Kumbe Ahmed Rajab kuna wakati taaluma anaweka mfukoni na kuvaa jezi. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kumbe Ahmed Rajab kuna wakati taaluma anaweka mfukoni na kuvaa jezi.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Byendangwero, Apr 30, 2011.

 1. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #1
  Apr 30, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Makala iliyoandikwa na Ahmed Rajab katika Raia mwema ya wiki hii, ambapo pamoja na mambo aligusia hatua ambayo ilichukuliwa na Baraza la wawakilishi ya kupitisha sheria inayoondoa suala la mafuta ya petroli na gasi miongoni ma masuala ya muungano, kwa maoni yangu, imemushushia hadhi yake kama mwana taaluma ambaye anapashwa aandike ukweli ulivyo bila ya kuhegemea kwa upande wowote. Ni jambo lililo dhahiri ya kwamba katika harakati zozote mbinu ni muimu sana. Haki ya mtu au kikundi inaweza kupotea au kucheleweshwa kusiko na lazima kwa kutumia mbinu potofu katika kuwasilisha tatizo linalohusika. Tuchukue hili suala la mafuta na gesi; katiba inatoa utaratibu unaopashwa kutumika katika kuongeza au kupunguza masuala ya muungano. Lakini kwa makusudi kabisa Baraza la wawakilishi liliamua kupindisha utaratibu huo, na sasa baraza hilo linatarajia serikali ya muungano ibariki ubabe huo, hilo haliwezekeni.
   
 2. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #2
  Apr 30, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Then what
   
 3. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #3
  Apr 30, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  yaani mtu akiandika tofauti na wewe basi huyo siyo. this is crazy. mimi nakubaliana naye. sio lazima kila kitu kiwe kile unachotaka wewe.
   
 4. mwankuga

  mwankuga JF-Expert Member

  #4
  Apr 30, 2011
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 329
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Myopic thinking!kama unasema Ahmed Rajab amepotosha alichokiandika,mbona wewe hujaandika chochote ambacho unahisi wewe ni ukweli.Tufike hatua wabongo tuelewe kutoa na kujenga hoja kuliko kulalama.Ukweli ni mmoja na huwa haugawanyiki na wala hakuna anaemiliki ukweli.Toa hoja watu wachambue.
   
 5. m

  mwabaluhi JF-Expert Member

  #5
  Apr 30, 2011
  Joined: Oct 16, 2010
  Messages: 561
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ni kweli. Na pia pamoja na hayo si lazima kile alichoandika huyo unae muunga mkono kiwe ndio ukweli uliotimilifu
   
 6. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #6
  Apr 30, 2011
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Hiyo taarifa uliyoiandika sikuisoma na ningependa sana kuiona. Waweza kui-paste hapa? Tafadhari.

  Namfahamu Ahmed, na nimeanza kusoma makala zake tangu miaka ya 90. Nimemsikiliza mara nyingi ktk vyombo vya habari vinavyomuamini juu ya mambo ya Afrika. Ni editor wa jarida linaloitwa Africa analysis.

  Udhaifu wake mtu huyu ni kwamba hana Analysis yoyote ya mambo ya Afrika kama jarida lake linavyoitwa. Niliwahi kumuomba aliite Africa Critique. Mara zote yeye anahangaika na taarifa za ku-criticize afrika. Hakuna analysis yoyote!

  Kumbukumbu yangu na heshima kubwa kabisa ya analysis ya mambo ya Afrika bado nampa Marehemu Babu, Abdurahman. Huyu Rajabu ni muhangaikaji tu! maandishi yake hayana taaluma yoyote! Hayo ndo yangu.
   
Loading...