Kumalizika kwa kesi ya Mbowe ghafla, Kumesababisha mapato yangu na Safari za Dodoma Dar kupotea ghafla

GUSSIE

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
3,866
11,100
Wanabodi, Kwa ufupi nikiri kuwa kesi ya Mbowe nilitegemea itafika at least mwezi wa tisa na hii ndio ilikuwa forecast yangu na wengine wengi tu

Sikuwahi andika habari za hii kesi sana kwani mara nyingi huwa naangalia maslahi kwanza, Kwenye maslahi ya pesa hutakiwi kuongea sana utaharibu mambo

Mimi nilikuwa member wa ile kamati ya kufuatilia mwenendo wa kesi hii nyuma ya Pazia iliyoundwa na mheshimiwa mkubwa wa kule toka kwenye korosho na kumpa taarifa ya usahihi kama Jamaa ni terrorist or not

Mara nyingi nilisafiri toka Dodoma Dar nikijipatia haki yangu ya msingi ya safari na mambo mengine kama member wa kamati

Nipo Dodoma Katika harakati zangu zile za PhD za Voda fasta, Hivyo ilikuwa inanilazimu kusafiri toka Dom to Dar kama member wa kamati

Kukatika ghafla kwa huu mnyororo wa pesa za kamati kwa kesi kumalizika ghafla ya Mbowe kumenipa Funzo kubwa sana

Kama mwana ccm nimejifunza mambo mengi sana kwenye kesi hii pia, Vitu kama PGO, Utunzaji wa ushahidi yaani Chain of Custody na umakini wa kujibu maswali


Kumalizika kwa kesi hii sio mimi tu mrija wa pesa umekatika bali hata kuna wanachadema pia wameumia kama mimi, Na kuna maofisa wengi tu hawakutegemea haya

Lakini yote haya yanapita na huu ni mwezi wa kwaresma na kesho ndio jumapili ya kwanza ya kwaresma
 
Shukran hizi pia zimundee putin,

Mama angeshupaza shingo Kama mwenzake Zelensky,

Hakika
Hii kesi ilikua inaelekea kutuzamisha katika Vita ya 3 ya Dunia.
IMG_20220305_175253.jpg
 
Back
Top Bottom