu sehemu lakini mafisi wako ngangali sana kuitafuna.. inabidi akina Technology waamke kabla Tanzania haijawa mifupa na kutupwa barabarani maana wakati huo ukifika sijui Technology atakuja kusema nini.. Ewe technology acha kukatisha wengine tamaa kama wewe umeamua kukaa na kusubiria solution ya umeme...
 
Kamwambie EL kwamba kwakuwa sasa amerudi ulingoni kupitia mlango wa kamati tena ya mambo ya nje basi awafuate tena wale washikaji zake wa Thailand waje na mvua zao za kubumba wazinyeshe pale mtera then utapata umeme.......

Ah! kaachana na mvua zisije muunganisha Richmond/Dowans. Sasa amekuja na ushauri wa kuongeza mishahara hata kama inflation itafikia 100%. Ile kamati ya Ntukamazina taarifa zake aliondoka nazo na zipo Monduli, na ni huyu huyu aliagiza vijana wamshughulikie (Tucta) Mkoba kwa virungu na mabomu. Ni smart kapita uani na sasa yupo stejini.
 
When lies confound even the liar..........................................we are tired of these thieves.................
 
Duh Mwanakijiji, hii ya majina ni ONE THING lakini hii ya tarehe mbona na yenyewe ni babu kubwa ? Iliwezekana namna gani TANESCO kuingia mkataba na Richmond Development Company LLC tarehe 23/ 6/ 2006 wakati ambao Richmond imeshakabidhiwa kwa Dowans tarehe 21/ 6/ 2006 kwa barua Ref. DOW/4000/1016/TANESCO ?
 
mkuu mwenzangu nadhani hapa wenyewe wana confuse tu:

a. Original contract kati ya Richmond na Tanesco ndio ulioingiwa June 23, 2006 (wakati huo hatukujua kuna Dowans - japo ilikuwepo tangu angalau 2005.

b. Baada ya Richmond kushindwa kuingiza mitambo ikaamua kuhamisha mkataba kwa kampuni nyingine;

c. Ili kuweza kuhamisha kwa kampuni nyingine ndio Tanesco ikatoa idhini yake Disemba 21, 2006 ya kuhamisha mkataba wake na Richmond uliosainiwa June 23, 2006 kwenda kwa Dowans.

d. Disemba 23, 2006 Tanesco ikaingia mkataba na Dowans Holdings S.A (ya Costa Rica???)

e. March 16 ndio tunaona mkataba huu tena...

f. March 17 Dowans Holdings S.A inahamisha majukumu yake kwenda kwa Dowans Tanzania Limited (kama nakumbuka vizuri).

Ni kama movement ya kufunga goli moja zuri kabisa. Mpira unaanzia kwa goli na hakuna mchezaji wa timu ya upinzani anayeugusa hadi goli..
 
Inanikumbusha kisa cha mkulima na wezi wa maboga shambani kwake..baada ya kubaini kuwa kuna mwivi anachuma maboga yake aliamua kuweka tangazo kwamba boga moja limetiwa sumu,ili kuharibu shughuli mwivi akaweka nae tangazo kua maboga mawili yametiwa sumu! hivyo kumchanganya hata mwenye shamba!
Maana yangu ni kwamba baada ya kubaini janja yao imebainika,Serikali (mwenye shamba) ilitafuta namna ya kujinasua kwa kuleta kwa makusudi kabisa utata wa nani ni mmiliki wa DOWANS...km navyofikiri ndivyo basi kuna namna mawasiliano baina ya waficha ukweli na wanaofichiwa ukweli hayakwenda sawa na matokeo yake ni hizi kampuni tata zilizosajiliwa sehemu tofauti tofauti!
 
PHP:
Duh Mwanakijiji, hii ya majina ni ONE THING lakini hii ya tarehe mbona  na yenyewe ni babu kubwa ? Iliwezekana namna gani TANESCO kuingia  mkataba na Richmond Development Company LLC tarehe 23/ 6/ 2006 wakati ambao Richmond imeshakabidhiwa kwa Dowans tarehe 21/ 6/ 2006 kwa barua Ref. DOW/4000/1016/TANESCO ?

Dowans wenyewe kwenye kesi yao na Richmond kule Texas walisema hawana kampuni tanzu...sasa hii ya Dowans Arabisc na Dowans Costa Rica zinatoka wapi??????????????????????????

Nionavyo Rostam Aziz na JK ndiyo wanaocheza huu mpira na mmiliki wa Richmond na hizi Dowans ni yule yule..................................
 
Duh Mwanakijiji, hii ya majina ni ONE THING lakini hii ya tarehe mbona na yenyewe ni babu kubwa ? Iliwezekana namna gani TANESCO kuingia mkataba na Richmond Development Company LLC tarehe 23/ 6/ 2006 wakati ambao Richmond imeshakabidhiwa kwa Dowans tarehe 21/ 6/ 2006 kwa barua Ref. DOW/4000/1016/TANESCO ?

Halafu tunatakiwa tuamini tu ili tusonge mbele bila kuhoji
 
Mzee Mwanakijiji elewewa siku hizi makampuni ya kiunjanja ujanja yanakuwa na vijikampuni vingi ili yakifanya blunder huwezi kuya trace.
 
Pandora Box imeshafunguka, basi ni mshikemshike kila kona na kila uchao. Haya na tuendelee.........
 
MKJJ,

Nadhani nchi nzima inahitaji metanoia. Kuanzia kwa Rais mpaka sisi raia wa kawaida. Hakuna njia utaweza kuelezea matukio yanavyokwenda hapa Tanzania, viongozi wanajisemea na kujitendea tu huku raia tunaumia na kulalamika bila kujua cha kufanya. Kina Slaa wanajitutumua kwa nguvu zao kidogo dola inawaandama pamoja na wapinzani wenzao.
 
we are tired with your stories na majungu, tunachohitaji watanzania ni umeme na si SIASA. wanaoukutuma waambie tumechoka na hadith tunahitaji umeme. akina sitta na mwakyembe wako wapi??? wametukimbia tumebaki na mateso ya umeme

Wacha upuuzi wa kifisadi umeambiwa mwanakijiji ndiyo anatoa umeme si Ngeleja na Kikwete wamekalia ufisadi na kuifanya Tanzania kuwa gizani wangekuwa wanataka kuleta umeme wasingetuletea mikataba ya kifisadi :A S 112::A S 112::A S 112:
 
Sipendi kuwa mjinga, sipendi kuonekana mjinga, sipendi kuchukuliwa mjinga. Ninakataa kuwa mjinga. Kama Rais Kikwete hawajui wamiliki wa Dowans basi na Papa hajui Vatican ilipo! by MM
 
Back
Top Bottom