Kumbe bidhaa kutoka Tanzania bara zikiingizwa Zanzibar inahesabika zimetoka nje ya nchi! Huu muungano haufai

Muuza Kangala

JF-Expert Member
Jul 21, 2021
1,124
4,162
Ndizi tokan Tanganyka zazuiwa huko Zanzibar
👇

Waziri aeleza sababu mwanamke aliyezuiwa kuingiza ndizi Zanzibar​

Zanzibar. Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Mifugo na Biashara wa Zanzibar, Shamata Shaame Khamis ametoa ufafanuzi kuhusu tukio la kutaifisha tenga 30 za ndizi za Veronica Mwanjala aliyekuwa akizisafirisha kutoka Tanzania Bara kwenda Zanzibar kwa ajili ya biashara.

Katika mitandao ya kijamii imeonekana taarifa inayoeleza tukio hilo ikimtaja mwanamke huyo ambaye anadaiwa mjane na kueleza jinsi waziri huyo alivyoagiza maofisa kutoka wizara yake wataifishe ndizi hizo na kumtoza faini ya Sh50,000 kwa madai Zanzibar haihitaji ndizi kutoka Tanzania Bara kwasababu inajitosheleza soko lake.

Tukio hilo linadaiwa kutokea jana Jumatano Februari Mosi, 2023 kisiwani humo.
Hata hivyo, akizungumza na Mwananchi Digital leo Alhamisi Februari 2, 2023, Waziri Shaame licha ya kukiri tukio hilo kutokea, amesema siyo kweli mzigo huo umekamatwa kwasababu Zanzibar inajitosheleza, isipokuwa ni kutokana na taratibu ambazo imejiwekea Zanzibar zinazokataza kuingiza ndizi kutoka nje kutokana na magonjwa yaliyoikumba migomba ya Tanzania Bara.

“Ni kweli tukio lipo lakini siyo kwa mazingira ambavyo linatangazwa kuwa Zanzibar inajitosheleza kwa ndizi ama kisa ni kutoka Tanzania Bara, uhitaji upo ila kwa mujibu wa sheria zilizopo haturuhusu kuingiza ndizi kwasababu ya kuzuia ugonjwa ulioshambulia migomba,” amesema.

Pia amesema mwanamke huyo aliingiza mzigo huo kimagendo maana hakuwa na kibali chochote huku akichanganya ndizo hizo na nyanya ili mzigo uonekane ni nyanya pekee.

“Hata hizo sanduku (matenga) sio 30 bali yalikuwa 15, na ndizi zilikuwa zimefichwa kwenye tungule (nyanya) ili kuonyesha kwamba mzigo huo ni wa nyanya kwahiyo inaonekana kabisa alikuwa akifanya jambo hilo akijua kuwa ni haramu,” amesema

Kuhusu faini, waziri amekiri mwanamke huyo kutozwa faini hiyo ya Sh50,000 lakini kuhusu kutaifisha mzigo akasema walitoa pendekezo kwa mwanamke huyo ama kuzirejesha alipozitoa au kuziharibu mbele yake akishuhudia jambo ambalo amedai hakuonyesha ushirikiano.

“Hivyo bado mzigo huo tunao, hakuonyesha ushirikiano, lakini kama akitaka kuuchukua tunamruhusu auchukue na asipouchukua tutaangalia ni njia ipi ya kufanya lengo kubwa ni kuzuia maganda yake ili yasilete magonjwa ya ndizi.
 
Hu muungano anae weza kuufafanua alikua Nyerere tu, na bahati alisha fariki, ni muungano special dunia nzima
Wanatuchanganya tu! Wangefanya zanzibar kua free port kama dubai pengine tungekua na nafuu kuliko haya malawama ya muungano! Na nchi nyingi zingetutegemea sana kibiashara
 
Ukiachia zaziba itakua kama Qatar au Dubai au Singapore hapo itatawaliwa tena, itakia nakipato kuipita Tanganyika, jambo ambao wengi wasingelipanda litokee
 
Kwa hiyo muungano ndio kinga ya zanzibar kutawaliwa tena!!!? Kwani wakiamua bagamoyo kua freeport nayo itaweza kutawaliwa huko mbeleni!!!? Sidhani kama hoja hiyo ina mashiko labda tu zanzibar ni nchi kamili na si mkoa mojawapo wa tanzania
 
Kwani bagamoyo ni kisiwa au nchi kama zazibar?
 
