Kumalilizika mkutano wa Bunge, yapi yalijiri kuhusu fao la kujitoa?

structuralist

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
1,230
907
Wakuu amani ya Muumba iwe juu yenu.
Natambua kuwa mkutano wa hunge la januari umeahirishwa pengine mpaka mwezi wa nne. Hata hivyo ningependa kufahamu kuwa je kuna kauli yoyote ya serikali ilitolewa kuhusiana na fao la kujitoa?

Binafsi nilibahataika kuona video fupi ya mbunge Heche na katika uwasilishaji wake aligusia juu ya fao hili na kwa pembeni niliona kama waziri anaandika aliyokuwa anayasema Mh Heche hata hivyo sijui kama kulitolewa ufafanuzi ama hivyo kama Kuna mwenye habari zaidi juu ya fao la kujitoa tunaomba atuhabarishe.
 
Kwani walijadili nini zaidi ya Makonda na Wabunge kukamatwa?
Dah mkuu ni kweli kuwa hayo niyo yalotikisa zaidi ila nilidhani labda kuna mjadala kidogo ulifanyika kwenye hoja hii. Ikumbukwe kuwa kuna baadhi ya wabunge walichangia kuhusu fao la kujitoa (sijui walikuwa wanajadili hoja gani haswa) hivyo naamini kulikuwa na ufafanuzi wa serikali kwenye hoja hii. Ngoja tusubiri pengine wengine waliskia tofauti na sisi.
 
Kwa bahati mbaya sana upepo wote umeelekea kwenye unga hivyo hoja hizi na zinginezo hata hazionekani hata hapa JF pia.
 
Kuna mapendekezo yamejadiliw nje bunge na wadau wengi sana wakiwemo vyama wafanyakazi tunasubiri mapendekezo yao.....labda kama wapo humu watakuja kuelezeaa
 
Hili fao la kujitoa nalitegemea sana .... maana hizi kazi za mikataba ni hatari tupu
 
Hili fao la kujitoa nalitegemea sana .... maana hizi kazi za mikataba ni hatari tupu
Mkuu hili fao ni mkombozi kwa wanyonge. Unajua watu wakiwa wanalipwa mishahara mikubwa na marupu rupu ya kutosha basi hawaoni yale wanayopitia watu wa chini. Mtu ana milioni 5 halafu kazi imekoma kisha anaambiwa asubiri miaka 20+ ijayo hii kweli haki?
Wakati angeweza kujiajiri kwenye kilimo na biashara ndogo ndogo tu na maisha yakaendelea vizuri tu. Kwahakika hili jambo halikubaliki.
 
Hili fao la kujitoa nalitegemea sana .... maana hizi kazi za mikataba ni hatari tupu
Kuna wabunge kwenye michango yao hasa Mh Heche nilimskia akiligusia hili fao na nikaona kwa pembeni kama kuna waziri anaandika hoja zile sasa kwakuwa sina access ya vyombo vya habari hasa TV nimeshindwa kuelewa ni kitu gani kilijiri kwenye ufafanuzi wa hoja kutoka serikalini.

Pili ningependa pia kujua ni kwanini mifuko izuie wakati hiyo sheria ya mabadiliko haijapitishwa rasmi na bunge? (na bunge litakuwa la ajabu sana likipitisha sheria ya namna hii)
 
Siku moja wananchi twende bungeni tukajitetee wenyewe sio hawa kenge bendera fata upepo wanaacha kusimamia mambo ya msingi
 
Kuna mapendekezo yamejadiliw nje bunge na wadau wengi sana wakiwemo vyama wafanyakazi tunasubiri mapendekezo yao.....labda kama wapo humu watakuja kuelezeaa

Nakubaliana na wewe mkuu kuwa kumekuwa na mijadala nje ya bunge inayohusu fao la kujitoa. Ila sijui mijadala hiyo inaendeshwa je na wapi ili watu tuweze kutoa mawazo yetu.

Ni muhimu pia kuhakikisha kuwa hili fao haliondolewi. Ukiwa kwenye ajira ya uhakika na haswa yenye maslahi makubwa huwezi thamini hili fao na huwezi jua umuhimu wa fao hili ila ukiwa unalipwa 500000/ tena sekta binafsi ndio utagundua umuhimu wake.
 
Hivi hili fao hata wabunge na rais wameondolewa?
Najaribu kufikiria ni kwa kiwango gani linawagusa.
Hapo ccm wanacheza tu na maisha ya watu
 
Hivi hili fao hata wabunge na rais wameondolewa?
Najaribu kufikiria ni kwa kiwango gani linawagusa.
Hapo ccm wanacheza tu na maisha ya watu
Mkuu kwa uelewa wangu hili haliwagusi. Ila nadhani kama tunatengeneza taifa mabalo litao haki kwa wote nadhani hili fao kama litaondolewa basi liondolewe na kwa wabunge na viongozi wengine. Hivi kama mbunge anauhakika wa kukaa miaka 5 ila akimaliza tu anapewa chake kisha anarudi tena miaka 5 vivyi hivyo anapewa chake, kwanini huyu mtumishi ambaye hana uhakika hata wakukaa miaka 2 asipewe chake akipoteza ama kuacha kazi?

Nadhani ni wakati muafaka wakuleta usawa kwa watu wote. Kama bunge litapitisha hii sheria basi sheria hii itumike kwa watu wote wakiwemo wao. Haiwezekani wao wakimaliza muda wao wapewe chao lakini akini sisi hohehahe ndio tuambiwe tusubiri miaka 60, hili halikubaliki.
 
Siwaamin tena wabunge makonda kafanya wakaonyesha rangi zao
Wabunge ni kawida yao kuwa wakali pale wanapoguswa wao moja kwa moja ila wakiguswa wengine wengi wao hujiweka kando. Unakumbuka hoja ya kodi kwenye mafao yao ilivoleta changamoto bungeni. Nadhani Husseinn Bashe ndiye kumbukumbu zangu zinaeleza kuwa alisema makato hayo yatekelezwe kwa viongozi wote ila hali ilikuwa tete bungeni. Mpaka baadhi ya mawziri wa awamu zilizopita waliwaka na kusema hiyo itakuwa double taxation wakati sisi huku kila siku tunakutana nazo hizo walizoziita double taxation. Hivyo hata kwenye hili wabunge nao wasubiri mpaka wafikishe 60 ndio wapewe hizo fedha vinginevyo kupitisha sheria hii kwa watumishi maskini itakuwa ni unyonyaji wa hali ya juu kabisa.
 
Mkuu kwa uelewa wangu hili haliwagusi. Ila nadhani kama tunatengeneza taifa mabalo litao haki kwa wote nadhani hili fao kama litaondolewa basi liondolewe na kwa wabunge na viongozi wengine. Hivi kama mbunge anauhakika wa kukaa miaka 5 ila akimaliza tu anapewa chake kisha anarudi tena miaka 5 vivyi hivyo anapewa chake, kwanini huyu mtumishi ambaye hana uhakika hata wakukaa miaka 2 asipewe chake akipoteza ama kuacha kazi?

Nadhani ni wakati muafaka wakuleta usawa kwa watu wote. Kama bunge litapitisha hii sheria basi sheria hii itumike kwa watu wote wakiwemo wao. Haiwezekani wao wakimaliza muda wao wapewe chao lakini akini sisi hohehahe ndio tuambiwe tusubiri miaka 60, hili halikubaliki.
Sijui ni lini tutapata watetezi wetu halisi maana naona kitu km hiki kinagusa sana wafanyakazi ila kwa maslahi binafsi (si ya mashirika husika bali ya serikali inayoyafilisi mashirika haya) wanatuwekea vikwazo kwenye hela zetu......
WANGEJU NILIVONA HASIRA NA HILI SWALA ACHA TU???!!!!!
 
Mkuu inauma sana kwakwli.
 
Back
Top Bottom