Kumbe 2016 tulikopa tril 2.7 Benki ya dunia na tumeomba mingine, huku tunaambiwa ni kodi za ndani.

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,867
PIC+RAIS.jpg



Kwa ufupi
  • Baadhi ya maeneo ya kipaumbele ni miundombinu na hasa ya barabara na reli.
By Mwandishi Wetu, Mwananchi
Benki ya Dunia imejipanga kuendelea kutoa mikopo nafuu kwa miradi ya maendeleo nchini ili kukuza uchumi na kupunguza umasikini.

Mwakilishi wa benki hiyo katika nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia, Bella Bird amesema hayo alipozungumza na Rais John Magufuli.

Bella ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Desemba 4,2017 Ikulu jijini Dar es Salaam na kubainisha maeneo ya kipaumbele kuwa ni miundombinu na hasa ya barabara na reli; kuongeza uzalishaji na usambazaji wa nishati ya umeme; Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) na elimu kwa kujielekeza katika ubora na kuhakikisha idadi ya wanaopata elimu inaongezeka.

Maeneo mengine ni kuboresha sekta ya afya, kuongeza upatikanaji wa maji, usimamizi bora wa ardhi, mawasiliano, huduma za fedha jumuishi, vituo vya pamoja vya Serikali na kusaidia familia masikini.

Bella amempongeza Rais Magufuli kwa usimamizi wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Benki ya Dunia. Amemuahidi benki hiyo itaendelea kushirikiana kwa karibu na Tanzania katika utekelezaji wa miradi mingine.

“Mwaka uliopita Benki ya Dunia ilitoa mikopo nafuu yenye thamani ya dola 1.2 bilioni za Marekani (Sh2.7 trilioni), fedha hizi zimekwenda katika miradi na tunafurahi kuwa inakwenda vizuri na wananchi wanafurahia; kwa sasa tunapanga namna tutakavyotoa mikopo kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za maendeleo katika kipindi kijacho,” amesema Bella.

Rais Magufuli ameishukuru Benki ya Dunia kwa ushirikiano na Tanzania na amemhakikishia Bella kuwa Serikali itasimamia fedha zote zinazotolewa na benki ili zilete matokeo yanayotarajiwa.

Amesema maeneo ambayo benki hiyo imeyataja kuwa ya kipaumbele katika fedha zitakazotolewa ni muhimu kwa ustawi wa Tanzania.

Chanzo: Mwananchi
 
Hata mm nilihisi ni pesa za mkopo lakini ilitakiwa ionekane kuwa ni ukusanyaji mzuri wa kodi kitu ambacho sio kweli. Anyway hiyo sio hoja sana, cha muhimu pesa zilizokopwa zifanyie shughuli sahihi. Tatizo ninaloliona kama tunafichwa ni kiasi gani tumekopa tutajuaje ufanisi wa matumizi ya mikopo?

Ni vyema haya mambo yakawa wazi kwani dunia ya leo ni nadra sana kuficha ukweli labda kama una nia ovu na kutaka sifa zisizo na uhalisia. Pia ni lazima bunge litaarifiwe ni mikopo ya muda gani.
 
Alishaambiwa zile mbwembwe za Tanzania Revenge Authority ni za kupika....hakuna kitu pale....ngoma limeshuka hadi bil 700....zinatosha salary pekeee iliyobakia anakopa kama hana akili....alidhania wenzake wanaiba sana na wanapitisha mizigo bila ushuru....walifika 900bil....sasa anaisoma na yeye....anakopa kila kitu....na bado itashuka zaidi nazaidi.......
 
Kwaiyo ukweli ni kwamba makusanyo yote ya Mwezi yanatumika kulipa Mishahara tu Serikalini..

Serikali inapumulia mashine, vyuma vimekaza hadi upande wao..

Ukweli MCHUNGU ambao hapendi kabisa kuusikia..!!
 
Kwaiyo ukweli ni kwamba makusanyo yote ya Mwezi yanatumika kulipa Mishahara tu Serikalini..

Serikali inapumulia mashine, vyuma vimekaza hadi upande wao..

Ukweli MCHUNGU ambao hapendi kabisa kuusikia..!!
Hii habari Kama inaukweli ndani yake basi imbombo gafu bhamulti.
 
Sasa naanza kuona ni kwanini wapinzani wananunuliwa na kunyamizishwa ni ili wasiongee ukweli. Kukopa sio aibu, labda ukope utumie vibaya hapo ndio kosa.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom