Kumbe benki ya NMB kwa Pinda iliteketezwa kwa radi ya kutengeneza!!!!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kumbe benki ya NMB kwa Pinda iliteketezwa kwa radi ya kutengeneza!!!!!!!

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by steering, Oct 5, 2012.

 1. s

  steering Member

  #1
  Oct 5, 2012
  Joined: Nov 28, 2011
  Messages: 71
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  “Ile benki iliunguzwa na radi na mzee mmoja mkulima wa kijiji cha Kizi baada ya aliibiwa hela nyingi katika akaunti yake, akaona alipe kisasi kwa njia ile. Ile benki iliungua wa radi, hakuna asiyejua,”

  story kamili
  Mwananchi
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"]Radi huuuzwa Sumbawanga kwa shilingi elfu 40 tu[/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Friday, 05 October 2012 08:52[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]
  digg
  [​IMG]Na Florence Majani
  KWA wakazi wa Dar es Salaam, mawingu yanapotanda angani na kutengeneza giza ambalo huashiria mvua, kwao huwa ni jambo la kawaida na pengine ni ahueni kwa karaha za joto kali.

  Lakini kwa wakazi wa mkoa wa Rukwa, ikiwemo hasa Sumbawanga, dalili ya mvua inayoambatana na radi ni tishio la umauti, kwani mara nyingi radi hizi si za kawaida au za asili bali ni za kichawi na hutengenezwa na wanadamu kwa madhumuni ya kuua.
  Mkoa wa Rukwa hususani wilaya ya Sumbawanga, ni eneo linalosifika kwa imani za kishirikina nchini. Lakini katika masuala ya utaalamu wa radi, yapo maeneo na watu maalum ambao wana uwezo wa kutengeneza radi.
  Ukiwa unatokea wilaya ya Sumbawanga kuelekea wilaya ya Nkasi, ndipo vilipo vijiji maarufu kwa kutengeneza radi hizo.
  Baadhi ya vijiji hivyo ni Sintale na Chipu, ambako ndiko walipo wataalamu wenye uwezo na nguvu za ziada za kutengeneza radi.
  Kwa nini radi zinatengenezwa?
  Radi hizi zinatengenezwa kwa ajili ya kuua au kuwajeruhi maadui. Kwa mfano, kama yupo aliyekudhulumu, aliyekuibia mke au mume, aliyekugonga na gari bila kukulipia gharama za matibabu au anayekutusi na kukukebehi.

  Vijiji vya Sintale, Chipu na Kalundi, vimepakana, kinaanza kijiji cha Kalundi kisha Sintale na cha mwisho ni Chipu. Vijiji hivyo viko duni kimaendeleo na ukubwa. Hata hivyo huku ndipo walipo watalaamu na mafundi wa kuunda radi.
  Nilipokuwa mkoani humo hivi karibuni na mwenyeji wangu, tulielekezwa na wenyeji wa Kalundi kwa mganga wa kwanza nayeitwa Mashaka ambaye anaaminiwa kwa kuunda radi.
  Baada ya kufika kwa Mashaka, tunamkuta akiwa na wateja kadhaa. Ninamweleza shida yangu na kumtonya kuwa ni shida ya kipekee kidogo.
  Namweleza kuwa nahitaji kununua radi kwani nina adui yangu aliyenidhulumu fedha nyingi. Mashaka anajibu kuwa yeye si mtaalamu wa radi bali anatibu maradhi tu.
  Anasema: “Lakini yupo mtaalamu wa radi, anaitwa mzee Chimwaga, anaishi kijiji cha Sintale. Ngoja nimpigie simu sasa hivi,”
  Mganga huyu anazungumza kwenye simu kwa lugha ya kifipa, na baada ya dakika chache anakata simu na kutugeukia na kusema: “Yupo- nendeni- kutoka hapa kwenda Sintale kwa Honda ni dakika 20, mkimuuliza yeyote, atawapeleka kwa mzee huyo,”
  Kwa kuhofia muda, hatukwenda kwa mganga Mzee Chimwaga, na badala yake tunakwenda eneo jingine na kuuliza iwapo kuna mganga mwingine mwenye utaalamu wa radi.
  Mzee mmoja anatuelekeza kuwa yupo mganga anayeitwa Ntoro, mwenyeji wa hapo hapo Kalundi ambaye naye ni mtaalamu wa radi.
  Tunaelekezwa kwa mganga Ntoro, tunapofika tunamkuta akiwa na wake zake wawili na watoto wasiopungua wanane. Anatukaribisha na tunamweleza shida yetu.
  Mganga Ntoro anasema, yeye hutengeneza radi lakini kwa wakati ule alikuwa kaishiwa vifaa, hivyo aliamua kumpigia simu mganga mwenzake mwenyeji wa kijiji cha Sintale ambaye ana ujuzi huo pia.
  Anashika simu, na kumpigia mganga huyo tuliyebaini kuwa anaitwa Maisha, huku akimsisitizia afike haraka azungumze na wateja.
  Wakati tukimsubiri Mganga Maisha afike, tulianza kumdodosa Mganga Ntoro kuhusu utaalamu huo wa kuunda radi.
  Ntoro anasema, kwa kawaida huduma ya radi huuzwa, au hutozwa gharama kwa bei ya kuanzia Sh40,000 hadi 30,000 tu na hiyo ni kulingana na umbali wa eneo alipo mtu anayetakiwa kuuwawa na aina ya radi.

