Kulingana na sheria ya ndoa kesi ya Dr. Slaa kupora mke imepitwa na wakati! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kulingana na sheria ya ndoa kesi ya Dr. Slaa kupora mke imepitwa na wakati!

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Rutashubanyuma, Oct 2, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Oct 2, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,787
  Trophy Points: 280

  Sheria ya ndoa ipo wazi watu wawili wanapoishi pamoja kama mke na mume watahesabika kuwa ni wanandoa kama hakuna anayebisha yaani (rebuttable evidence). Vile vile wanandoa wanapokuwa wametengana kwa kipindi kinachozidi miaka miwili au zaidi watahesabika kwa sheria hiyohiyo si wanandoa hii ni kwa sababu sheria ni msumeno na inakata pande zote mbili.

  Mdai ambaye ni mume wa Josephine anakiri mahakamani ya kuwa yeye na Josephine hawakuwa wanaishi kama wanandoa kwa zaidi ya miaka mitatu jambo ambalo hata mkewe wake wa zamani anakiri.

  Hivyo kuna “rebuttable evidence” baada ya miaka miwili ndoa hiyo ilikuwa imekufa yaani “irreparably broken” na wanandoa hao wa zamani walikuwa wamtengana kwa matendo yao ya hiari yao. Ikumbukwe ndoa msingi wake mkuu ni hiari na hakuna mahakama yoyote duniani yenye mamlaka ya kuwalazimisha watu ambao hawako tayari kuishi pamoja kama mke na mume kuishi hivyo. Hivyo ni umbumbumbu wa sheria kukimbilia mahakamani kwenda kudai ulidhalilishwa na mtaliki wako baada ya zaidi ya mwaka mmoja wa kisheria kwa sababu huyu sasa siyo tena mke wako. Mlalamikaji alipaswa kulalamika ndani ya miaka miwili ya kisheria baada ya kutengana na mkewe badala ya kusubiri miaka mitatu kupita na aliposikia mtaliki wake sasa amepata mtu mwenye uwezo wa kifedha kukimbilia mahakamani kudai fidia ya Tshs bilioni moja wakati yule sasa siyo mke wake bali ni mtaliki hata kama hakuna aliyeenda mahakamani kudai talaka.

  Hili Mlalamikaji hana ubishi nalo na ndiyo maana amejisweka kwenye nyumba ya mwanamama mmoja wa CCM ambaye anaishi naye kama mume na mke. Mwanamama huyo hivi sasa anagombea jimbo moja hapo Dar kwa tiketi ya CCM.

  Ni dhahiri Mlalamikaji alielewa ya kuwa ile ndoa ya mume mmoja kwa mke mmoja “until death does us apart” was all water under the bridge na ndiyo maana ameamua kuwekwa kimada na kigogo mmoja ndani ya chama cha mafisadi na ambacho ni maarufu kwa kujiita ni CCM.

  Sasa hizi purukushani za kutumiwa na mafisadi eti kwa sababu ya ujira mdogo atakao ulamba yanatoka wapi kama siyo kuidhalilisha mahakama na kujishushia yeye mwenyewe heshima ya kiutu uzima mbele ya jamii. Baada ya uchaguzi kupita, CCM kama kawaida yao watamtelekeza huyu ***** na wala hawatataka kuhusishwa naye tena. Si mnawajua CCM na sera yao ya “use and dump”? Si sera hii ndiyo imetuleta laana hiyo ya umasikini wa kutupwa? CCM ni magwiji wa kutulamba miguu kabla ya uchaguzi lakini wakisha pata baraka zetu huwa hatuwaoni hadi uchguzi wmwingine ndiyo hutukumbuka kwa fulana, kofia, kanga na wakati mwingine ubwabwa na nyamapori za kutokoswa.

  Mahakama Kuu inapaswa kutupilia mbali upuuzi huu ili iendelee kushughulikia maswala yenye tija kwa jamii
   
 2. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #2
  Oct 2, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Nawaomba wakuu tusifanye makosa kama yaliyofanyika kwenye kesi ya ZOMBE. tusiishadidie hii kesi maana is not our priority now na kama tujuavyo imefunguliwa kama kikwazo kwa mgombea wetu urais ionekane kwamba ana ishu ya kumtoa kwenye mbio za uchaguzi.

  Tuiache mahakama na mawakili wawekane sawa na kumaliza hii ishu kisheria zaidi. Hofu yangu ni kwamba mahakimu/ majaji wengi wanajiweka ktk position ya kiminya haki kwa sababu ndogo ndogo.

  Let us stick on pilicies and edecating our people to be part of the forthcoming change
   
 3. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #3
  Oct 3, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,787
  Trophy Points: 280
  Kwako Drphone

  Ninashukuru kwa udadisi wako. Sote ni wanafunzi lakini hukumu zifuatazo zitakuonyesha ya kuwa yule mama hata kama ameivunja hiyo ndoa bado anastahili mgawo stahili kulingana na mchango wake kwenye ndoa hiyo hadi pale alipojitoa.

  Mmoja wa wanandoa kujitoa hakumzui kufaidika na jasho lake kama lipo na haya ndiyo maelekezo ya mahakama ya rufaa na ya Mahakama Kuu kwenye kesi zifuatazo:-

  a) Roberto Aranjo v. Zena Mwijuma 1986 TLR 207 (CA):-

  b) Omari Chikamba v. Fatuma Mohamed malunga 1989 TLR 39 (HC):-

   
 4. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #4
  Oct 3, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,787
  Trophy Points: 280
  Kwako msanii.

  Kwanza ninashukuru sana kwa mchango wako.

  Kinachokatazwa na mahakama zetu ni kuujadili ushahidi uliopo mahamakamani yaani
  lakini utaratibu au
  kama ilitumika au kwanini haijatumika au utaratibu utakaotumika huo ni uwanja wetu wa mjadala haswaaaaaaaaa.

  Bahati nzuri haya niliyoyaongea hakuna upande ulioyaibua hadi hivi sasa hapo mahakamani na vyombo vyetu vya habari vimekuwa vikipotosha raia na ndiyo maana niliona kuna uhaja wa kutoa elimu ya uraia kwa bei poa ya msomaji kufungua makala hiyo.

  Mahakama zina kazi ya kufanya lakini nasi pia tuna jukumu la kutafakari yanayofanwa na mahakama zetu kama yatija kwa taifa hili.

   
 5. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #5
  Oct 3, 2010
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
 6. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #6
  Oct 3, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,787
  Trophy Points: 280
  Eeka Mangi

  Ni vyema ukaibua hoja tukaitafakari kwa sababu sheria hiyo ina mambo mengi sana.
   
 7. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #7
  Oct 3, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Kuna haja ya kuipitia hii sheria waweza kuwa muhanga ivi ivi
   
 8. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #8
  Oct 3, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,787
  Trophy Points: 280
  Kifungu hiki cha sheria kinafanya madai ya bilioni moja kuwa ni ndoto za alinacha na nina kinukuu:-


  Soma kifungu cha (C) kwa uangalifu utaona hakuna fidia kwa matendo yoyote ya kuvunjika kwa ndoa au kutotimiza wajibu ndani ya ndoa.

  Hivyo madai ya Tshs bilioni moja mahakama ni lazima itayatupa kwa sababu yanakatazwa na sheria.

  Madai haya yamewekwa pale ili kuonyesha picha ya kisiasa ya kuwa Dr. Slaa kuna kosa kubwa maelitenda wakati hakuna kosa lolote. Mlalamikaji sana sana apaswa kudai talaka yake mahakamani na hakuna fidia zaidi ya hiyo....

  Baada ya uchaguzi ccm wataingia mitini maana haitakuwa ni mtaji wa kisiasa tena
   
 9. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #9
  Oct 3, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,787
  Trophy Points: 280
  Sheria hii ya ndoa na ninainukuu inakataza kabisa Dr. Slaa au mama Josephine au hata yule Mlalamikaji kudaiwa chochote juu ya sakata la kuporwa mke ambalo CCM haswa kupitia magazeti ya uhuru na Habari Leo wanaona ni mtaji wa kisiasa.

  CCM sana sana wanachoonyesha ni kufilisika kisiasa na kiakili kuendelea na hii kazi ya kutwanga maji kwenye kinu...........Hata hivyo CCM ni chama cha vihiyo na mafisadi tulitegemea nini?

  Soma kwa makini kifungu cha 60 (c) hapo juu ndicho kinamaliza upuuzi huo ulioko mahakamani
   
 10. Lyangalo

  Lyangalo JF-Expert Member

  #10
  Oct 3, 2010
  Joined: Sep 10, 2009
  Messages: 681
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Hivi kweli mwanamke aliyekuwa ambae una sema ni mkeo hujakaa nae kwa miaka mitatu si kwamba amekwenda kusoma aaa yupo Tanzania na anadunda kivyake inawezekana kweli kusema ni mkeo? huyo jamaa hana cha kulalamika ila kwa mpuuzi inawezekana.
   
 11. t

  tanza New Member

  #11
  Oct 3, 2010
  Joined: Oct 3, 2010
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi dr. Slaa amekosa mwanamke wa kumnadi ktk mikutano yake mpaka amtumie huyu mwanamke controvercial aliyemtoroka mumewe?? Mimi naona kakurupuka kuchomoa mke bomu ili aonekane mgombea urais nayeye ana mke!, sasa bahati mbaya huyu ni mke wa mtu!
  Namshauri slaa kwanza amrudishe josephine mushumbushi kwa mwenyewe, halafu alipe fidia hata kama sio bilioni 1 ili kuonyesha kitendo alichikifanya ni kichafu lakini alidanganywa hivyo atakuwa ameonyesha utu na kwa kuwa yeye ni padri anajuwa maadili!!

