Kumbe Aliponea Chupuchupu: Kama Kesi ingepokelewa ICC saa hizi Magufuli angekuwa jela

Mahakama ya MUNGU ni mbinguni. Kwani unavojua wewe JPM asingefanya hayo unayoamin alikosea alipangiwa kuishi miaka mingapi?
Hapa duniani hakuna mwenye mamlaka au uwezo wa kujua kwa nini MUNGU ametaka fulani afe. Acheni kutumia Dini vby.
Unaweza kusema kwa nini Yesu alikufa akiwa na miaka 33 au. Muhamad kuishi 63 yrs.
Hebu tuambie kwenye familia yako waliokufa Watoto Wachanga, Vijana, Watu Wazima na Wazee kabla ya kuitwa Vikongwe walikosea nn wakahukumiwa na MUNGU kufa?

CHUKI ZA KISIASA ZIMETUFANYA TUWE WAJINGA SANA
Hukumu ya Mungu tayari hiyo imeishaaaa
 
Kama hujui dini kaa kimya. Hata huyo shetan ambaye unaamini mungu anamchukia, mbona bado angali hai.
na atakuwepo mpaka
kiama?
Kama una uelewa jenga hoja zenye nguvu na sio kutumia nguvu kujenga hoja
Hutaki kajinyonge
 
Sasa kama alikuwa hai mkashindwa kumfanya chochote, zaidi zaidi mkawa mnakimbia kimbia na kulialia huku na kule..

Kupambana naye akiwa amekufa ni dalili za watu waoga au wale mbwa koko wanaobweka bweka hovyo bila sababu huku wamekunja mkia.....ni bora mkae kimya na kuendelea na mambo mengine, kuendelea kumtajataja huyo jamaa ni dalili za kumkubali kwenye nafsu zenu bila ya wenyewe kujua...
 
Kuendelea kumtajamtaja JPM ni kumzidishia umaarufu aliokuwa nao maradufu yule mwamba...hizi kelele zenu zinamfanya awe maarufu na kuwafanya watu waendelee kuwa na fikra zake au kuzitukuza fikra zake...

Ukweli ambao mtabishana nao sana, binafsi nimefanya research kubwa sana mtaani na kugundua huyu mwamba kweli watu walimpenda na ameacha alama kwao na amekuwa kama SI UNIT kwenye mambo meeengi kwa raia huko mtaani....Nimebahatika kuvuka nchi kadhaa za jirani tangu kifo cha huyu mwamba, ukweli watu wengi nchi jirani walimuelewa sana...

Ukweli mwingine ambao vibaraka lazima muufahamu na mnajidhalaurisha saaana mbele ya hawa mabwana zenu....Hao mabeberu hata huko Belgium wakijifungia wenyewe wanawadharau sana kwa kumpinga yule bwana na kwenda kutafuta msaada kwao maana hata wao wanaamini philosophy za yule mwamba zilikuwa muarobaini wa mambo meengi....

Nilitofautiana baadhi ya mitazamo lakini yule Mwamba alitufaa sana kwenye baadhi ta mitazamo..

RIP JPM , tumuache apumzike tuyaenzi na kushaishi mazuri yake na mengine tumuachie Muumba mbingu na ardhi....
 
Back
Top Bottom