Kulingana umri kwa wapenzi/wachumba kuna athari gani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kulingana umri kwa wapenzi/wachumba kuna athari gani?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Seif al Islam, Sep 10, 2012.

 1. S

  Seif al Islam JF-Expert Member

  #1
  Sep 10, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 2,158
  Likes Received: 141
  Trophy Points: 160
  Jamani hebu tuwekane sawa katka hili.kuna watu wengi sana wanadai eti haifai na haishauriwi kwa wachumba/mke na mume kulingana umri.kuna sababu nyingi wanazotoa eti ooh mke atazeeka mapema(wakati kuna matunzo) na nyingine nyingi .naombeni sana wanajamvi wenzangu mnisaidie mm na wengine wanaotatizwa na kelele hizi ili tujue ukweli.
   
 2. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #2
  Sep 10, 2012
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Nimeshuhudia kijana wa miaka 30 alimuoa dada wa miaka 38 na maisha ni mazuri. Kwa Tanzania hatujazoea ila siku hizii naona inajitokeza mara chache na mwisho itazoeleka!!! Mbona wengine wako na mijimama unakuta 30s anakimbizana na mama wa miaka 40s hata na 50s!!!!??? Kwa upande wangu angalao msizidiane over 5 years kwa pande zote mbili.
   
 3. MATESLAA

  MATESLAA JF-Expert Member

  #3
  Sep 10, 2012
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 1,252
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mapenzi hayachagui umri
   
 4. SnowBall

  SnowBall JF-Expert Member

  #4
  Sep 10, 2012
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 3,067
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Hata kuwe na tofauti gani ya miaka..kama ni kuzeeka mtazeeka tu..
  Tii kiu yako...
   
 5. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #5
  Sep 10, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Hakuna tatizo we kama unataka kuoa, oa tu!
   
 6. Dr. Wansegamila

  Dr. Wansegamila JF-Expert Member

  #6
  Sep 10, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 1,233
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  Kwangu mimi kulingana umri haina shida....... What matters ni kupendana na kuheshimiana.
   
 7. V

  Von Mo JF-Expert Member

  #7
  Sep 11, 2012
  Joined: May 7, 2012
  Messages: 1,830
  Likes Received: 765
  Trophy Points: 280
  Ni kweli siyo sahihi, kwa sababu imethibitishwa akili/mawazo ya mwanamke na mwanaume yanatofautiana kutokana na nyumri, FANYA KUFUATILIA UTAGUNDUA WANAUME WANATULIA WAKIFIKA AT LEAST 30s wanataka kuoa, wakati watoto wa kike wao wanatulia kuanzia 24-27,pale unakuta wanataka kuolewa tu, unaweza ukaona mwanamke anapaswa kutofautiana umri na mumewe..at least 3years na kuendelea...nasema hivyo kwa sababu nimeshuhudia ndoa ya mwanaume wa 33yrs na mwanamke 21yrs and they were happy and you can't detect their age differences
   
 8. p

  pilau JF-Expert Member

  #8
  Sep 11, 2012
  Joined: Aug 16, 2012
  Messages: 1,523
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Kama ni mwanaume Usidangabyike tena usithubutu kuoa mwanamke ambaye mnalingana umri akifika miaka 50 na wewe mume 50 hapo mwanamke ataonekana mama yako mdogo, na kwa hali yoyote lazima utamkimbia hamtaongozana kwenye functions mbali mbali, angalau kwa waswahili sisi unapaswa mume kumzidi mke miaka 7 na kuendelea, mfano mdogo angalia wanawake wenye miaka 50 wanafananaje na wanaume wamiaka 50 wanafananje kisha utaamua

   
 9. DSpecial

  DSpecial JF-Expert Member

  #9
  Sep 11, 2012
  Joined: Dec 18, 2011
  Messages: 457
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Haya ndio mapenzi bwana.....hii kitu inayoitwa kupenda hii acheni tu jamani, ila cha muhimu ni kupendana tu kwa dhati wazee
   
 10. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #10
  Sep 11, 2012
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,927
  Likes Received: 2,079
  Trophy Points: 280
  Hawa katika hii picha wote wana miaka 85!

  [​IMG]
   
 11. lara 1

  lara 1 JF-Expert Member

  #11
  Sep 12, 2012
  Joined: Jun 10, 2012
  Messages: 15,444
  Likes Received: 10,122
  Trophy Points: 280
  Umri ishu kubwa ni heshima na upeo. Wanawake wanakuwa kiakili haraka kuliko wanaume, ndo maana binti wa 18yrs unaweza kumuozesha na akazaa na kumudu familia kama jembe la 30yrs bt mvulana 18yrs ukimuozesha itakuwa mshikemshike humo ndani.

  Hivo unakuta mkioana wote 25 to 25 wewe mwanaume ukiwa 25 upeo wako utakuwa kununua flashy cars, kunywa kidogo na wadau jioni, kupendeza na pamba na shoes za bei mbaya, hivi ndo vitu utaenjoy kuvifanya ila msichana yeye 25 atataka mzae mtoto, majukumu yatazidi, mjenge nyumba msipange, atadai shule nzuri ya mtoto, sasa utagundua mvulana ataanza kuona binti anmcontrol, anamnyima uhuru, anataka life la juu huku uwezo hma. Binti nae ataanza kuona mwanaume mzigo, hawajibiki vya kutosha na kuanza kuhisi maybe she made a wrong move!!! Atakuwa kila siku kumcompare mumewe na waume za mashosti zake. Basi ndo misuguano inaanza.

  Ila kukiwa na gap ya age Man in his 35 binti 25 hapo swadaktaa. Man anakuwa kajijenga, yupo stable kiuchumi, amebakiza kuzaa na kuijaza dunia! Binti nae hana pressure katuliaaa full kudeka kwa mmewe.
   
 12. V

  Von Mo JF-Expert Member

  #12
  Sep 12, 2012
  Joined: May 7, 2012
  Messages: 1,830
  Likes Received: 765
  Trophy Points: 280
   
 13. bombafresh

  bombafresh Senior Member

  #13
  Dec 24, 2013
  Joined: Feb 15, 2012
  Messages: 162
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  To the point !!
   
 14. R

  Ringtone JF-Expert Member

  #14
  Dec 24, 2013
  Joined: Nov 21, 2013
  Messages: 490
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tofauti ya umri si tatizo kwa wachumba kabisa.
  Zamani kazi nyingi ngumu zilifanywa na mwanamke.kulima,kukata kuni,mwendo mrefu kuchota maji,uzao wa watoto wengi bila lishe bora.kiukweli walikuwa wanazeeka kabla ya sis wanaume.
  Kwa sasa maisha yamerahisishwa sana na huduma za kijamii,technologia na zaidi wanawake kuwa sehemu muhimu ya labour force ktk ajira nyingi rasmi. Hivyo umri kuwa sawa au mwanamke kumzidi mwanaume sitatizo. I wish kama ningeoa aliyenizidi umri ingependeza zaidi.reason behind,wanawake wana mawazo ya kujenga as age goes on.
   
 15. Z

  Z Nyenza Member

  #15
  Dec 24, 2013
  Joined: Sep 22, 2013
  Messages: 77
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 15
  kwa hiyo picha tiyari mwanamke anaonekana mzee sana kuliko mwanaume japo wote ni wazee angalia vizuri hiyo picha
   
 16. kibella24

  kibella24 JF-Expert Member

  #16
  Dec 24, 2013
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 677
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kuoa mwanamke unayelingana naye umri si tatizo especially km wote mko matured kiasi chakuweza kuoana nakuishi pamoja. Ila kuoa mwanamke uliyemzidi umri ni jambo jema zaidi. Japo kila mtu ana maoni yake ila washauri wengi wa mambo ya ndoa (marriage counselors) wanasema difference ya miaka walau iwe 3yrs.
   
Loading...