Kulipa bima ya gari na kuacha kulipia bima ya nyumba zao tatizo ni nini?

MPUITI

Member
Sep 24, 2011
20
1
Naomba wana JF mnifahamishe juu ya hili: Kwa Watanzania wanaomiliki vyombo vya usafiri kama magari, wengi wao na kama si wote wamelamika kilipia bima magari hayo ambayo kwa hesabu ya kawaida thamani yake huenda ikawa ni ndogo ukilinganisha na nyumba ambamo wanaishi. Thamani ya nyumba zao ni kubwa kwani ndiyo sehamu pekee ambamo familia nzima inaishi na vitu vingi vya thamani vimo humo. Swali langu ni je? kwanini watu hao hawafikirii kulipia Bima nyumba zao? Tatizo ni nini? au kwa nini Shirika la Bima lisifikirie kuweka msisitizo na kuhamasisha wanachi kulipa Bima ya nyumba zao badala ya kulipia vyombo vya usafiri pekee? Pia, kwanini jeshi la polisi lisifanye msako na kuwakamata watu ambao hawalipii Bima nyumba zao badala yake wanahangaika na wenye vyombo vya usafiri pekee?
 
Back
Top Bottom