Kumbe CCM inataka kuwatosa Wafanyabiashara!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kumbe CCM inataka kuwatosa Wafanyabiashara!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kimbunga, May 15, 2011.

 1. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #1
  May 15, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  WanaJF katika taarifa ya habari ya TBC1 nimemsikia Katibu Mkuu wa CCM ndugu Wilson Mukama akisema kwamba CCM itawaengua wafanyabiashara ambao walijiunga CCM kwa hila na kufanya mambo ambayo jamii haiyataki. Nikiangalia ndani ya CCM naona WAKULIMA na WAFANYAKAZI wamebaki kidogo sana; Kwa miaka ya karibuni CCM iliamua kuwakumbatia wafanyabiashara na wengi wakapewa majina ya wafadhili wa chama na ndio maana tukaona kufumuka kwa wafanyabiashara wakigombea vyeo vya kisiasa kama ubunge. Sasa CCM ikiamua kuwaengua wafanyabiashara itabaki na nini kwa kuwa Wakulima na wafanyakazi walishatoswa!!!

  Lingine: Eti malumbano ya Nnape na CHADEMA ni kachumbali ya kisiasa!! Sikumwelewa
   
 2. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #2
  May 15, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Ni kazi rahisi. Hawa wanajulikana na sidhani kama wanaozungumziwa ni wale wafanyabiashara ya mchele na unga soko la tandale. Hawa ni wale wanaokitumia chama kufanya ufisadi wao.
   
 3. Hassan J. Mosoka

  Hassan J. Mosoka JF-Expert Member

  #3
  May 15, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 647
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Mkuu,
  Ubavu huo ccm haina kwa sababu hawa ndo wanaoendesha chama katika nyanja zooote ikiwa na pamoja na kugawa position mbali mbali za kiserikali. so hao watazama wote pamoja
   
 4. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #4
  May 15, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  CCM haina ubavu wa kuwaondoa hao wafanyabiashara inaowasema ni porojo tuuuuu
   
 5. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #5
  May 15, 2011
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Kwa hiyo katoa tena siku 90 au CCM inakubali kukaa na magamba (mafisadi) kwa siku ngapi?
   
 6. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #6
  May 16, 2011
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  RA kweli ni mfanyabiashara, Mzee wa Maamvi naye wanaweza kumtosa kwa nembo ya biashara zake, Naye wa Vijisenti sijui anabiashara gani iliyomwingizia vijisenti vyake...hata hivyo Mukama anarudia yaleyale ambayo JK alishawahi kusema na yakamshinda kuwa ni muhimu viongozi kuachanisha mambo ya siasa na bishara halafu hakuna kilichofanyika hadi wa leo hii wafanyabiashara ndio wamezidi kuliko wakati alivyokuwa anaota njozi hizo.
   
Loading...