Kumbe Bi Siti Mwinyi Ndo Mmiliki Wa Mv SPICE ISLANDER,

Uhusiano wa kukufanya uwe na hasira kwa kuambiwa mmiliki wa meli na magamba upo wapi? zaidi ya roho mbaya uliyonayo? tuwe wakweli nchi hata siku moja haitajengwa kwa mawazo ya ajabu kiasi hiki
Nchi ishameguka unakumbuka kujengwa,We utakuwa magamba tu tena original,

Magamba mmesha ibomoa nchi kwa siasa uchwara na za kulindana.
Magamba nchi hii mmeiweka Rehani kwenye mikono ya wezi.

Magamba mmeifanya nchi hii kupumulia matamvua mithili ya samaki.

Ukwapi huo ujengwaji unaoutaka wewe,kama kila siku nchi inanyonywa na wanyonyaji wazalendo.
 
Kwa huyu mama tuhuma hizi ni za mtoto.Mimi nyingine niliposikia matumbo yaliuma.Itoshe kusema kwamba sikuamini binadamu anaweza kufanya mambo kama hayo.
Baada ya Kuripotiwa Mmiliki wa Meli ni yule mbunge mh Jaku.kumbe yule ni Msimamizi tu,lakini wamiliki halali ni mke alieachika wa awamu ya pili aliekutwa na madawa ya kulevya Bi Siti Mwinyi.Na mwanae Dr Hussein mwinyi ambae ni Waziri wa ulinzi.

Baada ya kusikia hZ TAARIFA nilianza kuziuliza kwa wapemba ninao wafahamu ambao ni wanajeshi jwtz Wote walikiri kuwa Wamiliki wa Meli hao niliowataja hapo juu na wakaenda mbali zaidi kuwa serikali haitamtaja kamwe,zaidi ya kuweka propaganda tu hapo
"Wazanzibar wengi tunajua hilo lakini hatuwezi kusema"

Kama hz hbr ni za kweli sitakuwa na budi kuendelea kuchukia HAYA MAGAMBA.
 
hivi hiyo meli ilikuwa na insurance? Je, waliofiwa wanalipwa fidia kiasi gani? Ama ndio pata potea?
 
hivi hiyo meli ilikuwa na insurance? Je, waliofiwa wanalipwa fidia kiasi gani? Ama ndio pata potea?
Insurance Ilikuwepo nadhani watakuwa Alliance kama sikosei lakini kuna Conditions zake za kulipa.

Sheria za Marine lazima zifuatwe watalipa kiasi kinachostahili tu
Zengine watalipa Wamiliki tatizo kama kuna harufu ya kimagamba hapo ujue kutakuwa na utata Arabuni Mmiliki hunyongwa
 
mungu anaonyesha.mali zimewajaa kupita kipimo.hata ghorofa jipya pale kijitonyama huenda likabomoka.
 
Jamani mmiliki wa meli ana kesi ya kujibu?? kama kibali cha biashara anacho tatizo lipo kwa mamlaka zinazosimamia usafiri wa majini..

Hapa auliziwe ni nani mwenyekiti wa mamlaka ya usafiri wa majini Zanzibar?? na woote walio chini yake..Awe Sitti mwinyi au Husein au hata mimi mwenyewe..Je nikakae kuangalia meli imepakia abiria wangapi na wakati kuna watu wenye wajibu bandarini? Sasa kwenye Ndege ingekuwa ni lengo kujaza si wangepakia kama magari ya Mbagala??? Hapa pana hoja ya maana ambayo ni walioundwa kuwa tume na wenye mamlaka ya usafirishaji Zanzibar Si mtoto wa mjomba kwa shangazi????? Nimeyazoea hapa unguja..kila mtu ndugu kwa mwenzie...

Kwa hali ya kawaida, ningekubaliana na wewe kwa asilimia 100. Ila kwa kuangalia hali ya Tanzania na mifano mingi niijuayo, naona umepotoka kidogo.

Chenge alipoigonga ila bajaji na kuuwa watu wawili Oysterbay, jaribio la kwanza lilikuwa kumsukumia kesi dereva wa bajaji na mmliki wake. Ilipokwama, bado wakamshitaki mmiliki kwa kutotoa taarifa za wapi alipo dereva wake.

Ajali ya treni Dodoma/Singida miaka ya 90 walipomkosa mmoja wa watuhumiwa, walishikwa mke wake na mdogo wake kusaidia uchunguzi.

Miaka pia ya late 80s baada ya msafara wa Salim A. Salim (akiwa Waziri wa Ulinzi au Waziri Mkuu) kukoswakoswa na daladala UWT road, alishikwa dereva, konda, utingo na mmiliki wake. Mmiliki alifuatwa Morogoro.

Kuna kesi nyingi sana kama hizo ambazo wamiliki wamerundikwa ndani kwa kosa la kuwa 'wamiliki' wa vyombo vya usafiri ambavyo vimepewa vibali na mamlaka zinazosimamia usafiri huo.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom