Kulingana na sheria ya ndoa kesi ya Dr. Slaa kupora mke imepitwa na wakati!

Kwako Kanda2

Soma kifungu cha 65(c) cha sheria ya ndoa na tafakari hoja nilizozitoa. Ukifanya hayo mawili ninaamini utazifuta kauli zako hizi kuwa hazina mantiki na ninazinukuu:-

My 50cent

Slaa anadai alikuwa "hajui" kuwa Josephine ni mke wa mtu, granted! sasa kishajua na vithibitisho vime tolewa vikiwemo hati za ndoa nk. Lakini kwa jeuri na anaendelea kumtangaza kuwa ni mchumba kwa maana nyingine anavunja sheria huku sasa akijua kuwa anavunja sheria.

Huyu ndie anaepigiwa debe hapa aje kuwa "command in chief" kwa jeuri aliyo tukuka anavunja sheria mchana kweupe. Watanzani tuna elekea wapi?
 
My 50cent

Slaa anadai alikuwa "hajui" kuwa Josephine ni mke wa mtu, granted! sasa kishajua na vithibitisho vime tolewa vikiwemo hati za ndoa nk. Lakini kwa jeuri na anaendelea kumtangaza kuwa ni mchumba kwa maana nyingine anavunja sheria huku sasa akijua kuwa anavunja sheria.

Huyu ndie anaepigiwa debe hapa aje kuwa "command in chief" kwa jeuri aliyo tukuka anavunja sheria mchana kweupe. Watanzani tuna elekea wapi?

Ni vyema tukaelewana kuwa mahakama "zinatoa haki kwa mujibu wa sheria na si kwa mujibu wa uhalisia wa tukio". hapa namaanisha kuwa kama sheria inakataza jambo, jambo hilo linakuwa ni kosa kwa mujibu wa sheria hiyo, lakini kama sheria haijakataza jambo husika jambo hilo linakuwa si kosa (hata kama utamaduni au mazoea ya jamii husika suala hilo linaonekana ni baya au dhambi)

Hivyo ni vyema tukaelewa tuwapo katika kesi mahakamani mbele ya hakimu ni tofauti uwapo kwenye kesi mbele ya Sheikh, Padri au mchungaji. uwapo mahakamani uanatoa majibu kwa kuzingatia masuala ya kisheria na uwapo mbele ya Sheikh, Padri au mchungaji unatoa majibu kuzingatia ukweli mbele ya MUNGU.
Hivyo mahakamani hatutoi majibu eti kujionyesha sisi ni wakweli au wastaarabu au ni viongozi bora bali tuna toa majibu kulingana matakwa ya sheria na kesi inayokukabili. Hivyo majibu ya SLAA mahakamani yanazingatia mambo hayo. Na yatupasa tukumbuke kuwa kwa mujibu wa sheria zetu mzigo wa kuthibitisha kosa kufanyika (burden of proof) upo kwa mlalamikaji na si mlalamikiwa, hivyo BWANA MAHIMBO ndio anapaswa kuithibitishia mahakama bila kuwepo na shaka yoyote kuwa mlalamikiwa SLAA ametenda kosa la kumpora mke, na ni matendo au mambo gani yaliyofanywa na DKT SLAA yanathibitisha kuwa katenda kosa hilo. Na uthibitisho wote huo autoe kwa kuzingatia sheria na si kwa maneno ya mitaani ukumbuke kuwa mgogoro huu au kesi hii ni ya ndoa hivyo sheria ya ndoa lazima hiusike kwa asilimia kubwa ikijumuisha na sheria nyingine mf. sheria ya madai nk. Na swala la kwanza linalohitajika kuthibitishwa ni kuwa je kuna ndoa kati ya Bw. MAHIMBO na Bi. JOSEPHINE. naomba nikumbushe kuwa swali hilo litahitaji kupata jibu la kisheria na si la kidini, yaani kwa mujibu wa sheria ya ndoa kuna ndoa kati ya mahimbo na josephine.Kwa kifupi RUTASHUBANYUMA katika POST yake amebainisha utata wa uwepo wa ndoa ya wawili hao. Ni vyema tukasubiri mahakama itoe maamuzi yake kuhusina na kesi hiyo.
Kuhusu kwa nini anamnadi JOSEPHINE majukwaani , Jiulize mwenyewe kwa mujibu wa sheria kama RUTASHUBANYUMA alivyotuwekea kwenye POST yake hapo juu, je JOSEPHINE na MAHIMBO ni mtu na mkewe? Je MAHIMBO kuwekwa kinyumba na mama kiongozi wa CCM kunafanya ndoa yake iendelee kuwa ndoa kwa mujibu wa sheria ya ndoa (kama ndoa hiyo hipo). TAFAKARI KISHA ....................................
 
Wednesday, 06 October 2010 08:13
James Magai

MLALAMIKAJI katika kesi inayomkabili katibu mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa sasa atalazimika kujenga hoja kukabili utetezi uliowasilishwa na mgombea huyo wa urais ambaye amedai kuwa hakufahamu kwamba mwanamke aliyemtangaza kuwa ni mchumba wake, alikuwa mke wa mtu.

Mlalamikaji huyo, Aminiel Mahimbo, ambaye amefungua kesi ya madai namba 122/2010, anataka alipwe fidia ya Sh1 bilioni akidai kuwa kitendo cha Dk Slaa kumtambulisha mkewe, Josephine Mushmbuzi kuwa ni mchumba wake, kilimdhalilisha.

Lakini sasa, Mahimbo na wakili wake watakuwa na siku saba za kuandaa hoja dhidi ya utetezi wa upande wa walalamikiwa na kuziwasilisha mahakamani, kama utaratibu wa kesi za madai unavyotaka.
Jaji anayesikiliza kesi hiyo, Zainabu Muruke alitoa muda huo wa siku saba baada ya wakili wa mlalamikaji, Abduel Kitururu kuomba muda wa kujibu hoja za utetezi wa mlalamikiwa.

Upande wa utetezi, ambao unawakilishwa na kampuni ya uwakili ya Marando & Mnyele Advocates ulisema hauna pingamizi na ombi hilo na Jaji Muruke alimtaka mlalamikaji kuwasilisha majibu ya hoja hizo za utetezi wa mlalamikiwa ifikapo Oktoba 12.

Pia mahahakama hiyo imepanga Oktoba 15 pande zote katika kesi hiyo kukutana pamoja kwa lengo la kuandaa na kupanga lini na namna ya kuendesha kesi hiyo.

Katika maelezo ya utetezi wake wa maandishi aliyoyawasilisha mahakamani Septemba 29, Wakili Mabere Marando alisema kuwa Dk Slaa alikiri kuwa na uhusiano na Josephene lakini akajitetea kuwa hakujua kuwa mwanamke huyo ni mke wa mtu kwa kuwa hakumwambia kuwa ameolewa.

Alidai kuwa alisikia kwa mara ya kwanza habari za ndoa baina ya mlalamikaji na mwanamke huyo aliposoma habari hizo kwenye vyombo vya habari na hivyo kumtupia mzigo mlalamikaji athibitishe kuwa mteja wake alikuwa akijua kuwa mwanamke huyo ameolewa.

Dk Slaa pia amekana madai ya kufanya uzinzi na Josephine wala kumtangaza kama mke wake na hivyo anamtaka mlalamikaji atoe ushahidi wa madai hayo.

Kuhusu madai ya kumdhalilisha, kumshushia hadhi na kumsababishia usumbufu mlalamikaji, Dk Slaa pia ameyakana na kudai kuwa mlalamikaji mwenyewe ndiye aliyejisababishia hayo kwa kukubali kutoa taarifa hizo kwenye vyombo vya habari.

Kama vile haitoshai Dk Slaa amemtuhumu mlalamikaji huyo kulipwa na chama cha siasa kuruhusu habari zake hizo ziandikwe kwenye vyombo vya habari kwa malengo ya kisiasa
Dk Slaa anadai kuwa kwa kitendo cha mlalamikaji huyo kuruhusu habari hizo zitangazwe na vyombo vya habari kimemfanya apoteze heshima yake na hivyo hata madai yake hayana msingi na hayana budi yatupiliwe mbali.

Mahimbo alifungua mashtaka hayo Septemba 7 mwaka huu akitaka alipwe fidia ya Sh1 bilioni kwa madai kuwa mwanasiasa huyo ameingilia ndoa yake na kufanya uzinzi na mke wake huyo.


Source: Mwananchi





MY TAKE:

kwa kuwa suala hili limeletwa ('kisiasa?') kipindi hiki cha uchaguzi mkuu, nimeona bora niweke kwenye jukwaa hili. aidha, kwa kuwa suala lenyewe bado liko mahakamani, napendelea zaidi kuliwasilisha kwenu kama habari ila discussion yoyote ni at your risk.
 
Hii kwa mtazamo wangu ni kesi ya msimu - uchaguzi ukipita na hii kesi imepita (none event)
 
Nasikia ccm wanataka kuliingiza swala hilo kwenye ahadi zao , kuwa wakipata urais swala hilo litakua kwenye agenda zao ili kulipatia ufumbuzi wakudumu.
 
Ndugu yangu Lutanyuma sheria isitafusiriwe kisiasa. Sheria ya Ndoa haikutungwa maalumu kwa tukio la DR SLAA au mtu mwingine yoyote maalumu. Sifa ya sheria ni kwamba inawahusu watu wote wa wakati uliopo na ujao mpaka itakapofutwa.

Umezungumzia juu ya dhana ya kuwepo na kutokuwepo kwa ndoa. Katika lugha yenu ya wanasheria dhana juu ya uwepo au kutokuwepo kwa ukweli fulani wa mambo inaweza kuwa isiyokanushika (irrebutable) na inayopingika (reputable). Tunaposema dhana inakanukisha inaana ya kwamba isipokuwa tu kama kuna ushahidi unaoashilia vinginevyo, mtu akikaa bila mwanandoa mwenzie kwa mda wa miaka miwili anachukuliwa kama walishaachana. Dhana hii inapingika kwa mwanandoa mwenzie kujitokeza na kuonesha vyeti vya ndoa na kuthibitisha kwamba hajawahi kumuacha katika taratibu zozote zinazokubalika.


Kwa ufahamu wangu ndoa kati ya Josephine na mwenzake ambayo ilikuwa ya maisha na ya mke mmoja bado ipo kisheria na haiwezi kuhesabika kutokuwepo mpaka mahakama itamke kwamba imevunjika au mmoja kati yao aage dunia. Hilo sidhani kama ni moja ya mambo yanayobishaniwa. Utetezi wa msingi wa mheshimiwa DR SLAA ni kwamba hakuwa anajua kwamba JOSEPHINE ni mke wa mtu na si kwamba JOSEPHINE si mke wa mtu kwa mjibu wa sheria zetu. Ebu jaribu kutafakari vizuri bila muelekeo wa kisiasa.
 
Kweli hii kesi ni ya msimu. Slaa ana muda mrefu na Josephine kama sikosei tangu 2007. Sasa leo hii 2010 ndiyo inaibuliwa. Kama ni kosa linaonekana leo baada ya miaka 4? siasa ni ukichaa.
 
Hilo ndugu yangu lina ukweli fulani. Kwamba pengine DR SLAA asingegombea URAISI au asingekuwa na ushawishi mkubwa katika uchaguzi kesi hii isingefunguliwa. Lakini hilo peke yake halifanyi kesi kutosimama. Kwani mtu mwenye haki yake kisheria akiamua asiende mahakamani kwa sababu yoyote haimaanishi kwamba amenyan'ganywa haki yake ya kushitaki. Anaweza kupoteza haki yake kama ukomo wa muda wa kufungua kesi kisheria umekwisha
 
Huyu Slaa si Daktari wa Kanoni? Sasa wenye kujuwa sheria za kanoni watueleze aliyoyafanya / anayoyafanya yanakubalika na shria za kanoni? au sheria za ukatoliki?
 
Katika pita pita kwenye mtandao, nimekutana na hii:

[FONT=trebuchet ms,arial,helvetica]Variety of Bible-based beliefs:

We are faced with a dilemma:
[/FONT]
topbul1d.gif
[FONT=trebuchet ms,arial,helvetica]Various Christian groups -- conservative Protestants, liberal Protestants and Roman Catholics have reached different beliefs about when, if ever, the Bible permits divorce and remarriage. [/FONT]
topbul1d.gif
[FONT=trebuchet ms,arial,helvetica]Each of the authors and webmasters who has written on these topics appear to believe that their belief alone is the correct interpretation of the Bible. [/FONT] [FONT=trebuchet ms,arial,helvetica] The main positions are:

