Kumbe CHADEMA haina imani na Zitto! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kumbe CHADEMA haina imani na Zitto!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mtu wa Pwani, Nov 29, 2007.

 1. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #1
  Nov 29, 2007
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Kumbe CHADEMA haina imani na Zitto!

  Tambwe Hiza aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chama cha Wananchi (CUF), lakini kwa sasa ni kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Naibu Mkuu wa Kitengo cha Propaganda na Uenezi cha CCM.
  http://www.freemedia.co.tz/daima/2007/11/28/makala4.php
   
 2. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #2
  Nov 29, 2007
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  .........................by Tambwe Hiza
   
 3. M

  Mkandara Verified User

  #3
  Nov 29, 2007
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Tambwe Hiza,
  Ni matumaini yangu ndugu Hiza unapitia ktk kijiwe kama wanavyofanya wengine. Makala yako imebeba mtazamo wako na dhana ambazo umezijengea tuhuma bila wewe mwenyewe kuwa na Uthibitisho. Ni rahisi kunyooshea watu kidole na kudai ushahidi wakati hayo uyasemayo wewe hayana ushahidi isipokuwa habari za kuokoteza ktk magazeni na vijiwe.

  Kiswahili ni lugha nyepesi sana na ikiwa utakuwa ukitafsiri vitu kwa mtazamo huo basi mjomba una kazi kubwa mbeleni na hasa ktk shughuli ulizojihusisha nazo.

  Maelezo yako yamejijenga sehemu moja KUJIKOSHA ama kwa kiswahili cha kizamani tunasema KUJIPENDEKEZA kwani umeyaona mabaya sehemu moja tu bila kujali uzito wa tuhuma ama lawama hizo.

  Lini umeona Tuhuma zikitanguliwa na uthibitisho?.... hata jambazi linapokamatwa huanza na tuhuma kisha ukafanyika Upelelezi wakafuatwa baadhi ya watuhumiwa na sio wananchi wote pasipo kuwepo ushahidi wa kutosha kuweza kumweka mtuhumiwa chini ya Ulinzi. Ni huo Upelelezi ndio utakuja vumbua ushahidi tosha wa Kulifikisha jambazi mahakamani, haiwezekani vinginevyo..

  Hiyo misingi ya kusingiziana kama ulivyosema hutokea tu ikiwa serikali itapuuza tuhuma hizi kwa madai ya ushahidi jambo ambalo haliwezi tokea kwa aina yeyote ya kesi duniani. Waziri wa Fedha mama Meghji mwenyewe alipoingia Kisha kubali kuwepo kwa ubadhilifu wa fedha, sasa without suspects ataweza vipi kujenga hoja ya kuanzisha uchunguzi?.

  Ulichoweza kukiona vizuri ni toka Upande wapili tu! Upande wa Chadema ambako kwa lugha yako mwenyewe umeonyesha kuzua tuhuma ambazo hazina uthibitisho kwani mgongano wa mawazo baina ya wanachama haina maana kabisa ni kukosekana kwa imani kati yao.

  Unapomkataza mkeo kutoshiriki ktk vikao vya majungu haina maana huna imani na mkeo isipokuwa huna imani na aidha wahusika ama vikao hivyo.

  Pili, Ukimkataza mwanao kutotembea na kundi fulani la watu haina maana huna imani naye isipokuwa huna imani na hao vijana wenziwe...na mabishano yoyote kati yako na mwanao hayana maana kuwa kuna kutokuelewana ndani ya nyumba.

  maelezo yako yote ni CCM against the REST.. yaani hata maoni ya WANANCHI umeyaweka chini na kutanguliza maslahi ya chama CCM hata kukiweka kuwa kina maadui..CCM ina maadui hii lugha gani kwa mwanasiasa kuweza kuitumia hasa pale wananchi wanapodai haki yao. Leo unawaona Chadema kama Wapinzani, sintashangaa kesho ukianza kuwaita Chadema ni maadui wa CCM.

  Pole mjomba, katika zizi la CCM bado kabisa hujapata barehe yani wapo wanaume wanaoweza kuonekana umaarufu na wala Umaarufu hautafutwi kwa njia hizi.
   
 4. H

  Hume JF-Expert Member

  #4
  Nov 29, 2007
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 338
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 45
  Hapo mzee Mkandara umenena,
   
 5. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #5
  Nov 29, 2007
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Heshima yako mkuu wangu,

  Bob unazidi kunifanya niamini kuna vipaji vingi tu Tanzania.Duh,maneno mazito hayo mkuu wangu
   
 6. M

  Mugo"The Great" JF-Expert Member

  #6
  Nov 29, 2007
  Joined: Oct 7, 2007
  Messages: 263
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Ndugu Tambwe, Title yako ni Vague haiko specific in relation to the main body of your article" Umejaribu ku-widen the net katika harakati zako za propaganda dhidi ya vyama vya upinzani. Nimejaribu kuchambua hoja chache tu kati ya mengi uliyoeleza, watanzania wenzangu wataongezea au kupunguza katika niliyoyasema na pengine kuzi-dissect hoja zako ambazo mimi sikuzigusia.


  Marais wa nchi nyingine huwekwa kitimoto hata kama wapo madarakani( refer to Clinton Vs Lewinsky saga). Sembuse ya huyu Mkapa kuhusishwa na matumizi mabaya ya madaraka akiwa madarakani, tena ambayo yanaendelea ku-cost Watz dearly.

  "Enzi za chama kimoja, ilikuwa ni utawala msonge, habari nyingi zilikuwa zinafichwa, lakini katika Dunia hii ya utandawazi plus watu walioko kwenye system kuchoshwa na Muungwana na Team yake, ndiyo maana imekuwa rahisi zaidi kupata "Classified" information ambazo nyingi ni mikataba mibovu kabisa ambayo haijawahi kutokea. Marais wa nchi zenye kujua nini maana ya uwajibikaji hujiuzulu pindi wanapotuhumiwa sembuse mawaziri wa Danganyika. Haihitaji shule kubwa kujua kuwa uchumi wetu upo taabani, na labda wakijiuzulu hali itaboreka zaidi kuliko ilivyo sasa."

  Mr. Tambwe, umeonyesha unazi wa waziwazi, Hivi kweli hizo "Classfied information" unaziita "Mabomu ya wapinzani" Je, Machunde amekanusha kuwa si mwajiriwa wa Karamagi? Kashfa ya RADA unaiita mabomu wakati inawagharimu watanzania maskini. Please be serious and fair. Vyama hivi vitakuja na kupita lakini Generation ya watanzania is there to stay. Usiandike tu ili upate mkate wa leo bila kujali your grandchildren. Jitihada za kujikwamua kiuchumi haziwezi kufanywa na kutekelezwa na watu selfish ambao kila kukicha wanafikiria kuanzisha "Multi-billions projects" kwa ajili ya kushibisha matumbo yao. Was it fair to privatize NBC kwa bei ya kununua peremende? Umeona wenzetu wanavyoona mbali baada ya kuinunua, wameiuza NBC kwa faida kubwa. Na haya kwako ni mabomu. Uchumi unakuzwa kwa sera bora, mikakati na nia ya dhati na ya kizalendo ya kuitekeleza mikakati hiyo na siyo kuiingiza nchi kwenye mikataba kama ya Richmonduli.

  "Imani ya wananchi kwa Bunge imepungua sana, tatizo limebaki kwenye katiba. Tume ya uchaguzi wakati hu-play role kubwa sana kwenye maamuzi ya kura. Hivyo, hadi hapo tutakapokuwa na tume huru ya Uchaguzi,bunge letu litaendelea ku-rubber stamp mikakati ya serikali hata kama inaua nchi.Hivi mwananchi ni nani? Unajua hata Watu wanaovujisha siri toka sirikali(ni) ni wananchi, tena wazalendo. Hapa ndipo naifagilia JF kwa sababu inatoa nafasi kwa watu kama hao kuendelea kuianika Serikali wanapoona Walalahoi hawatendewi haki."


  Hapa suala si ushindi kwa nani, hoja ni accountability kwa watanzania waliompa dhamana. Kumbe wewe upo kwenye dunia ya nani mshindi hata kama ushindi huo una madhara kwa Taifa. Kweli tuna safari ndefu sana katika kufikia maisha bora.


  "Usipotoshe umma wa Tanzania,nchi haiko kwenye mikono ya JK peke yake, imo mikononi mwa watanzania wote ila JK amepewa jukumu la kuwaongoza. Sasa hawezi kuachiwa peke yake 'ETI KWA KUAMINI NCHI IKO KWENYE MIKONO SALAMA'. JK ni binadamu kama tulivyo wengine, anaweza kukosea kama wanavyokosea wengine. Unless unataka tuamini kuwa ana uwezo usio wa kawaida ulio juu ya Watanzania wengine.Naona kweli umepania, unaanza hata kumpigia debe ili achaguliwe 2010?"
   
 7. Kitila Mkumbo

  Kitila Mkumbo Verified User

  #7
  Nov 29, 2007
  Joined: Feb 25, 2006
  Messages: 3,347
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Huyu bwana alimwanika Tambwe uchi kabisa kiasi kwamba kama Tambwe angekuwa na akili ya binadamu wa kawaida asingerudia kuandika ujinga huu. Hebu soma hii makala hapa.
  _____________________________________________________

  Mkapa anapochuuzwa na kina Hiza


  Nkuzi Kwanzi

  KWA aliyesoma utumbo wa mtu anayetapatapa kwa kujifanya msemaji wa Rais mstaafu Benjamin Mkapa, aitwaye Tambwe Hiza, atakuwa amesikitika na kuwashangaa Mkapa na Hiza.

