Kumbe Balali hakuwa mwajiriwa wa serikali?

NakuliliaTanzania

JF-Expert Member
Sep 24, 2007
555
7
Naona mambo mabichi kabisa.....kumbe hakufukuzwa kazi in the real sense...ndo maana wakasema wametengua...nadhani Balali bado anazo nguvu nyingi na mambo mengi anayojua

Je ina maana alikuwa anafanya kazi kama consultant? au raia wa kigeni?



Meghji: Ballali hakuwa mtumishi wa serikali




na Mwandishi Wetu, Dodoma



ALIYEKUWA Gavana wa Benki Kuu Tanzania (BoT), Dk. Daudi Ballali, ambaye uteuzi wake ulitenguliwa hivi karibuni na Rais Jakaya Kikwete, hakuwa mtumishi wa serikali, Tanzania Daima imebaini.
Uhakika kwamba Dk. Ballali hakuwa mwajiriwa wa serikali, ulitolewa hivi karibuni na Waziri wa Fedha, Zakia Meghji, wakati alipokuwa akizungumza na redio moja inayorusha matangazo yake kupitia intanet.

Meghji alisema kuwa, Dk. Ballali alikuwa na mkataba wa kuwa Gavana tu na hakuwa na mkataba wa ajira serikalini, na kumaliza utata uliokuwa umetanda kuhusu iwapo kiongozi huyo alikuwa mwajiriwa wa serikali.

Meghji alisema kuwa, kwa maana hiyo, mkataba baina ya serikali na Dk. Ballali uliisha siku ambapo uteuzi wake wa kuwa Gavana ulipotenguliwa.

Ballali aliteuliwa kama Gavana wa Benki Kuu, alipokuja alikuja kama gavana wa Benki Kuu, hakuwa mtumishi wa Serikali ya Tanzania, alikuja kama gavana tu," alisema.

Kwa upande mwingine, alipoulizwa kuwa iwapo kuna uchunguzi mwingine wowote unaofanywa katika akaunti nyingine za BoT kutokana na madai kuwa Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) iliyochunguzwa ni sehemu ndogo tu ya ubadhirifu, Meghji alisema kuwa hakuna uchunguzi mwingine unaofanyika.

Alisema kuwa kinachoangaliwa hivi sasa ni ripoti ya mkaguzi kuhusu EPA ambayo imeshasimamishwa na kuwa mambo mengine yataangaliwa pia.

Meghji alisema, baada ya mambo yaliyotokea, kuna haja ya kuangalia kwa kina mahusiano baina ya Benki Kuu, kama taasisi na Wizara ya Fedha kwa upande mmoja na serikali kwa upande mwingine.

Alisema kuwa hilo ni muhimu na kuwa kinachopaswa kuangaliwa kiundani ni sheria ya Benki Kuu iliyopitishwa na Bunge mwaka jana.

Waziri huyo alisema kuwa, suala hilo ni muhimu liangaliwe kwa sababu sheria hiyo inampa uhuru Gavana wa BoT kama mtendaji mkuu wa taasisi hiyo nyeti na pia anakuwa Mwenyekiti wa Bodi ya BoT.

Alisema hilo linapaswa kuangaliwa baada ya kubainika kuwa yeye alidanganywa na aliyekuwa Gavana na kusaini barua iliyokuwa inaonyesha kuwa kampuni ya Kagoda Agriculture Ltd, ililipwa kihalali kwa kazi zinazohusu usalama wa taifa.

Meghji alisema kuwa, BoT inapaswa kuwa huru, lakini uhuru huo unapaswa kuangaliwa na jinsi ambavyo Gavana anafanya kazi na mahusiano yake na Wizara ya Fedha.

Alisema hivi sasa, kisheria, bodi na BoT pamoja na Gavana, wapo huru kufanya mambo yao ingawa kuna wajumbe katika bodi ambao wanatoka nje ya BoT na kuwa hawana haki ya kupiga kura.

Akizungumza na Tanzania Daima jana, Waziri Meghji alikiri kufanya mahojiano na redio hiyo na kusema taarifa alizokuwa nazo ni kwamba Ballali alikuwa akifanya kazi kwa mkataba maalumu, hakuwa mtumishi wa serikali.


http://www.freemedia.co.tz/daima/2008/2/4/habari3.php
 
I thought the governor was the CEO equivalent for a central bank, how ridiculous not to make him a government employee.If he was not a government employee, and indeed he was a contractor, with whom did he enter the contact? To whom was he answerable?

Hogwash!
 
Na nani alikuwa anamlipa mshahara???????? Nna wasiwasi na uelewa wa mama hapo!!!!
 
Nafikiri huyu mama definition ya mwajili na mwajiliwa haielewi sawa sawa.
 
Lakini niliwahi kusikia kuwa Prez Mkapa alimuomba/alimuazima kutoka IMF kuja kuwa mshauri wake na mwishoni akaishia kuwa gavana.
 
Jamani poleni na kazi,
Nina ukata kiasi kwamba siwezi kunununua software, instead inabid nitumie Evaluation Version. Nero Burning Rom inaweza kutatua matatizo yangu. Nimeenda kwenye site hii http://www.soft32.com/download_263.html na kufanikiwa ku-download file (.exe). Wkt wa ku-install hii evalaution version, ninahitajika ku-supply licence key, ambayo sina na hata kwenye site sijafanikiwa kuiona popote. Kuna mtu anaweza kunisaidia wapi naweza kuipata/kuiona hiyo key!
Nawatakia maisha mema sana,
 
Jamani poleni na kazi,
Nina ukata kiasi kwamba siwezi kunununua software, instead inabid nitumie Evaluation Version. Nero Burning Rom inaweza kutatua matatizo yangu. Nimeenda kwenye site hii http://www.soft32.com/download_263.html na kufanikiwa ku-download file (.exe). Wkt wa ku-install hii evalaution version, ninahitajika ku-supply licence key, ambayo sina na hata kwenye site sijafanikiwa kuiona popote. Kuna mtu anaweza kunisaidia wapi naweza kuipata/kuiona hiyo key!
Nawatakia maisha mema sana,

Kuna kasehemu ka IT...labda kama unataka watu wafungue hiyo site uue mjadala kwa virusi!
 
Wanabodi,
Kifupi kama mimi ni rais leo hii mama Meghji angekuwa hana kazi kabisa!
Yaani ndio kazidi kujikaanga mwenyewe...
Ikiwa Balali hakuwa mwajiriwa wa serikali imekuwaje yeye awe na nguvu ya kumlazimisha yeye waziri wa fedha kuweka sahihi kuruhusu fedha za Umma zitumike kwa mabo ya Usalalam amabyo yeye kama sii mwajiriwa hakutakiwa kabisa kuwa na info nazo!...How can someone outside the government anaweza kukughiribu wewe utoe sahihi yako hali huyu mtu yupo under contract!..
Maajabu yanazidi kujitokeza yenyewe.... Duh
 
.........ni "the weakest link" she has to go..........

........"how dare she!!!"...........anataka kutuambia nini hasa,.....................ukiondoa vitu vichache as permanent employee wa serikali.....Conditions of Service kama Gavana wa serikali zinabaki pale pale
 
Back
Top Bottom