  “Kwa mfano watu wanaotoka Zambia au Kongo tunawachaji fedha nyingi zaidi kwa sababu ya umbali, lakini kwa maeneo ya karibu bei ni nafuu kidogo,” anasema Ntoro.
  Radi hutengenezwaje?
  Ntoro anasema, kwa kabila la kifipa, utaalam wa kuunda radi huitwa ‘Namasata’.
  Radi hutengenezwa kichawi, lakini mtu yeyote anaweza kufundishwa na kuweza kuitengeneza, ili mradi afuate masharti.

  Anasema zipo radi za aina tatu, ya kwanza ni ya maji, ya pili ni ya pembe, na ya tatu ni ya gome la mti. Zote hizo hutengenezwa kulingana na umbali na ubora wake.
  “Radi ya pembe ni ya hatari zaidi, huchoma na kuweza kutekeza watu na mali, na huenda umbali mrefu tofauti na radi ya gome la miti,” anasema
  Huku tukiendelea kumdadisi, mganga Ntoro anasema, radi ya maji hutengenezwa kwa kuchukua sahani mpya, bakuli mpya au chupa ya udongo. Kisha mtaalamu huweka dawa ndani ya chupa au bakuli na kuisemea maneno fulani.
  “Ukishanuiza, unaviweka vifaa hivyo ndani, kesho asubuhi utakuta maji ndani ya chupa au kama uliweka bakuli basi utaona maji ndani ya bakuli,” anasema na kuongeza,
  “Baada ya hapo unachukua vifaa vile na kuanza kunuiza adhabu unayotaka impate mbaya wako, kwa kumtaja jina. Kama huna jina basi uwe na nyayo zake, nguo au kitu chake chochote kile.”
  Anasema baada ya kunuiza, unachukua bakuli au chupa ikiwa juu ya sahani na kuyarusha maji yale juu, kwa nguvu za kichawi, maji yale hupotea lakini kama kutakuwa na kasoro yeyote, maji yale humrudia aliyeyarusha.
  Endapo mtaalamu atairusha radi ile kwa mtu asiye na makosa, basi maji yatarudi chini na kama kweli mtu yule amefanya kosa, basi maji hayatarudi na yatakwenda angani na kuanza kutengeneza wingu jeusi linaloambatana na ngurumo.
  “Maji yakisharushwa juu, baada ya saa moja tu, utaanza kuona angani kiwingu cheusi na kizito sana, mvua inaweza kunyesha kidogo na kisha ngurumo za kutisha … basi hapo ujue kazi tayari na mbaya wako kashamalizwa,” anasema na kuongeza:

  “Kama unairusha radi kwa mtu asiye na makosa kabisa, au ukakosea masharti radi inaweza kukurudia na kukuunguza wewe. Mtu akiniudhi mimi huwa nazirusha tu,”

  Radi ya pembe hutengenezwaje?
  Wakati tukiendelea kumsubiri mganga Maisha, kutoka Chipu, Mganga Ntoro anaendelea kutupa utaalamu huo bila kujua kuwa alikuwa akichunguzwa.

