Kulipia Daraja la Nyerere Kigamboni

Hivi hakuna namna serikali inaweza kufanya ili kuwapunguzia mzigo wananchi wa Kigamboni wanaolazimika kulipia daraja wavuke kwenda kwao on a daily basis?

Serikali inaweza kulipa deni hilo kwa NSSF kupitia kodi za wananchi maana madaraja mengine yamejengwa kwa kodi za wote. Yaani mlipa kodi Kigamboni amechangia ujenzi wa daraja la Mkapa na Busisi, kwanini walipakodi wa huko wasichangie la Kigamboni?

Alternatively, orodha ya wananchi wanaoishi Kigamboni wanaopita na magari ingejulikana halafu wangekuwa wanalipa kwa mwaka hata 100,000/= halafu wanaepuka usumbufu wa kulipia kila siku.

Kazi iendelee
Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jamani tuweni WAZALENDO kumbuka gharama za ujenzi wa daraja la Nyerere zimekopwa kutoka kwenye Taasisi ya Serikali yaani NSSF kwahiyo ni WAJIBU kurudisha mkopo ukilinganisha na gharama za Vivuko ambazo Fedha yake inatoka Serikalini na bado Wananchi wanalipia ili kurudisha gharama
 
Kama hutaki kulipa, pita Kongowe...

Maana hata sisi wengine tunaona bora tu mlipishwa sababu pesa iliyotumika kujenga daraja ni ya wananchi wote hata ambao si wakazi wa Kigamboni...
 
Kama hutaki kulipa, pita Kongowe...

Maana hata sisi wengine tunaona bora tu mlipishwa sababu pesa iliyotumika kujenga daraja ni ya wananchi wote hata ambao si wakazi wa Kigamboni...
Aisee! Siku hizi ipo njia unaingilia Kijichi unatokea Mikwambe mbele kidogo ya Kibada.
 
Hoja ya kuwa ilijengwa kwa fedha za wastaafu wa nssf sioni mantiki yake ktk kulipia, labda hoja ya kuwa ni mkataba usiovunjika kuwa nssf watakusanya maduhuli kwa miaka. Kama tunataka za kulipa wastaafu tupeleke bungeni ktk bajeti ili tuwe na uhakika deni ni kiasi gani ili makusanyo ya kodi ya kila mwezi tuwe tunatenga pasenti kwenda kulipia daraja.

On another note, nakubaliana na mjumbe hapo juu kuwa ipo haja deni lijulikane ni kiasi gani, imelipwa kiasi gani, imebaki ngapi na italipwa hadi lini
 
Back
Top Bottom