Ndizi tokan Tanganyka zazuiwa huko Zanzibar

Waziri aeleza sababu mwanamke aliyezuiwa kuingiza ndizi Zanzibar​

Zanzibar. Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Mifugo na Biashara wa Zanzibar, Shamata Shaame Khamis ametoa ufafanuzi kuhusu tukio la kutaifisha tenga 30 za ndizi za Veronica Mwanjala aliyekuwa akizisafirisha kutoka Tanzania Bara kwenda Zanzibar kwa ajili ya biashara.

Katika mitandao ya kijamii imeonekana taarifa inayoeleza tukio hilo ikimtaja mwanamke huyo ambaye anadaiwa mjane na kueleza jinsi waziri huyo alivyoagiza maofisa kutoka wizara yake wataifishe ndizi hizo na kumtoza faini ya Sh50,000 kwa madai Zanzibar haihitaji ndizi kutoka Tanzania Bara kwasababu inajitosheleza soko lake.

Tukio hilo linadaiwa kutokea jana Jumatano Februari Mosi, 2023 kisiwani humo.
Hata hivyo, akizungumza na Mwananchi Digital leo Alhamisi Februari 2, 2023, Waziri Shaame licha ya kukiri tukio hilo kutokea, amesema siyo kweli mzigo huo umekamatwa kwasababu Zanzibar inajitosheleza, isipokuwa ni kutokana na taratibu ambazo imejiwekea Zanzibar zinazokataza kuingiza ndizi kutoka nje kutokana na magonjwa yaliyoikumba migomba ya Tanzania Bara.

“Ni kweli tukio lipo lakini siyo kwa mazingira ambavyo linatangazwa kuwa Zanzibar inajitosheleza kwa ndizi ama kisa ni kutoka Tanzania Bara, uhitaji upo ila kwa mujibu wa sheria zilizopo haturuhusu kuingiza ndizi kwasababu ya kuzuia ugonjwa ulioshambulia migomba,” amesema.

Pia amesema mwanamke huyo aliingiza mzigo huo kimagendo maana hakuwa na kibali chochote huku akichanganya ndizo hizo na nyanya ili mzigo uonekane ni nyanya pekee.

“Hata hizo sanduku (matenga) sio 30 bali yalikuwa 15, na ndizi zilikuwa zimefichwa kwenye tungule (nyanya) ili kuonyesha kwamba mzigo huo ni wa nyanya kwahiyo inaonekana kabisa alikuwa akifanya jambo hilo akijua kuwa ni haramu,” amesema

Kuhusu faini, waziri amekiri mwanamke huyo kutozwa faini hiyo ya Sh50,000 lakini kuhusu kutaifisha mzigo akasema walitoa pendekezo kwa mwanamke huyo ama kuzirejesha alipozitoa au kuziharibu mbele yake akishuhudia jambo ambalo amedai hakuonyesha ushirikiano.

“Hivyo bado mzigo huo tunao, hakuonyesha ushirikiano, lakini kama akitaka kuuchukua tunamruhusu auchukue na asipouchukua tutaangalia ni njia ipi ya kufanya lengo kubwa ni kuzuia maganda yake ili yasilete magonjwa ya ndizi.
Waziri waziri Hili jambo sio dogo
 
Watanganyika ni zero brain.
JamiiForums2073952431.jpg
 
Wanatuchanganya tu! Wangefanya zanzibar kua free port kama dubai pengine tungekua na nafuu kuliko haya malawama ya muungano! Na nchi nyingi zingetutegemea sana kibiashara
Fafanua?
Unadhani kwa nini Comoro wameshindwa?
 
Back
Top Bottom