Kuliokoa taifa twahitaji wanaharakati, si vyama na wanasiasa

Remmy

JF-Expert Member
Jun 9, 2009
4,703
1,797
Kwanza niunge mkono hoja ya mwandishi Joseph Mihangwa kwenye gazeti la Raia Mwema la Septemba 7. Ni kweli watanzania kwa hali tuliyofikia hatuwahitaji tena wanasiasa katika kuleta maendeleo bali wanaharakati, nina nukuu maneno yake machache mwandishi, anasema

"Viongozi wetu wamekubuhu kwa maovu, dharau na kukebehi umma, kwao kashfa za kiuongozi si jambo la aibu wala la kutisha tena; bali kwao ni sifa kuonyesha kwamba wao ni wanaume wa shoka, hawana mchezo. Kwao hoja za wananchi ni dua la kuku lisiloweza kumdhuru mwewe".

Hivyo basi tunawahitaji wanaharakati zaidi na si wanasiasa, na tukiwaangalia wanaharakati wengi wamefanikiwa kwenye harakati zao.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom