Kulipa Kodi ya Mwaka Mzima ni Poa au Kunaumiza? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kulipa Kodi ya Mwaka Mzima ni Poa au Kunaumiza?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mnhenwa Ndege, Aug 13, 2009.

 1. Mnhenwa Ndege

  Mnhenwa Ndege JF-Expert Member

  #1
  Aug 13, 2009
  Joined: Dec 5, 2007
  Messages: 243
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  [​IMG]
  [​IMG]

  Gazeti la Uhuru linaendelea hivi
  Wanaotumia fedha za umma kulipia pongo. "licha ya kwamba za Dar es salaam na kwengineko nchini hazina hadhi ya kulinda haki ya mtu kuishi katika mazingira safi salama, si halali kisheria kwa mwenye nyumba kutoza kodi kwa kipindi zaidi ya mwezi mmoja kwa mara moja, tena kabla ya mpangaji hajakaa kwenye nyumba. Soma zaidi......

  "Ni kosa kubwa kumlazimisha mtu alipe kodi ya mwaka, hana uwezo au fedha hizo. Sheria tunayo tatizo hatuna watekelezaji hizi sheria," alisema Kahangwa. (mwisho wa kunakili gazeti)

  Imegundulika kuwa watu (hususana vijana) wanaoanza maisha inakuwa vigumu sana kumudu gharama halisi za kuishi. Utakuta mtu anapoanza kazi analipwa mshahara pengine Tsh 300,000 kwa mwezi. Kodi ya nyumba ni Tsh 75,000 kwa mwezi ila anatakiwa alipe Tsh 900,000 ambayo ni kodi ya mwaka (hapo fee ya dalali hatuja hesabu). Vijana wengi hukopa ili waweze kumudu gharama halisi. Wengine hukopa mikopo ambayo marejesho ni ya miaka mitatu kisha akalipa kodi ya mwaka wa kwanza. Mwaka unapomalizika kijana husika hukwama maana mkopo haujafikia hata nusu na anatakiwa alipekodi ya mwaka mzima tena. Hali hii huchangia watu kujihusisha na mbinu mbadala za kujipatia fedha, ambazo mbinu nyengine huwa kinyume na sheria.
   
 2. Wa mmoja

  Wa mmoja Member

  #2
  Aug 18, 2009
  Joined: Aug 4, 2009
  Messages: 99
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kulipa kodi kwa style hii kunaumiza sanaaaa!Hata hivyo ni vizuri mtu akatafuta nyumba ambayo ataweza kulipa kodi na si kutafuta nyumba ambayo kodi yake ipo juu kuliko kipato achokipata.
   
 3. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #3
  Aug 18, 2009
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Sikuwa nafahamu hivi ndivyo sheria inavyoelekeza.

  Mkenya mmoja alikuwa anashangaa jinsi wabongo wanavyoweza kuvumilia huu utaratibu wa malipo ya kodi ya nyumba za kupanga. Alionekana kushangaa zaidi kuona kwamba pale nyumba inapohitaji matengenezo kwa mfano, mpangaji anakuwa hana jeuri ya kumshinikiza mwenye nyumba kufanya repair.
   
 4. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #4
  Aug 18, 2009
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Hawa NCCR nao ni hovyo tu. Wanasheria wanao, tena huenda wanaishi kwenye hizo nyumba za kupanga. Wameshindwa kuonesha mfano kwa vitendo? Peleka kesi mbili au tatu mahakamani to create awareness!

  Too much talking, and what have they accomplished so far?!
   
Loading...