Kulinganisha Njia Mbalimbali za Kupata Elimu

Mlenge

R I P
Oct 31, 2006
2,125
2,291
NGAZI YA ELIMU(1) UFUNDI STADI(2) UFUNDI(3) VYUO VIKUU(4) UTAALAMU(5) ELIMU HAINA MWISHO
10​
Shahada ya UzamivuShahada ya Uzamivu<<===
9​
Shahada ya UzamiliShahada ya UzamiliCheti cha Utaalam Ngazi ya 4 (Utaalamu Bingwa 2)<<===
8​
Shahada ya KwanzaShahada ya KwanzaCheti cha Utaalam Ngazi ya 3 (Utaalamu Bingwa 1)<<===
7​
Diploma ya JuuDiploma ya JuuCheti cha Utaalam Ngazi ya 2<<===
6​
Diploma ya KawaidaDiploma ya KawaidaCheti cha Utaalam Ngazi ya 1<<===
5​
NTA Level 5
FTC (zamani)
Cheti cha Kidato cha 6Cheti cha Utaalam Ngazi ya Fundi Mchundo 2<<===
4​
NVA III

VTC Gredi I (zamani)
Cheti cha NTA Level 4
GCE (zamani)
Cheti cha Kidato cha 4Cheti cha Utaalam Ngazi ya Fundi Mchundo 1<<===
3​
NVA II

VTC Gredi II (zamani)
<<===
2​
NVA I

VTC Gredi III (zamani)
<<===
1​
ELIMU YA MSINGI<<===
 
Ziko njia tano za kujipatia Elimu hapa Tanzania. Tutazichambua njia moja baada ya nyingine.

Hapa tutaweka mambo mtambuka kuzihusu.

Maandishi haya ni sehemu ya uelimishaji umma.

//Viambatisho: Baadhi ya Rejea
 
Attachments

  • 10.5923.j.ijcem.20200902.03.pdf
    913.5 KB · Views: 42
  • RPL DSM 2017.pdf
    183.5 KB · Views: 14
  • wcms_744730.pdf
    7 MB · Views: 16
  • Curr_NTA-Level-4_27.pdf
    2.1 MB · Views: 16
  • REGULATIONS-NATIONAL-TECHNICAL-AWARDS.pdf
    163.9 KB · Views: 13
Njia ya kwanza ya kupata elimu, ni ya ufundi-stadi (Vocational). Mazoea yalikuwa ni kwamba mhitimu wa shule ya msingi angeweza kwenda chuo cha ufundi (VTC) na kujifunza kuhusu fani apendayo. Sifa ya kujua kusoma, kuandika na kuhesabu ndiyo iliyokuwa sifa kuu. Ikiambatana na cheti cha kuhitimu elimu ya msingi.

Kwa kuwa mtu aliyejiunga alianzia mwanzo, mtu yeyote angeweza kujiunga.

Gredi 3 (siku hizi NVA 1), Gredi 2 (siku hizi NVA 2) na Gredi 1 (siku hizi NVA 3). Kwa wastani, kila mhitimu angeweza kupata Gredi moja baada ya mafunzo ya mwaka mzima.

Kwa sasa, baadhi ya watu huiona njia hii kama chaguo la mwisho, la mtu aliyeshindwa kupata elimu kwa njia nyingine jadiliwa.

Baada ya Gredi 1 (NVA 3) hakuna njia inayoeleweka ya kujiendeleza kwenye mafunzo ya ufundi.
 
Njia ya pili ya kujipatia elimu ni ya ufundi (Technical). Njia hii ilipokea wanafunzi waliohitimu mafunzo ya sekondari za ufundi (GCE). Kwa sasa hupokea wanafunzi waliohitimu sekondari za kidato cha nne na kwa baadhi ya kozi, hupokea waliohitimu ufundi (NVA 3).

Apitiaye njia hii, huweza kujiendeleza kwenye fani husika mpaka kiwango cha shahada ya kwanza, pili na tatu.

Hivyo, inawezekana kabisa kwa mtu ambaye hakusoma shule ya msingi, au aliyeishia darasa la saba, kujifunza ufundi mpaka ngazi ya gredi 1 (siku hizi NVA 3), na kisha kuhamia njia hii ya ufundi-mchundo akianzia ngazi ya nne (NTA 4). Kwa mtazamo wangu, kama mtu alihitimu NVA3 angetakiwa aweze kujiunga moja kwa moja NTA 5 kwa fani husika.

Hata hivyo, japokuwa ngazi ya nne ya njia hii ni sawa (au kubwa kidogo kuliko kidato cha nne), cheti cha njia hii hakiheshimiwi ipasavyo sokoni, hasa kwenye utumishi. Utaona kila mahali panadai cheti cha kidato cha nne. Ambapo mtu aliyepitia njia hii asipokuwa nacho huonekana ni mbabaishaji, na hawezi kuajiriwa. Baadhi ya vyuo vyenye kutoa elimu ya ufundi navyo hudai cheti cha kidato cha nne kwa baadhi ya kozi au kama sharti la kuajiriwa kama mwalimu kwenye vyuo hivyo.
 
Njia ya tatu, ni elimu ya vyuo vikuu. Ndiyo njia pendwa ya kupata elimu. Njia hii huanzia elimu ya msingi, ambayo kila mtoto hulazimishwa kuipitia. Mtoto akipitishwa njia nyingine za elimu mbali na hii, wazazi huweza kushitakiwa mahakamani, na kukumbwa na adhabu kali iwe fundisho :D.

Njia hii ndio ELIMU, kwa inavyoonekana. Zamani ukipitia njia hii, uligombewa na taasisi mbalimbali za umma zikitaka kukuajiri. Ngazi ya nne ya elimu hii (kidato cha nne) ndio takwa la kudahiliwa vyuo vya elimu ya juu na hata kupata ajira kwenye utumishi wa umma.

Jinsi njia hii inavyoonekana ndio yenyewe, hata uwe na elimu ngazi kubwa kuliko ya nne, lakini umepitia njia nyingine za kupata elimu, utaonekana hujui wala huwezi, na tena utaulizwa uliwezaje kufika huko juu bila kupitia njia hii. Na baadhi ya njia zingine za kupata elimu zimeingia kwenye mtego wa kudai cheti cha kidato cha nne kwa ajili ya walimu au wanafunzi.

Ni njia hii ambayo wazazi huwa radhi kuingia gharama kubwa kuhakikishwa watoto wao wanaipitia. "Elimu" mara nyingi humaanisha njia hii. "Nataka mwanangu asome!" humaanisha "nataka mwanangu apitie njia ya vyuo vikuu".

Huwa pana tafrani baadhi ya familia, pale mzazi anapotaka mtoto wake "asome", mf. atoke kidato cha nne aende cha tano; na pale mtoto anapotaka "akajifunze" kwa kupitia njia nyingine, kama vile ya elimu ya ufundi.

Wanaofikia ngazi ya nane ya njia hii (digrii) au kuzidi hapo huaminika wana fursa nyingi. Baadhi ya fursa hizo ziko kisheria ("lazima uwe na digrii ili uweze kuwa..."). Zamani njia hii, hasa digrii, ilikuwa ni njia ya uhakika wa kupata ajira (serikalini au mashirika ya umma na taasisi zengine za serikali.)

Utakuta kijana aliyepata matokeo yasiyomridhisha kwenye njia hii, huwa radhi kurudia mitihani mpaka "afaulu" na kupata cheti kinachomuwezesha kuendelea na masomo ya njia hii.

Njia hii kwa siku hizi iko "overrated" kama wasemavyo baadhi ya watu.
 
Njia ya nne ni ya elimu ya Utaalam (Professional). Njia hii ni fursa kubwa sana ambayo wachache huitumia. Njia hii huwafanya walioipitia kuwa wataalam, na aghalabu wasio na changamoto ya ajira.

Njia hii huwezesha mhitimu kupata kutambuliwa na bodi husika ya utaalam, na hivyo kupata ruksa ya kutumikia umma kwenye fani husika.

Njia hii haina mikingamo. Unaweza kujiunga bila kujali ulipitia njia ipi ya elimu, na uliishia ngazi ipi. Mtu yeyote anakaribishwa. Mwishoni mwa njia hii mhitimu huweza kufikia ngazi ya tisa ya elimu.

Kwa kuwa baadhi ya fani hulazimisha mtu awe amefuzu kwa kupitia njia hii, wale waliopitia njia ile pendwa ya elimu hulazimika nao pia kupita tena kwenye njia hii. Mara nyingine hukutana na wale walioachana ngazi za zamani huku wapo, wamewatangulia au wako pamoja.
 
Njia ya Tano ya kujipatia elimu ni ile ya Elimu Haina Mwisho (Lifelong Learning). Kwenye njia hii mtu hujifunza na kuwa mahiri kwenye kitu, pasipo kuingia darasani.

Kwa mfano, asilimia kubwa ya watakaosoma maandishi haya ni wazungumzaji wa Kiswahili. Hawakufundishwa na mtu darasani namna ya kuzungumza Kiswahili. Japo yawezekana walikutana na somo la "Kiswahili" darasani, walijifunza zaidi taaluma ya lugha (linguistics) zaidi kuliko kujifunza lugha yenyewe (language).

Mambo mengine ya kujifunza mwenyewe hali kadhalika yanaleta umahiri kwa mhusika. Kwa kutambua hayo, zamani fani watu walijifunza kwa wanaoishi kwa kutumia fani hizo. Mfumo wa uanagenzi (apprenticeship). Mifano iko mingi:

1. Michael Faraday. Huyu alijifunza mwenyewe mambo ya umeme kwa kusoma vitabu. Na kisha akawa mwanagenzi wa Humphrey Davy.

Faraday sasa ni jina kubwa kwenye sayansi. Lakini hakuwa na digrii :D

2. Mafundi magari -- wengi wa wasomaji hapa watakuwa wanapeleka magari yao kwa mafundi waliojifunzia gereji. Siyo waliotoka kwenye vyuo vya mafunzo ya ufundi. Mafundi hao huwaona wenzao waliotoka vyuoni kama ambao ni "mafundi wa vitabu". Ukiongea nao watakupa stori nyingi za mafundi "wa vitabuni" wanavyoshindwa kutatua matatizo ya magari, kutokana na wao kukariri mambo ya vitabuni yasiyoendana na uhalisia.

3. Mafundi nguo -- kama ulipeleka kwa fundi mtaani akushonee nguo, uwezekano mkubwa fundi huyo alijifunza kwa fundi mwenziwe. Fundi mmoja alipata kuniambia kwamba mafundi nguo "wa vitabuni" wanapohitimu wanaweza kushona kaptura tu. Sijui kama ni ya kweli hayo.

Jamii toka kale na kale zilikuwa zikichukua watoto na vijana na kuwaweka kwenye uanagenzi wa fani mbalimbali husika kwenye jamii hizo.

Kwa sasa kwenye ulimwengu wa utandawazi na maendeleo ya tekinolojia, elimu kubwa imerudi kuwa wazi kwa anayetaka kujifunza. Kwenye baadhi ya fani, wajifunzao wenyewe huwa na umahiri na weledi mkubwa zaidi kuliko wenye vyeti vya kuhitimu.

Na elimu sasa imewekwa wazi (Open Education), na ambapo mtu anaweza kujifunza kitu chochote.

Kwa hiyo, kwa kuzingatia yote haya, mtu ambaye hakuenda darasani anaweza kuwa na umahiri sawa na mtu wa ngazi ya 10, 9, 8... hata ya 1.

Njia hii ya tano imeanza kutambuliwatambuliwa. Pana utaratibu wa kutambua waliopitia njia hii (Recognition of Prior Learning, RPL). Lakini bado safari ndefu.
 
Mtoa mada ahsante kwa mada yako nyeti sana, nianze kusema awali nilihisi umechanganya sehemu ya ufundi mchundo na ya ufudni kuwa umefanya vice versa, lakini nahisi nmeelewa japo sijui kama iko sahihi sehemu ulizoziweka, ila umefafanua vyema kwa kila njia, nami niongezeee kidogo kwa uelewa wangu na nliyoyaona.

1. Kuhusu njia ya Ufundi ambapo mtu anafikia hadi kuwa na NVA3 japo katika ufundi kwenyewe hawajaweka muendelezo baada ya hapo lakini katika general education, niseme kifupi labda katika muongozo wa Elimu ya Juu chini ya TCU wanatambua mwenye NVA3 ktk kupata Bachelor, mfano, ili uweze kujiunga Bachelor Degree lazima uwe na cheti cha form four chenye angalau D 4, ila kama una cheti cha form four ila D hazijafika 4, labda ziko mbili au tatu ili uendelee hadi Bachelor Degree yakupasa uwe na NVA3 then hiyo Diploma (NTA 6) hivyo kwa wenye NVA3 wana fursa ya kuendelea zaidi pia.

2. mwishoni kbs nmeona umeandika kuhusu RPL, hii nmeiona nchi nyingi iko applicable na hapa kwetu kuna muda ilkua applicable na tuliona hata Eric Shigongo akinufaika na hii hata kupata Bachelor Degree yake, lakini then wakaifuta, nafkiri hapa TCU wana haja ya ku-review na kuirudisha hii kitu maana ina umuhimu mkubwa sana.
 
Kuhusu pointi namba 1, Vocational Education (Ufundi Stadi) na Technical Education (Ufundi) wakati mwingine huchanganywa sehemu moja.

Kuhusu pointi namba 2, ufumbuzi ni kuanzishwa kwa Mamlaka ya Kulinganisha Elimu (National Qualifications Authority, NQA), kama ambavyo Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) 2015 inavyosema:

Na pia Sera ya Utumishi wa Umma iseme kiwango cha chini cha elimu ya mtumishi aliyeajiriwa baada ya mwaka 2004 iwe ngazi ya nne ya elimu kama ilivyoainishwa kwenye NQF au kama itakavyotafsiriwa na NQA. Ngazi ya nne inaweza ikawa NVA3, Kidato cha Nne, RPL, NTA 4, au ngazi fulani ya utaalamu. Badala ya ilivyo sasa ambavyo sera inatambua kifungu kimoja tu cha ngazi ya elimu (kidato cha nne).
 
Kuhusu pointi namba 1, Vocational Education (Ufundi) na Technical Education (Ufundi-Mchundo) wakati mwingine huchanganywa sehemu moja.

Kuhusu pointi namba 2, ufumbuzi ni kuanzishwa kwa Mamlaka ya Kulinganisha Elimu (National Qualifications Authority, NQA), kama ambavyo Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) 2015 inavyosema:

Na pia Sera ya Utumishi wa Umma iseme kiwango cha chini cha elimu ya mtumishi aliyeajiriwa baada ya mwaka 2004 iwe ngazi ya nne ya elimu kama ilivyoainishwa kwenye NQF au kama itakavyotafsiriwa na NQA. Ngazi ya nne inaweza ikawa NVA3, Kidato cha Nne, RPL, NTA 4, au ngazi fulani ya utaalamu. Badala ya ilivyo sasa ambavyo sera inatambua kifungu kimoja tu cha ngazi ya elimu (kidato cha nne).
sawa Mkuu, nmekuelewa vyema kabisa, hongera kwa ufafanuzi mzuri.
Lakini pia kama hiyo NQA ikianzishwa huoni kama kutakua na mlundikano wa Taasisi za kielimu, kwanini hilo jukumu la kuja kufanywa na hiyo NQA lisiwekwe kwa mfano huko TCU tu au NECTA tu?
 
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
52 (b) Kuhuisha taratibu za kujiunga na taasisi zinazotoa elimu na mafunzo katika ngazi mbalimbali kwa kutambua sifa zinazopatikana katika mifumo na taasisi tofauti ili kuhakikisha kwamba:-
(i) Asilimia 20 ya wahitimu wa Elimumsingi wanaendelea na masomo katika ngazi za Sekondari ya Juu na asilimia 80 kuendelea na elimu au mafunzo ya ufundi katika ngazi ya cheti, stashahada au shahada kulingana na sifa, vipaji au vipawa;
(ii) Asilimia 80 ya wahitimu wa Elimu ya Sekondari ya Juu kujiunga na Elimu ya Juu ya Taaluma na asilimia 20 kuendelea na Elimu ya Ufundi, katika ngazi ya cheti, stashahada au shahada kulingana na sifa; na
(iii) Asilimia 70 ya wahitimu wa Elimu au Mafunzo ya Ufundi na Taaluma wanapata ajira kwa kujiajiri au kuajiriwa.

(Ukurasa wa 92.)

===================================​

SERA YA ELIMU NA MAFUNZO 2014

Vile vile, taasisi kama vile Taasisi ya Elimu Tanzania, Baraza la Taifa la Mitihani Tanzania, Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi, Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania huratibu ithibati na uthibiti wa viwango vya ubora wa elimu na mafunzo katika ngazi mbalimbali. Kila taasisi ina bodi ya utendaji ambayo hutoa maamuzi kuhusu masuala ya utoaji na uendeshaji wa elimu na mafunzo katika maeneo ya mamlaka zao. Tathmini ilibaini kuwa taasisi hizi zinahitaji muunganiko fanisi wa utendaji kazi kisheria ili kuongeza ufanisi katika usimamizi wa ubora wa elimu na mafunzo nchini.

(Ukurasa wa 10).

===

3.2.22. Serikali itaweka na kusimamia mfumo wa kitaifa wa sifa linganifu wa tuzo kwa ngazi zote za elimu na mafunzo ili kurahisisha wahitimu kuweza kujiendeleza kielimu na mafunzo.