  Sasa anasimulia namna ya kutengeneza radi ya pembe. Anasema, radi hii hutengenezwa kwa pembe ya mbuzi au kondoo, ambayo kwa kawaida huwa na uwazi katikati.
  ‘Tunachukua pembe, tunaweka dawa ndani yake, (yaani kwenye uwazi) tunafunga hirizi kuizunguka pembe, pamoja na shanga, kisha tunanuiza maneno kadhaa ya kichawi, na kisha tunairusha kuelekea alipo mlengwa,” anasema
  Radi hii ni kama kimondo, inaporushwa, hupaa angani na hufuka moshi katika upande wa mbele wa pembe wenye uwazi kama zifanyavyo ndege za kushambulia(rocket).

  Mganga Ntoro anasema, radi hii huweza kupaa umbali mrefu na huweza kuharibu mali, mifugo na binadamu ambaye anawindwa.
  Kuhusu namna ya kutengenez radi ya gome la mti, Ntoro anasema hiyo ina masharti makali ambayo si rahisi kuzitoa siri zake kwa kila mtu.
  Hata hivyo, baada ya muda mfupi, mganga Maisha anapiga simu na kusema kuwa ameshindwa kufika kwa sababu ametingwa na shughuli za mazishi na kutaka twende siku inayofuata asubuhi na mapema.
  Mkazi mwingine wa kijiji hicho, David Ntare anasema mauaji ya radi ni jambo la muda mrefu mahali hapo kwani wanaotumia uchawi wa radi wamekuwa wakijigamba mitaani kwa uweza wao huo.
  “Tangu nazaliwa nasikia vifo vya radi na nina uhakika si radi za kawaida kwa sababu, wanaokufa mara nyingi huwa na uhasama na mtu, kama kumuibia mke,mume, kuiba au kutukana,” anasema Ntare.
  Ntare analihusisha tukio la kuungua kwa benki ya NMB, wilayani Nkasi, tarafa ya Namanyere lililotokea miaka ya nyuma na uchawi wa radi.
  “Ile benki iliunguzwa na radi na mzee mmoja mkulima wa kijiji cha Kizi baada ya aliibiwa hela nyingi katika akaunti yake, akaona alipe kisasi kwa njia ile. Ile benki iliungua wa radi, hakuna asiyejua,” anasema
  Inadaiwa kuwa wenyeji wa hapa aghalabu huviona vitu hivi na hujua madhumuni yake na mara nyingi vifo vya aina hii hutokea wilayani Sumbawanga.
  Anasema, kwa kawaida mtu aliyeungua kwa radi huwa kama aliyeungua kwa umeme.
  “Huungua na kuwa weusi kama mkaa, na wakati mwingine radi hukataa kumuua mtu akiwa ndani, bali humrusha nje na kumchoma huko ili isiwadhuru watu wengine,” anasema.

  Mwalimu wa shule ya msingi Chalantala, Abeid Kisanga, anasema siku moja akiwafundisha wanafunzi wa darasa la tatu somo la sayansi kuhusu radi , mwanafunzi wa kiume alinyoosha kidole na kusema ‘mimi najua kutengeneza radi, baba kanifundisha,”
  Anjelo Singo, Afisa wa Polisi tarafa ya Namanyere anasema suala la ushirikina wilaya ya Sumbawanga na Nkasi ni kubwa na yamekuwapo matukio kadhaa ya vifo vinavyodaiwa kusababishwa na imani hizo.
  “Ingawa serikali haiamini uchawi, lakini matukio ya radi yanayotokea hapa mengi ni ya kishirikina, au matukio ya watu kuuwawa na kukatwa sehemu za siri vilevile ni ya kishirikina,” anasema
  Anasema ni ukweli usiopingika kuwa uchawi umesheheni katika maeneo haya na wakazi wake wameshaathirika kisaiolojia kuhusu hilo.
  Mkuu wa mkoa wa Rukwa, Mhandisi Stella Manyanya anasema ameshawahi kusikia taarifa za kuwepo kwa wataalamu wa kuunda radi lakini akasema hata hivyo hana uhakika nazo.
  “Unajua jiografia ya mkoa wa Rukwa imekaa katika nyanda za juu, ni rahisi radi kulipuka maeneo haya. Hata hivyo hili suala ni la kiimani zaidi,” anasema
  Anasema pamoja na mambo mengi yanayosemwa kuhusu mkoa huo, kwa sasa maendeleo yanakwenda kwa kasi na anaamini miaka michache ijayo, imani za ushirikina zitapungua kama sio kwisha kabisa.


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Kennedy

  Kennedy JF-Expert Member

  #2
  Oct 5, 2012
  Joined: Dec 28, 2011
  Messages: 11,270
  Likes Received: 2,947
  Trophy Points: 280
  Mmmh makubwa haya,bora akapige BOT.
   
 3. Kimbori

  Kimbori JF-Expert Member

  #3
  Oct 6, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 2,725
  Likes Received: 347
  Trophy Points: 180
  Hii teknolojia ni hatari, ndio maana kila kona ya jiji kuna matangazo "Mganga wa Jadi kutoka Sumbawanga".
   
 4. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #4
  Oct 6, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  mkuu Kimbori kwa sababu ya Uchawi wa Radi tu kila mtu anajitia yeye (Mganga

  toka Sumbawanga?)
  Matapeli hao Waganga Kama kweli hao Wachawi wana uwezo wanifanyie miye Uchawi ili

  niwe Tajiri Kuliko Bill Gates niwe Trillionea wa pesa nikiamka tu nizikute pesa chini ya mto hazina idadi ya

  kuhesabu uchawi wenyewe wa kudhuru watu huko Sumbawanga? mimi nilifikiri wana uchawi wakupata Utajiri wa

  pesa?ahh mahali popte pale penye uchawi hapana Maendeleo yoyote yale.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. Baba V

  Baba V JF-Expert Member

  #5
  Oct 6, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 19,507
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  Ila hilo ni kweli kabisa, nikiwa nasoma high school Kantalamba sumbawanga kun mwenzetu alikuwa anamchukua bi mdogo wa mganga wa kienyeji, alivyostukiwa ikabidi akajisalimishe kwa Sangoma mmoja amtengenezee kinga, kesho yake usiku wa saa nane zilipiga radi mbili nyuma ya bweni letu na kuvunja miti mikubwa miwili, jioni jamaa kaja kutusimulia kuwa Sangoma wake kamweleza kila tukio as if naye alikuwamo bwenini. kamwambia zindiko ndo limemuokoa otherwise ndo walikuja kumchukua
   
 6. Mama Mdogo

  Mama Mdogo JF-Expert Member

  #6
  Oct 6, 2012
  Joined: Nov 21, 2007
  Messages: 2,865
  Likes Received: 430
  Trophy Points: 180

  Kuwazia kuipiga BOT kwa radi nafikiri ni kosa la uhujumu uchumi!!! Au una maana radi ipige BOT halafu ibague na kuunguza mafisadi tu, wa EPA, etc??? Hapo poa tu!!!
   
 7. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #7
  Oct 6, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 0
  Bora radi itengenezwe ipige lkulu
   
 8. Globu

  Globu JF-Expert Member

  #8
  Oct 7, 2012
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 7,975
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Duh!!! hii ya Radi ya Man made imeniacha hoi. Kweli dunia ina mambo.
   
 9. Globu

  Globu JF-Expert Member

  #9
  Oct 7, 2012
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 7,975
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Duh!!! hii ya Radi ya Man made imeniacha hoi. Kweli dunia ina mambo.
   
 10. alphoncetz

  alphoncetz JF-Expert Member

  #10
  Oct 7, 2012
  Joined: May 1, 2011
  Messages: 282
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Serikali iwachukue ifanye nao mkataba watengeneze radi nyingi zikae standby kwa ajili ya kulipua kila anayeiba pesa ya serikali, yaani wawe replacement ya polisi na takukuru!
   
 11. Kambaku

  Kambaku JF-Expert Member

  #11
  Oct 7, 2012
  Joined: Nov 12, 2011
  Messages: 1,987
  Likes Received: 2,889
  Trophy Points: 280
  Aisee mngetuwekea na bei jamani, kuna mtu anajifanya mjanja nataka nimuoneshe kazi!
   
 12. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #12
  Oct 8, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  Mkuu TIQO Hiyo Radi ipige Ikulu impige nani tena?

  Mkuu Kambaku unataka kuuwa mtu? Ni dhambi kuu hiyo.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...