Kumaliza/kupunguza tatizo la maji safi Tanzania

Mparee2

JF-Expert Member
Sep 2, 2012
2,580
4,262
Wote tunafaham kuwa kumekuwa na changamoto ya maji safi ambayo pamoja na juhudi kubwa za Serikali inachukua muda kupata suluhu kwani kila wakipunguza eneo moja kuna eneo lingine linaongezeka kwa upungufu
Tatizo
1. Visima/chemchem nyingi zimekauka/zinaendelea kukauka
2. Kuchimba kisima kwa mashine kuonekana kuwa ni anasa
3. Kufanya Maji ni biashara (Hapa simaanishi watu waache kulipia bili)


Suluhisho

1. Kila Wilaya, Tarafa, Kata, na Vijiji vitambue maeneo yao yenye Chemchem/yaliyokuwa na Chemchem siku za karibuni Wahakikishe wanapanda miti kwenye eneo husika (msitu wa asili) wa ile miti ya maji (isiyokausha maji). Hii ni pamoja na kutoruhusu kabisa shughului za maendeleo katika maeneo ya Chemchem. Kwa kufanya hivyo watajihakikishia visima kuendelea kuwepo. Wilaya inaweza kusaidia kuandaa bustani ya miti husika

2. Watu wenye uwezo wa kuchimba Visima virefu kwa ajili ya matumizi ya nyumbani waruhusiwe bila masharti au pengine mashart nafuu kabisa ya kuwaelekeza waweke mazingira watu wa eneo husika (majirani) waweze kuchota maji kwao bure au Pengine kwa kuchangia gharama za umeme.

3. Wanachi au mtu binafsi mwenye uwezo wa kusambaza maji katika eneo lao wasiingiliwe sijui wawekewe mita nk kwani hiyo ni sawa na kuchota maji kwenye Kisima

4. Serikali iendelee na utaratibu wake wa kupeleka maji maeneo ambayo hayana au hayafiki kwa urahisi na kutoza gharama za uendeshaji
5. Maji yawe huduma na sio Biashara
 
Serikali gani inashindwa hata kutoa maji safi na salama kwenye mji mkuu wake?
 
Back
Top Bottom