  1. Neither divorce nor remarriage are allowed. (Conservative Protestant view)
  2. Divorce is OK, but not remarriage. (Ditto)
  3. Divorce is OK in cases of adultery or desertion; remarriage is OK. (Ditto)
  4. Divorce is OK for many reasons; remarriage is OK. (Ditto)
  5. Divorce is impossible unless the marriage can be proven to have never existed -- described below. (Roman Catholic)
  6. Divorce is OK in cases of marriage breakdown; remarriage is OK. Religious liberal and secular view.
This essay describes the fifth position: the Roman Catholic believes that the Bible does not allow divorce on any grounds. Valid marriages are indissoluble. However, if it can be proven that a valid marriage had never taken place, then an annulment is obtained. Remarriage is often allowed after an annulment.
topruled.gif
Overview:

The position of the Roman Catholic church on divorce and remarriage can be summed up in a few sentences:​
[/FONT]
topbul1d.gif
[FONT=trebuchet ms,arial,helvetica] [/FONT]
[FONT=trebuchet ms,arial,helvetica]Divorce was allowed in Hebrew Scriptures (Old Testament) times. But the permanence of marriage was restored by Jesus in the first century CE.[/FONT]​
topbul1d.gif
[FONT=trebuchet ms,arial,helvetica] [/FONT]
[FONT=trebuchet ms,arial,helvetica]Marriage is a sacrament that is indissoluble. Once a valid marriage has been consummated, It endures until one spouse dies.[/FONT]​
topbul1d.gif
[FONT=trebuchet ms,arial,helvetica] [/FONT]
[FONT=trebuchet ms,arial,helvetica]The church does not issue divorces or recognize divorces issued by other institutions.[/FONT]​
topbul1d.gif
[FONT=trebuchet ms,arial,helvetica] [/FONT]
[FONT=trebuchet ms,arial,helvetica]The church can issue an annulment. However, the couple must first prove to a church tribunal that the marriage was invalid.[/FONT]


[FONT=trebuchet ms,arial,helvetica]source: Divorce, remarriage and annulment within the Roman Catholic Church
[/FONT]​
 
Kweli hii kesi ni ya msimu. Slaa ana muda mrefu na Josephine kama sikosei tangu 2007. Sasa leo hii 2010 ndiyo inaibuliwa. Kama ni kosa linaonekana leo baada ya miaka 4? siasa ni ukichaa.

Kweli siasa ni kichaa. Lakini tukumbuke hawa viongozi wa siasa wanatakiwa wawe na maadili mema ili wawe viongozi wema, sasa huyu Slaa anapingana hata na dini yake, kweli atafaa kutuongoza wa Tanzania? Kupingana na CCM ni haki yake msingi lakini kupingana na dini yake? sijui hii imekaaje kwako?
 
Hivi dr. Slaa amekosa mwanamke wa kumnadi ktk mikutano yake mpaka amtumie huyu mwanamke controvercial aliyemtoroka mumewe?? Mimi naona kakurupuka kuchomoa mke bomu ili aonekane mgombea urais nayeye ana mke!, sasa bahati mbaya huyu ni mke wa mtu!
Namshauri slaa kwanza amrudishe josephine mushumbushi kwa mwenyewe, halafu alipe fidia hata kama sio bilioni 1 ili kuonyesha kitendo alichikifanya ni kichafu lakini alidanganywa hivyo atakuwa ameonyesha utu na kwa kuwa yeye ni padri anajuwa maadili!!

Tunakuomba rais wetu mtarajiwa kabla hujaingia ikulu ambayo ni takatifu achana na huyu changudoa na tafuta mke mwingine kwa haraka ili siku ukiapishwa uwe na mkeo pembeni lakini wa halali sio wa kuokoteza barabarani!!!!

Kweli mnafiki hana soni. Dr. Slaa anaweza kuwa Rais wako mtarajiwa wewe mnafiki? Waambie waliokutuma haina mshiko hiyo
 
Kweli siasa ni kichaa. Lakini tukumbuke hawa viongozi wa siasa wanatakiwa wawe na maadili mema ili wawe viongozi wema, sasa huyu Slaa anapingana hata na dini yake, kweli atafaa kutuongoza wa Tanzania? Kupingana na CCM ni haki yake msingi lakini kupingana na dini yake? sijui hii imekaaje kwako?

Wewe unaijua dini yake kuliko Pope? Imeishia wapi sasa?
 
Back
Top Bottom