Kumbe BongoFleva inalipa!! Diamond Platnumz anaingiza Milioni 200 kwa mwezi kwa matangazo tu

Mayu

JF-Expert Member
May 11, 2010
6,612
10,664
Msanii wa Bongofleva, Naseeb Abdul maarufu Diamond Platnumz amesema kila mwezi huingiza Sh200 milioni kutokana na kuingia mikataba na kampuni mbalimbali kuwa balozi wa bidhaa zao.

Akizungumza katika kipindi cha TheSwitch kinachorushwa na redio ya Wasafi leo Alhamisi Januari 28, 2021, Diamond amesema fedha hizo ni mbali na zile anazoingiza kupitia muziki.

Amebainisha kuwa anaingia mikataba na kampuni na amekuwa akifanya hivyo kwa kila kampuni inayohitaji huduma yake.

“Endosment zangu mimi mshahara wangu kwa mwezi si chini ya milioni 200, na tunasaini mikataba kila siku. Ninaingiza kwa wiki Sh55 milioni kwa siku Sh7 milioni kwa saa moja Sh300,000 na kwa sekunde Sh6,000.”

Amesema mwaka 2021 fedha anazozipata katika eneo hilo huenda zikaongezeka kwa kuwa anatarajia kuwa balozi wa vitu vingi zaidi kwa kuwa ameamua kufanya muziki kuwa kazi na biashara.

1611917259105.png

=====

Ina maana hii ni kwa endorsement za matangazo tu
 
Makampuni yanayompa mikataba ya matangazo ndio yanatotakiwa ku-withhold hiyo kodi, ndio maana ana Jeuri ya kuzungumza hadharani kwasababu jukumu la kupeleka kodi TRA ni la makampuni yanayompa mikataba
Bado pia mshikaj ni moja ya walipaji wazuri Tu wa kodi
 
Makampuni yanayompa mikataba ya matangazo ndio yanatotakiwa ku-withhold hiyo kodi, ndio maana ana Jeuri ya kuzungumza hadharani kwasababu jukumu la kupeleka kodi TRA ni la makampuni yanayompa mikataba
Itakuhitaji darasa kidogo kuhusu withholding tax mkuu
Imagine angekua analipwa yote, si angetakiwa kulipa Kodi ile ile mkuu
Mbona hesabu ndogo tu, na unajiita IFRS
 
Back
Top Bottom