  Licha ya utetezi wake kuwa mfu na usio na mashiko, ni tahadhari kwa Mkapa kuwa kama hatakuwa makini, waganga njaa watamtumia wakijionyesha wanampenda, kumtetea na kumjali ilhali ukweli ni kwamba wanapaza sauti ili awasikie na awatupie makombo.

  Hakuna mtu aliyetapatapa kipindi hiki kama Hiza. Alianza na kuvizushia vyama vya upinzani huku akijirejesha kundini alikokuwa kwa kulamba matapishi yake.

  Hakujua kuwa CCM waliishaistukia janja uchwara ya wachumia matumbo na matapeli wanaohama hama vyama kukidhi njaa zao.

  Kutokana na usuhuba na Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba, Hiza na makapi wengine walifinyangiwa ofisi na idara ya uani ya propaganda!

  Jaribio la kuuza machukizo ya kundi hili wakati wa kutapatapa kutetea bajeti mikoani, waliishia kuzomewa.

  Hiza hakuchoka kuusaka mkate na kuridhisha wasitiri wake. Aligombea ujumbe wa NEC na kubwagwa kama taka. Ameona hii janja ya nyani kutofanikiwa, amedandia utetezi mfu wa Mkapa.


  Kwa mtu mwenye akili timamu na hekima na anayemjua Mkapa vizuri na zigo la madhambi yake, hawezi kupoteza muda wake kutaka kufanya muujiza wa kumsafisha.

  Hiza ni nani akilinganishwa na vigogo kama Daudi Mwakawago, Jaji Mark Bomani, Joseph Butiku na watu wengine wenye majina na waliomuonya Mkapa kuwa anachojaribu kufanya ni kujichimbia kaburi na hakistahili kufanywa na mtu wa nafasi yake?

  Watetezi wa Mkapa wanamdhalilisha sawa na wapambe wa utawala wa sasa wanavyousukumizia motoni. Hakuna kitu kibaya kama kumdanganya mtu. Maana ni kumfanya mpumbavu.

  Kibaya zaidi ni kudanganya nawe ukajidanganya. Adui yako kweli muombee njaa. Hiza anajifanya kama Mtanzania aliyekuwa ughaibuni wakati ukweli kuhusu Mkapa ukiwekwa njia panda ili kila mpita njia ajionee na kuhukumu.

  Hiza ataleta jipya gani iwapo akina Kingunge, Makamba, Mwanri, Warioba wamechemsha? Hiza anajua nini zaidi ya kuendeshwa na mkuno wa njaa tumboni?

  Bahati mbaya CCM nayo imekula hasara. Maana kama kuna fasheni inayotumika kuiibia na kuitapeli si nyingine ni watu kuhama vyama au taaluma zao tayari kupewa kazi ya kuzoa uchafu wake wasiuweze. Dawa ya yote haya ni kusafisha nyumba yako na kuwa msafi.

  Hiza asiyejua hata kujenga hoja zaidi ya kulalamika na kusifia, ana msaada gani kwa Mkapa iwapo ameshindwa kujisaidia mwenyewe kiasi cha kusaidiwa kwa njia ya kudhalilishwa? We Hiza we, tafuta njia ya uhakika ya kuishi na siyo salata na urongo.

  Hata bata bingwa wa kuchokoa taka huwa halali chooni wala kujisifia matendo yake. Yeye kama hayawani hana jinsi. Hayo ni majaliwa yake. Nepi siku zote ni nguo ya aibu si vizuri kujisifia unepi wala fisi mpenda mizoga hajisifii ufisi wake. Hiza ni mahuluku wa ajabu anayeonekana kuendeshwa na njaa kiasi cha kuvuka mipaka!

  Na hili inabidi liwe somo kwa watawala wasio waadilifu. Ufisadi unamtoa mtu utu na heshima kiasi cha kutetewa na majambazi wa kisiasa. Tangu lini kuku akamtetea mwewe hata ahaidiwe kutoliwa vifaranga vyake? Visipoliwa vyake vya wenzake vitaliwa. Je, kuna usaliti mchafu kama huu?

  Mkapa kwa kutetewa na vyangu wa kisiasa, anazidi kumomonyoka na kuonekana mhalifu japo hataki aeleweke hivyo. Hakanushi wala hata kuwakemea kimya kimya huko wanakokutana kama wanakutana.

  Je, Mkapa anawatuma akina Hiza kufanya kazi chafu kwa ajili yake au wanajikomba na kujipendekeza ili lau waambue makombo? Kama ni mkakati, basi umeshindwa hata kabla ya kufanyiwa kazi.

  Hivi nani anadhani Watanzania ni majuha na wendawizimu kumsikiliza au kumwamini kiumbe asiyejiamini wala kuamini anachosema? Nani mpuuzi amuamini mkaanga sumu na majungu.

  Hiza anadhani kuwa alipokuwa Mbeya hivi karibuni alijivua nguo hadharani kwa kukiri kuwa alikuwa mpika majungu mkuu alipokuwa CUF? Je, ameokoka lini kuacha kilema hiki cha akili hadi tumwamini?

  Mkapa, kwa viwango vyovyote ni msomi, hata kama elimu yake aliitumia vibaya. Tangu lini msomi akatetewa na mbumbumbu mzungu wa reli? Ni ajabu kipofu kumtetea mwenye macho au shehe kutetewa na mlevi! Hii inazidi kumfanya Mkapa aonekane si Mr Clean kama tulivyoaminishwa.

  Wazungu husema ‘show me your friends I will tell you who you are’. Na Mkapa japo amekataa kujitetea, bado hajahukumiwa kiasi cha kutetewa na vibaka na wasaka mkate. Ni aibu na hatari kwake.

  Watu wenye majina yao, japo walipotea njia kama akina Jaji Joseph Warioba walijaribu wakazomewa na kusutwa, sasa wamenywea itakuwa Hiza!

  Aliponiacha hoi Hiza ni pale alipowasingizia marehemu. Anadai Oscar Kambona alikuwa mwanazuoni! Pia anadai alipomtuhumu mwalimu JK Nyerere eti Mwalimu alinyamaza! Uongo, tena unaonuka.

  Kama Hiza kaishiwa hoja afunge mdomo. Kwani Nyerere alieleza bayana kuwa hana tatizo na madai ya Kambona bali anachoomba auleze umma na vyombo vyake zilipo na zikiwapo basi wazichukue.

  iza anachokifanya ni kujenga mazingira mazuri ya kuweza kujuana na Mkapa (kama atakuwa naye ameishiwa kiasi hicho) kwa kujifanya ni mtetezi wake. Tumewaona wengi hata waliofanya utapeli kwa kusingizia walitekwa na CCM kumbe ilikuwa ni kuwachuuza wenzao.

  Ila tunakokwenda mchezo huu ni hatari. Maana ni usaliti. Wanachofanya ni kujipaka mafuta halafu wanakwenda kupita kati kati ya moto.

  Kwa mtu anayeunga mkono mambo ya Mkapa na biashara zake za Ikulu iwe ni kwa njaa zake au upenzi wake au kwa vile alinufaika chini ya utawala wake, ni adui wa umma.

  Nafasi haitoshi. La muhimu ni wananchi kuanza kuongeza idadi ya maadui wao kama umma ambapo hili genge jipya linalotumiwa au kujipandikiza kutetea uoza na kuhujumu harakati zao inabidi liangaliwe kwa jicho baya.
   
 8. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #8
  Nov 29, 2007
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,222
  Likes Received: 2,085
  Trophy Points: 280
  Niliusoma uchambuzi huu kwa makini kabisa, nami nikajazi wa kwangu, nadhani kama Tambwe angekuwa na uelewa hata wa mtoto wa shule ya chekechekea basi asingethubutu kuendelea kuubeba msalaba ambao inaonekana unamwelemea.

  Nimeona waganga njaa wengi lakini huyu bwana ni mwisho wa yote.
   
 9. C

  Chuma JF-Expert Member

  #9
  Nov 29, 2007
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  sikuona uhusiano wa Title na article....
   
 10. Nzokanhyilu

  Nzokanhyilu JF-Expert Member

  #10
  Nov 30, 2007
  Joined: Feb 19, 2007
  Messages: 1,087
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  Kweli, unajua nimeanza kusoma thread nikajua Zitto ndio kaandika. Nikakuta mwandishi kaweka bold vijisehemu vya Zitto. Katika paragraph 31, ni para 4 zimewekwa bold. Paragraph 4 zimeipa title thread.....mmh.
  Naona Nkuzi Kwanzi na Mkandara wamefunika.
   
 11. B

  BroJay4 JF-Expert Member

  #11
  Nov 30, 2007
  Joined: Aug 27, 2007
  Messages: 236
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  nilifikiri huo ujumbe umeandikwa na Zitto,kumbe ni tapeli Hiza,halafu huyu Mtu wa Pwani,naona hana kazi ya kufanya,yaani kutwa na usiku amekalia majungu tu,aone wapi wamezungumza mambo ya chadema,ili alete kijiweni.Huyu jamaa wa wapi?Kaa ukijua kuwa kinachoendelea nchini,ni zaidi ya chadema na ccm,watu wamechoka na viongozi wababaishaji.
   
Loading...