(Ukurasa wa 40. Tamko mojawapo la sera. Msisitizo ni wa asili)

=====

Baadhi ya nukuu za ILANI na Sera.​
 
sawa Mkuu, nmekuelewa vyema kabisa, hongera kwa ufafanuzi mzuri.
Lakini pia kama hiyo NQA ikianzishwa huoni kama kutakua na mlundikano wa Taasisi za kielimu, kwanini hilo jukumu la kuja kufanywa na hiyo NQA lisiwekwe kwa mfano huko TCU tu au NECTA tu?
Kila taasisi kwa sasa imekuwa kama "silo". NQA itakuwa ina "harmonize" njia mbalimbali za elimu. Jukumu hilo likiachiwa NECTA au TCU, itakuwa ni kuleta "Refa-mshambuliaji" mwingine. TCU na NECTA zote ni taasisi kwenye njia moja tu ya elimu. Ziko njia nyingine nne... zenye taasisi mbalimbali.
 
Mtoa mada ahsante kwa mada yako nyeti sana, nianze kusema awali nilihisi umechanganya sehemu ya ufundi mchundo na ya ufudni kuwa umefanya vice versa, lakini nahisi nmeelewa japo sijui kama iko sahihi sehemu ulizoziweka, ila umefafanua vyema kwa kila njia, nami niongezeee kidogo kwa uelewa wangu na nliyoyaona.
Nimeboresha. Ufundi Stadi (Vocational) na Ufundi (Technical) nilikuwa nimevichanganya. Asante kwa kubaini.
 
Kila taasisi kwa sasa imekuwa kama "silo". NQA itakuwa ina "harmonize" njia mbalimbali za elimu. Jukumu hilo likiachiwa NECTA au TCU, itakuwa ni kuleta "Refa-mshambuliaji" mwingine. TCU na NECTA zote ni taasisi kwenye njia moja tu ya elimu. Ziko njia nyingine nne... zenye taasisi mbalimbali.
kaka nmekuelewa vyema kbs, nazidi kukupongeza juuu ya hili. nmeelewa kuhusu NQA pia. lakini nasisitiza kama walivyoonyesha hapo kwenye ilani kuna haja ya baadhi ya Taasisi aidha kuunganishwa kuwa moja au baadhi ya majukumu yahamie kwingine, mfano VETA na NACTE kuna majukumu wanafanana na kuna mmoja anafanya zaidi nafkiri aidha ziunganishwe ziwe taasisi moja au baadhi ya majukumu yatoke VETA yaende NACTE ili kupunguza urasimu katika shughuli za VETA na kuongeza ufanisi zaidi!!
 
Asante bro. Ilipata kusikika miaka kidogo iliyopita, palikuwa na mpango wa kuunganisha TCU, NACTE, VETA n.k., ili kupunguza utitiri wa taasisi. Sina hakika mipango hiyo kama ipo kweli. Kadhalika, sina hakika na kemia iliyoko baina ya taasisi hizo. Pengine an umbrella organization, particularly with respect to harmonizing their awards inawezekana kuwa ya muhimu.

Kuhusu TzQA, pana dokumento moja ya UNESCO, inasema:

The institutional set-up for the TzQF is not yet complete. In line with international best practice, Tanzania intends to establish a national qualifications authority, the TzQA, which will create and maintain an electronic register for all TzQF qualifications and providers. Establishment of the TzQA will be enacted by Parliament. The TzQA Act will, among other things, stipulate the responsibilities of existing bodies such as the National Examinations Council of Tanzania (NECTA), the Vocational Education and Training Authority (VETA), NACTE, the TCU and professional bodies with respect to the TzQF

(ukurasa wa pili, https://uil.unesco.org/fileadmin/keydocuments/LifelongLearning/en/Tanzania.pdf )

Nyatunyatu zinaashiria ukinzani mkubwa dhidi ya mfumo huu wa kulinganisha elimu.
 
Nafkiri bado tuna safari ndefu kama hatutochukua hatua za ziada juu ya hili, na nna wazo flan hivi nlkua najadili na wadau, ngoja nkitulia nliweke vzr tujadili hapa
 
Wakati huohuo, kwa kila mtu asemalo, aambiwa, "nionyeshe cheti cha ufaulu kidato cha nne", mithili ya kinachojiri kwenye matangazo ya "Show me the Carfox". Jambo hili ni la kubadilishwa.
 
Back
Top Bottom