bigilankana
Senior Member
- Dec 15, 2009
- 144
- 4
CCM yaweweseka kwa Slaa
Na Waandishi wetu
6th January 2010
B-pepe
Chapa
Maoni
Dk. Wilbroad Slaa, Katibu Mkuu wa CHADEMA
Macho ya Watanzania yakiekelezwa kwenye uchaguzi mkuu wa rais na wabunge utakaofanyika Oktoba mwaka huu, Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Arusha bado kinaliota jimbo la Karatu ambalo limeshikiliwa na mwanasiasa machachari wa upinzani, Dk. Wilbroad Slaa, tangu mwaka 1995.
Dk. Slaa, Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), amekuwa vinywani mwa makada wa CCM mkoani hapa na jana Katibu wa CCM wa mkoa huo, Mary Chatanda, aliweka hadharani jinsi wanavyolitamani jimbo la Karatu.
Bila kuonyesha kama majimbo mengine ya mkoa wa Arusha yanawakosesha usingizi kwa kuwa yanashikiliwa na CCM, Chatanda alisema watalinyakua jimbo la Karatu katika uchaguzi mkuu ujao kwa madai kwamba Chadema haijaleta maendeleo.
Katibu huyo alitamba kwamba ni wakati sasa wa Dk. Slaa kujiandaa na kufungasha virago kwani jimbo hilo litachukuliwa na CCM kwa kuwa wananchi wa Karatu wana hamu ya kuongozwa na CCM.
Chatanda alidai wananchi wa Karatu wanaipenda CCM ndiyo maana mkoani Arusha wamepata viti vingi katika uchaguzi wa serikali za mitaa na vitongoji uliofanyika mwaka jana mwishoni.
Katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliopita, CCM ilionyesha wazi kuwa inakubalika kisiasa kwa kuwa ilipata viongozi wa vijiji na vitongoji wengi kuliko Chadema na hata katika kitongoji anachoishi Dk Slaa," alisema Katibu huyo.
Aidha, Chatanda alisema kuwa hali ya kisiasa kwa CCM katika Mkoa wa Arusha na wilaya zake ni nzuri na dalili zilionyesha katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa kuwapata viongozi wa vijiji, mitaa na vitongoji.
Wakati Chatanda akielezea kuweweseka na jimbo la Karatu, ametoboa siri kuwa njaa kali ya wapambe ndani ya chama hicho imezua balaa kiasi cha kuwagonganisha viongozi wanaotaka kuwania nafasi za kuchaguliwa.
Wakati katibu huyo akionyesha matamanio yake kwa jimbo la Karatu, Dk. Slaa amesema hatima ya jimbo hilo itaamuliwa na wananchi wake.
Dk. Slaa alitoa kauli hiyo jana alipozungumza na Nipashe kuhusiana na mikakati ya CCM kutaka kumung'oa.
Katika mahojiano hayo, Nipashe ilitaka kujua Dk. Slaa, ambaye pia ni Naibu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni kama yuko tayari kungoka na kuacha jimbo hilo liwakilishwe na mbunge kutoka CCM.
Waulizeni wananchi wa Karatu, kwa sababu wao ndio walioniweka, alisema Dk. Slaa kwa ufupi.
Awali, katika mahojiano hayo, Dk. Slaa aliwashangaa wanaCCM na watu wengine, wanaodhani kwamba CCM italikomboa jimbo la Karatu, katika uchaguzi ujao kwa kutumia kigezo cha matokeo ya uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji, uliofanyika wilayani humo mwaka jana.
Hizo ni ndoto za mchana. Chadema hatuhangaiki na ndoto za mchana. Kinachozungumzwa ni takwimu na si propaganda, alisema Dk. Slaa.
Alisema watu wenye mawazo kwamba, Chadema itangolewa Karatu katika uchaguzi mkuu wa Oktoba wanatakiwa wafanye tathmini ya kina ya matokeo ya uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji jimboni humo, badala ya kutumia propaganda.
Dk. Slaa alisema katika uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji wa mwaka jana, Chadema ilishinda katika vijiji 19 dhidi ya 16 ilivyopata katika uchaguzi wa mwaka 2004 jimboni humo.
Sasa hicho ndicho kigezo cha wao (CCM) kushinda mwaka huu?, alihoji.
Katika uchaguzi wa serikali ya vijiji wa mwaka 2004, CCM ilishinda vijiji 29 kati ya 45 vilivyokuwapo.
Alisema mbali ya kuongeza idadi ya viti katika vijiji hivyo, katika uchaguzi wa mwaka jana, Chadema walikuwa wanyakue viti zaidi dhidi ya CCM katika eneo la Karatu mjini, lakini wakalazimika kuvipoteza kutokana na mabadiliko ya muundo wa jimbo.
Dk. Slaa alisema mabadiliko ya muundo huo, yalisababisha mitaa yote sita, ambayo Chadema ilishinda katika eneo la Karatu mjini katika uchaguzi wa mwaka jana kuondoshwa.
Kama katika uchaguzi wa serikali ya vijiji mwaka jana, CCM walishinda viti 24 na Chadema 19, vile viti sita kama visingeondolewa katika hayo mabadiliko ya muundo, nani angekuwa ameshinda?, alihoji Dk. Slaa.
Kwa jumla Karatu ni jamhuri ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, sababu Chadema inatekeleza Ilani yake, tumeunda halmashauri na tuna Meya, aliongeza.
Chama tawala kimekuwa kikiibuka na mikakati ya kukomboa majimbo yanayoshikiliwa na upinzani kila uchaguzi unapokaribia.
Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005, CCM kilipania kuyakomboa majimbo ya Kigoma Mjini lililokuwa linashikiliwa na Chadema, Karatu, Bukoba Mjini lililokuwa linashikiliwa na CUF na Moshi Mjini, linaloshikiliwa na Chadema.
Hata hivyo, Dk. Slaa na Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo, walitetea majimbo yao wakati waliokuwa wabunge wa Kigoma Mjini na Bukoba Mjini, Dk. Aman Walid Kabourou na Wilfred Lwakatare walishindwa kutetea majimbo yao.
Hivi sasa majimbo yanayoshikiliwa na upinzani kwa upande wa Tanzania bara ni Karatu, Moshi Mjini, Kigoma Kaskazini, Tarime na Mpanda Kati.
Imeandikwa na Charles Ole Ngereza, Arusha na Muhib Said, Dar.

- Takwimu za huu uchaguzi zitoke sasa maana mimi nilijua CHADEMA ilishinda kwa mbali Karatu kufuatia habari zilizoletwa humu. Kumbe CCM ndio iliongoza Karatu?
- Karatu sio Jamhuri ndani ya Jamhuri. Nadhani hapa Daktari katereza. Najua hana nia mbaya ila kauli kama hii haipaswi kutoka kwa kiongozi aliyekaa Bungeni zaidi ya muongo mmoja na nusu.
- Kama mwaka 2004 CCM walipata viti 29 kati ya 45 na kupoteza Ubunge, Mwaka 2009 wamepata 24 kati ya 45 na watapoteza tena Ubunge wa Karatu.
- CHADEMA wasiogope kusema matokeo yale kwani hayana mahusiano na Uchaguzi Mkuu.