  Tunakuomba rais wetu mtarajiwa kabla hujaingia ikulu ambayo ni takatifu achana na huyu changudoa na tafuta mke mwingine kwa haraka ili siku ukiapishwa uwe na mkeo pembeni lakini wa halali sio wa kuokoteza barabarani!!!!
   
 12. K

  Kadogoo JF-Expert Member

  #12
  Oct 4, 2010
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,072
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  kama huna hoja si unyamaze? Nani kakulazimisha kuongea? Yaani nilazima tu muandike hata kama ni pumba!!!! Mwenzako anazungumzia usiku we umebaki mchana!!!
   
 13. WA MAMNDENII

  WA MAMNDENII JF-Expert Member

  #13
  Oct 4, 2010
  Joined: Jun 5, 2010
  Messages: 310
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  we tanza hujakaribishwa unaanza kuchonga , kaa kwanza kitako ufikiri kwa kina hili sio jukwaa la kuingia na kuja na hoja zako kwa pupa
   
 14. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #14
  Oct 4, 2010
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Unajua hawa Habari na wote wanaotaka kutumia hii issue ya Dr Slaa kama mtaji wameshindwa. Kinachoendelea sasa ni kujaribu kukumbushia kwa kuandika habari hizi ambazo watanzania wamezikataa kwani haziwaondolei umasikini wao wala kuwapatia ajira. Uzuri ni kuwa watanzania wanafahamu wazi kuwa watu wanaoongoza kwa ufuska ni viongozi wa juu wa CCM, na serikali. Unapoleta suala la Dr Slaa kama standard ya kiongozi inakuwa haileti maana kwani wote tunajua kuwa hakuna watu wachafuzi wa wanawake kama viongozi wa chama na serikali waliopo madarakani kwa sasa. Hawa wote mambo yao tunayajua wazi hivyo suala la Dr Slaa is nothing mbele ya hawa mafuska.

  Ninampongeza sana Dr Slaa kwa kukataa politics of distraction and stay on the issues which matter most to Tanzanians.
   
 15. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #15
  Oct 4, 2010
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  ngoja nikupe mifano ya viongozi wazuri na ndoa zao
  1. Mfalme daudi aliuwa askari wake ili amchukue mke wake.
  2.sarckozy aliingia madarakani akamtimua mkewe akachukua kifaa kingine(carla buny)
  3.mandela hakutaka longolongo za winie kakamata mke wa mshkaji wake maisha yakasonga.
  4.zuma amepigiwa mpaka na waziri wake lakini bado ni kiongozi imara.
  5huyo rais wako kahonga uwaziri ili apate jiko.
  6moi jirani yetu nk
  tunachotaka ni kichwa cha slaa hayo mengine watajuana na josephine na rozi.na wewe nakushauri kaa vizuri na mkeo watu watalamba na utabaki umeduwaa na hupati hata senti tano.
   
 16. k

  kanda2 JF-Expert Member

  #16
  Oct 4, 2010
  Joined: Apr 22, 2007
  Messages: 1,318
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  My 50cent

  Slaa anadai alikuwa "hajui" kuwa Josephine ni mke wa mtu, granted! sasa kishajua na vithibitisho vime tolewa vikiwemo hati za ndoa nk. Lakini kwa jeuri na anaendelea kumtangaza kuwa ni mchumba kwa maana nyingine anavunja sheria huku sasa akijua kuwa anavunja sheria.

  Huyu ndie anaepigiwa debe hapa aje kuwa "command in chief" kwa jeuri aliyo tukuka anavunja sheria mchana kweupe. Watanzani tuna elekea wapi?
   
 17. M

  MC JF-Expert Member

  #17
  Oct 4, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 751
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Kweli wewe ni Kandambili
   
 18. kibhopile

  kibhopile JF-Expert Member

  #18
  Oct 4, 2010
  Joined: Aug 5, 2010
  Messages: 1,307
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  crap,,,,
   
 19. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #19
  Oct 4, 2010
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Tunaelekea kuwamaliza mafisadi wooote kwanza then tuangalie kama maswala ya kingono kama nayo yanatuathiri au lah? kwasababu baadhi ya waliopo madarakani kwenye ngono wamo na kwenye ufisadi wapo, hebu tu-deal kwanza na ufisadi, maana huo unamuathiri kila mtu, lakini ndugu Jakaya Kikwete au Dr Slaa kuwa mzinifu/mtulivu haitusaidii.
   
 20. KAZIMOTO

  KAZIMOTO JF-Expert Member

  #20
  Oct 4, 2010
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 1,073
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  .

  Una maana Dr Slaa anaendelea kuzini. Makubwa hayo ya firauni ni madogo
   
Loading...