Kumbe aliyekuwa anaogopewa ni hayati Magufuli lakini siyo utawala wake, Magufuli Bus Terminal mambo ni vurugu tupu!

Kiukweli hayati Magufuli aliogopwa yeye binafsi na wala siyo utawala wake kwa sababu kuna maeneo mambo ni vurugu tupu lakini watendaji ni wale wale.

Nimefika Magufuli Bus Terminal utaratibu wa ukataji tiketi na mpangilio wa mabasi ni hovyo kabisa.

Kwenye parking ya mabasi yaani wanapaki hadi barabarani na kuzibiana njia, basi la kuondoka saa 12 asubuhi linaweza kuondoka saa 1:15 kwa sababu tu ya kuzibiwa njia na mabasi mengine.

Mkuu wa mkoa liangalie hili.

Pili kwa sababu parking ina uwezo wa kuchukua mabasi 108 na mabasi yanayotoka asubuhi ni zaidi ya 200 basi yaruhusuni mabasi yanayoanzia Shekilango yasiingie hapo stendi kuu Mbezi.

Eid Mubarak!
Magufuli aliwafundisha jinsi ya kufuatilia kero za wananchi lkn wote wamesha sahau, wapo viongozi wachache ambao huwa wanajituma sana ktk kufuatilia kero za wananchi mfano.
Mhe. Awesu, mhe. Mwigulu, Jafo, Biteko, Lukuvi, wa Mifugo, Bashe, Gwajima, n.k,
wengine kwakweli ni kama wamegwaya.

kwani hiyo stendi ipo ktk wilaya gani?
maana hilo ni jukumu la mkuu wa wilaya husika na kamati zake akishindwa ndipo apande juu. lkn wamelala.

ndio maaana tumeona jana Bandarini hadi PM ameenda kutatua kero kanakwamba hamna waziri wala naibu waziri wala katibu mkuu!!
 
Hivi kweli serikali Ijenge stand ya mabasi halafu Rais aje asimamie mipangilio ya mabasi kweli, halafu mtu unakuja kumlaumu mwendazake hii ni akili matope. Sema ustaarabu hatuna full stop. Tumepewa kitu kizuri tuwe wastaarabu.
Yaan awe anatoka alfajir pale ikulu, afike mbezi aanze kupangisha line ya folen ma bus

Sent from my Infinix X652C using JamiiForums mobile app
 
Magufuli alikuwa na rundo la hirizi zilizokuwa zinawatisha mpaka kina Kinana sasa huyu mvaa ushungi kazi anayo
 
Magufuli hakujenga system alijiamini yeye kama yeye. Sasa hii ndio shida sasa.
Hoja kituko na dhaifu kabisa..si hayupo sasa jengeni system mnazotaka..as if system ni automated na haitegemei watu. Mnajificha udhaifu wa usimamizi katika kulaumu asiyekuwapo mpaka lini
 
Bi Samia ana kibarua kigumu mbele yake, inaweza kuchukua karibia miezi 18 kuweza kurudisha Utawala wenye kufuata Sheria na taratibu za Nchi, Magufuli alifanya kazi yeye kama yeye na hakuzingatia maisha ya raia wengine kwa kupuuza au kuzifutilia mbali taratibu za mipango miji.
Ubeti mkongwe huu Magufuli alikuwa hivi alikuwa vile..makasuku mnapokezana tu, napenda wimbo huu muendelee nao sio miaka 5 tu ijayo bali hadi akili zitapowaingia kuwa mnawajibika kutatua changamoto za nyakati zenu kwa kutumia akili zenu
 
Wasipoangalia huyu Mama atamaliza muda wake na kuingia mwengine ila wao watakuwa wanamuimba Magufuli tu.
 
Hilo lipo chini ya Trafik wafanye kama UBT, yaani kuna bus zinazoanza safari saa 11:30 zitoke kwanza kisha za saa 12:00 mbona rahisi sana wale trafiki pale getini kazi yao nini?
 
Magufuli hakujenga system alijiamininyeye kama yeye.Sasa hii.ndio shida sasa
Hoja kituko na dhaifu kabisa..si hayupo sasa jengeni system mnazotaka..as if system ni automated na haitegemei watu. Mnajificha udhaifu wa usimamizi katika kulaumu asiyekuwapo mpaka lini
Hatuwezi kujenga system kwa mwezi.mmoja.Taifa linajenga mifumo yake kwa.muda mrefu na sio siku moja.By the way CCM hiyo hiyo ndio imeshindwa kujenga mfumo imara tangu uhuru.Magufuli hata Angekaa 39yrs bado asingeweza.Halafu huyu mama si alikuwa makamu wake usilete POVU
 
Shida ni viongozi wetu kushindwa kujifunza mazuri kutoka kwa Hayati Magufuli.
Ni vigumu kama hakuwaweka karibu nae.Hata wazazi wasipoweka mifumo imara kwa familia kila kitu hupotea pending wanapokufa.Tujifunze kuanzia ngazi ya familia
 
Kumbuka ki kawaida hapa Bongo kiongozi atajenga system yake anapokuwepo, akimaliza wakati wake ataonekana hafai anakuja mwingine na mfumo wake. Ndo ilivyo kote hata huko katika sekta mbalimbali.
Magufuli alikuwa mkali na hii aliieneza kwa viongozi wake. Mama kaingia kasema system yake ni upole na kubembeleza hivyo waliopo wanafuata mam anavyotaka. Hivyo tusimlaumu Magufuli, kamaliza wakati wake kaondoka. Sasa ni wakati wa Mama Samia. Kubembelezana.
Kwa kweli tumvumilia kila mtu na style yake hatuwezi kufanana hata kama wangezaliwa mapacha.Tujifunze kukubali mabadiliko
 
Kujenga mfumo imara kupitia CCM haiwezekani. CCM wanajua wazi kwamba kama wakijenga taasisi na mifumo imara ndio utakuwa mwisho wao. Magu alitambua hilo ndio maana akaamua kutumia nguvu yake binafsi kuongoza.
Sasa nguvu sio sustainable kwa kuwa ukiondoka unaondoka na nguvu zako.CCM kuna vitu nakubaliana na wewe wanafanya makusuditu ili mfumo uliopo uwanufaishe
 
Magufuli hakujenga system alijiamininyeye kama yeye.Sasa hii.ndio shida sasa

Hatuwezi kujenga system kwa mwezi.mmoja.Taifa linajenga mifumo yake kwa.muda mrefu na sio siku moja.By the way CCM hiyo hiyo ndio imeshindwa kujenga mfumo imara tangu uhuru.Magufuli hata Angekaa 39yrs bado asingeweza.Halafu huyu mama si alikuwa makamu wake usilete POVU
Hoja za kikasuku hizo manju akianzisha wimbo nyote mnaitikia korasi moja mlokaririshwa. Nasema hivi nyimbo yenu ni tamu endelea na korasi ya hakujenga mfumo mpaka siku akili iwaingie
 
Kiukweli hayati Magufuli aliogopwa yeye binafsi na wala siyo utawala wake kwa sababu kuna maeneo mambo ni vurugu tupu lakini watendaji ni wale wale.

Nimefika Magufuli Bus Terminal utaratibu wa ukataji tiketi na mpangilio wa mabasi ni hovyo kabisa.

Kwenye parking ya mabasi yaani wanapaki hadi barabarani na kuzibiana njia, basi la kuondoka saa 12 asubuhi linaweza kuondoka saa 1:15 kwa sababu tu ya kuzibiwa njia na mabasi mengine.

Mkuu wa mkoa liangalie hili.

Pili kwa sababu parking ina uwezo wa kuchukua mabasi 108 na mabasi yanayotoka asubuhi ni zaidi ya 200 basi yaruhusuni mabasi yanayoanzia Shekilango yasiingie hapo stendi kuu Mbezi.

Eid Mubarak!
Pole sana mkuu, kwani mkuu wa mkoa huwa hana watu hapo standi.?
 
Sahau hilo la Samia kufuata sheria.
Bi Samia ana kibarua kigumu mbele yake, inaweza kuchukua karibia miezi 18 kuweza kurudisha Utawala wenye kufuata Sheria na taratibu za Nchi, Magufuli alifanya kazi yeye kama yeye na hakuzingatia maisha ya raia wengine kwa kupuuza au kuzifutilia mbali taratibu za mipango miji.
 
Magu alikuwa ana vituko kweli, alikuwa anazitishia mamlaka zifanye atakavyo, kisha anazitumia mamlaka hizo hizo kufanya kinyume na sheria ili kutimiza utashi wake! Rejea uchafuzi ulioitwa uchaguzi. Matokeo yake, watu wakawa wanafanya wakisikia anaenda maeneo yao, na taarifa zilikuwa zinapikwa ili kumuhadaa.
Ahaaa, ndugu kama ulipoteza vijisenti basi sahau. Hata ngoma ikirudiwa hutoboi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom