Kulwa Masanja Isenge anyakua milioni 5 katika Shindano la 'Stories of change' 2022

JamiiForums

JF Official Account
Nov 9, 2006
6,202
4,991
Baada ya takriban miezi 4 ya kusubiri kumjua atayejishindia zawadi ya andiko bora kwenye kinyang'anyiro cha storie of change 2022 siku imefika, leo ndio leo, washindi watatangazwa na kupewa zawadi zao.

Mshindi wa Shindano la “JF Stories Of Change” atakayejinyakulia kitita cha Tsh. Milioni 5 anatarajiwa kutangazwa na kupewa kitita hicho Jioni ya leo November 18, 2022 katika hafla fupi itakayoanza saa 12 jioni Jijini Dar. Washindi 20 kukabidhiwa zawadi siku ya leo jioni.

Zawadi kwa washindi zitakuwa kama ifuatavyo:-

Mshindi wa Kwanza Tsh. 5,000,000
Mshindi wa Pili Tsh. 3,000,000
Mshindi wa Tatu Tsh. 2,000,000
Mshindi wa Nne Tsh. 1,000,000
Mshindi wa Tano Tsh. 500,000
Mshindi wa Sita hadi kumi Tsh. 300,000
Mshindi wa Kumi na Moja hadi wa Ishirini Tsh. 200,000

Kuhusu Shindano hili


Jamii Forums (JF) ilitoa nafasi kwa wadau wake na wananchi wote wenye uwezo wa kutayarisha maudhui kushiriki kwenye shindano la uandishi wa maudhui mtandaoni wenye kuleta mabadiliko (Stories of Change 2022) kwa awamu ya pili.

Shindano lilikusudia kuongeza maudhui bora mtandaoni hususani ya lugha ya Kiswahili kwa ajili ya vizazi vya sasa na vya baadaye.

Pia, shindano lililenga kuhamasisha ushiriki wa raia pamoja na makundi yasiyopewa vipaumbele kama watu wanaoishi na ulemavu kushiriki katika ukusanyaji na utayarishaji wa taarifa nchini.

Shindano hili lilianza Julai 15 hadi Septemba 15, 2022

Zaidi soma: Uzinduzi wa Awamu ya Pili ya Shindano la Stories of Change(2022)

Tutawapa live kinachojiri katika utoaji zawadi kwa Washindi kutoka ukumbini kupitia huu uzi.

Storie of change 2022 mambo ni motoooooo. tukutane jioni.

Awamu ya kwanza ya shindano hili lilifanyika mwaka 2021, Soma: Stories of Change: Golder Anael Mmari ashinda Tsh. 5,000,000/- toka JamiiForums, katika awamu ya kwanza Golder Anael Mmari alitwaa ushindi. Je, nani leo kulala na kicheko?

Tukutane jioni ya leo.
IMG_20221118_190432_246.jpg


Hafla imeanza


Mgeni Rasmi Waziri, Nape Mnauye anaingia ukumbini muda huu, ameongozana na Mkurugenzi wa Jamii Forums, Maxence Melo pamoja na wageni waalikwa wengine.

Maxence Melo atambulisha wageni waalikwa na kumkaribisha mgeni rasmi
Mkurugenzi wa Jamii Forums, Maxence Melo anatambulisha pamoja na kuwakaribisha wageni waalikwa waliofika kwenye hafoa hii, wapo, bodi ya Jamiiforums, Balozi mbalimbali na wengine wengi.

Pamoja na kutangazwa washindi pia leo Jamiiforums, inazindua mfumo wa kuhakiki uhakika wa taarifa yaani Jamii check, katika mfumo huu wananchi wataweza kuuliza, kuperuziau kuuliza uhakika wa taarifa zilizopo mtandaoni ili kuepuka kuamini uzushi au kuwa na taarifa zisizo sahihi - Maxence Melo

Jamii Check itakuwa hewani leo kuanza kutumika, kama ni mwanachama wa Jamiiforums, hutatakiwa kufungua akaunti mpya kwa kuwa Jamiicheck ipo pamoja na Jamii forums ila kamahuna akaunt utatakiwa kufungua akaunt na kuweza kutumia.

Mgeni rasmi, Nape Mnauye akaribishwa kutoa neno

Natumia fursa hii kuwapongeza washindi, na pia nawapongeza Jamiiforims kwa kuzindua jukwaa la Jamii check na kuandaa shindano hili la Stories of change, ambalo linasaidia kuongeza maudhui bora mtandaoni.

Natoa wito kwa watu kushiriki kuandika au kuandaa maudhui mitandaoni kwani katika ulimwengu huu wa teknolojia hiki ni kitu muhimu.

Katika mazingira haya ya kidigitali mtu anaweza kuandika chochote mtandaoni ivyo kuwepo kwa Jamii check itasaidia kuweka usahihi wa habari rasmi na kuepeusha Uzushi.

Jamii forums mmesaidia kazi ya Wizara yangu maana tutapaga sehemj ya kujua ukweli wa taarifa, kwa niaba ya Serikali Jamiiforums mmefanya kazi nzuri na mnachagia katika kuufanha mtandao kuwa salama, ndio maana nimeona nije, na mimi ni mwanachama wa JamiiForums na nasoma mabo mengi sana japo wakati mwingine nasemwa ila nasoma.

Shindano hili la Stories of Change, tangu limeanzishwa limeibua mambo mengi mazuri na yanafanyiwa kazi na Serikali, hivuo mzidi kuandika na kusema na nawahakikishia Serikali inafurahishwa na kuna sheria ya ulinzi wa taarifa binafsi unakuja na sheria hiuo ni mchango wa Jamiiforums, na wadaj wengine, hivyo Jioji ya leo natambua mchango wa Jamiiforums katika Taifa hili.

Pia katika sheria hiyo, kuna mambo yameongezeka wanataka kuwekwe usawa wa kijinsia, na nimelivhukua na nitalifanyia kazi, kwa kweli Jamiiforums inaoeta mawazo mazuri na nawapongeza katika ushiriki huu kwa jamii katika kuhakikisha jamii inakuwanna sehemu salama ya kuishi.

Nimefurahi, kuwepo hapa jioni ya leo na nawashukuru sana kwa mwaliko. Asanteni.
_____

Kwa sasa kuna mapumziko mafupi na burudani ya muziki Kabla ya zoezi la kutangaza washindi kuanza.

Maxence Melo na Mgeni Rasmi wakaribishwa kwa ajili ya kuanza kutangaza washindi

Washindi wa Stories of change


Mshindi wa 20. Daraja la miti ,
Andiko lake SoC 2022 - Mambo muhimu ya kuyafahamu kabla ya kuomba wazo la biashara mtandaoni

Mshindi wa 19. Nsama
Andiko lake SoC 2022 - Nimfiche wapi Binti yangu?

Mshindi wa 18. Hamza Iddy Nsiha
Andiko lake SoC 2022 - Kilio changu katika sekta ya Afya

Mshindi wa 17. Respick Hugolini Tairo
Andiko lake SoC 2022 - Elimu nchini ikombolewe kwanza ili iweze kumkomboa Mtanzania

Mshindi wa 16. Stephen Ngalya Chelu
Andiko lake SoC 2022 - Natamani kufumba macho, lakini ni nani ataisimulia leo katika kesho yenye mpasuko?

Mshindi wa 15. Buddah07
Andiko lake SoC 2022 - Masaa 3! mtihani wa masaa 3 tu imekuwa sababu ya kuwaacha vijana wengi wa Kitanzania wakitapatapa mtaani bila tumaini

Mshindi wa 14. Charles Shauri
Andiko lake SoC 2022 - Kwenye Ujasiriamali wangu, nalenga kwenye bidhaa na huduma zangu nipate sarafu na sio noti

Mshindi wa 13. Gilbert Anthony
Andiko lake SoC 2022 - Tusasishe mila na desturi zetu

Mshindi wa 12. Marko Mabula Kaswahili
Andiko lake SoC 2022 - Matumizi ya teknolojia ya viumbe hai wadogo (Bacteria na Archaea) katika uchimbaji madini katika kutunza mazingira na viumbe hai

Mshindi wa 11. Constantine Samali Mauki
Andiko lake SoC 2022 - Matumizi mabaya ya Rasilimali Asili ni Chanzo cha Mabadiliko ya Tabianchi

Mshindi wa 10. James William Godfrey
Andiko lake SoC 2022 - Matumizi ya Sayansi na Teknolojia katika kuhifadhi mazao ya kilimo yanayoharibika haraka mfano matunda na mboga za majani

Mshindi wa 9. Jeremia Mathayo Mahenda
Andiko lake SoC 2022 - Mfumo utakaosaidia uendeshaji na usimamizi wa taarifa muhimu kwa Serikali za Mitaa katika kila Kata ndani ya Wilaya

Mshindi wa 8. Agathon Abdon Ndaala
Andiko lake SoC 2022 - Hongera Serikali kwa mikopo ya Halmashauri: Kuwepo na elimu zaidi, ufatiliaji na uboreshwaji wa kanuni wenye kuendana na mazingira na uhitaji

Mshindi wa 7. Timothy Peter Msuya
Andiko lake SoC 2022 - Mama wa nyumbani au Kiwanda kilichojificha?

Mshindi wa 6. Baraka Emmanuel Mhembano
Andiko lake SoC 2022 - Utitiri na uholela wa ufungaji wa ‘cctv’ katika maeneo mbalimbali unavyohatarisha haki ya faragha ya taarifa za watu


Mshindi wa tano ni philibert Moshi Bisama

Ameshinda Shilingi laki tano

Andiko lake ni: SoC 2022 - Mtoto ndani ya giza jeusi

Mshindi wa nne ni Abeid Othman

Amejishindia Shilingi milioni 1

Andiko lake ni: SoC 2022 - Madarasa ya TEHAMA muhimu Shuleni

Mshindi wa tatu ni Nathaniel Atanas Mpasi

Amejishindia Shilingi milioni 2

Andiko lake ni: SoC 2022 - Mfumo Huru wa Kompyuta wa Kupigiana Kura. Jina La Mfumo: Fair Election (FAEL)

Mshindi wa pili ni Rayson Julius Mkelame

Amejishindia Shilingi milioni 3

Andiko lake ni: SoC 2022 - Jinsi harufu ya Simba inavyoweza kukomesha migogoro ya wakulima na wafugaji

1. Mshindi wa kwanza ni Kulwa Masanja Isenge

Amejishindia kiasi Cha Shilingi milioni 5

Andiko lake ni: SoC 2022 - Nilivyobuni kifaa cha kutatua changamoto ya malipo ya bili za Umeme kwa wapangaji
 
Back
Top Bottom