Kulinda tunu ya Muungano ni pamoja na kuuboresha

Kakke

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
1,883
1,482
[h=1][/h] Written by makame silima // 30/03/2014 // Habari // 1 Comment

Hawra+Shamte-401x272.jpg

Hawra Mohammed Shamte


Na Hawra Shamte


Posted Jumapili,Marchi30 2014 saa 12:58 PM


Hiyo maana yake ni kuwa tangu awali zilipaswa kuwapo Serikali tatu, lakini kwa kuwa Zanzibar iliruhusu mambo ya Muungano yaendeshwe na Tanganyika, Mwalimu Julius Nyerere hakuona umuhimu wa kutenganisha shughuli za Tanganyika na zile za Muungano hasa kwa sababu yeye alikuwa ndiye Rais wa Tanganyika na ndiye Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


“Muungano wa serikali mbili waliotuachia waasisi siyo uliopo sasa. Umebadilishwa mara nyingi, wakati mwingine bila ya kufanya mabadiliko kwenye Katiba. Waasisi walituachia Muungano wa nchi moja yenye Serikali mbili na siyo nchi mbili zenye Serikali tatu.”

Haya ni maneno aliyoyasema Jaji Joseph Warioba wakati alipowasilisha ripoti kuhusu Rasimu ya Pili ya Katiba, mbele ya Bunge Maalumu la Katiba.

Kwa hakika maneno haya ni swadakta na yanahitaji kudadavuliwa kwa kina si tu na mimi niandikaye safu hii, bali na Watanzania wote au niseme wapenda ukweli wote.

Tatizo la wengi wetu ni hofu, hofu imetutawala mpaka tunaogopa kivuli chetu wenyewe. Lakini sishangai kwa sababu ni kawaida ya watu kuogopa au hata kupinga mabadiliko yoyote yale yanapotokea.


Chukulia mfano mdogo tu wa chumba unacholala, akitokea mtu akabadilisha mwelekeo wa kitanda, akakiweka katikati badala ya pembeni ulikozoea, bila shaka cha kwanza utakachofanya ni kukunja uso, kisha ndipo utakapotoa maoni yako na kusema chumba hakijapendeza, au kumekuwa na kiza ama sasa wewe uliyezoea kulala pembeni kuna uwezekano wa kuanguka… ili mradi zohali zitakuwa nyingi.


Hiyo ndiyo hali inayojitokeza hivi sasa wakati Watanzania wanapojitathmini na kujipanga upya baada ya miaka 50 ya utaifa wao, lakini kwa binadamu kuwa na wasiwasi ni jambo la kawaida kabisa.


Kinachonishangaza ni kuona wadadavuaji wa mambo wakidadavua kuwa eti: “Mgogoro utakaozalishwa kwa kuifufua Tanganyika na kuleta Serikali tatu utakuwa msingi mama wa mitanzuko, kero nyingi zaidi na kifo cha Tanzania.”


Hii ni hofu tu miongoni mwa hofu nyingi tulizonazo Watanzania kwa sababu ya kuwapo uwezekano wa kutokea jambo tusilolizoea. Ni wazi kuwa wengi wetu hatukuikuta Tanganyika, hatuijui bali tunaisikia tu ilikuwapo na hata waliokuwapo wanasema kuwa hawaijui Tanganyika huru kwa sababu ilidumu kuwa huru kwa muda wa miaka miwili na miezi minne tu kuanzia Desemba 9, 1961 – Aprili 26, 1964.


Lakini ukweli huo hauondoshi ukweli kuwa Tanganyika ilikuwapo na ilikuwa nchi na sasa hatuzungumzii kuirudisha Tanganyika kama nchi iliyokuwapo kabla ya mwaka 1961 au hata baada yake, bali tunazungumzia kuwapo kwa Serikali ya Tanganyika iliyoungana na Serikali ya Zanzibar kuunda serikali ya Muungano ambayo kimsingi ipo ila imejificha nyuma ya Muungano, sasa kinachotaka kufanyika ni kuifichua na kuipa mamlaka yake, je, hilo nalo pia lina utatanishi?
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, alisema bila ya kumung’unya maneno kuwa waasisi walituachia Muungano wa nchi moja yenye Serikali mbili na siyo nchi mbili zenye serikali mbili.


Alhaj Aboud Jumbe aliyewahi kuwa Rais wa Zanzibar kuanzia Aprili 11, 1972 hadi Januari 30, 1984 alipolazimishwa kujiuzulu kutokana na kutenda dhambi ya kuhoji muundo wa Muungano, katika kitabu chake alichokiita The Partnership sura ya sita ukurasa wa 79 alielezea dosari za Muungano na kusema upo ukiukwaji katika Mkataba wa Muungano na Sheria za Muungano. Mkataba wa Muungano, 1964, ulitoa sura ya kuwapo kwa shirikisho la serikali tatu ambapo hapangekuwa na serikali moja iliyo na mamlaka makubwa kushinda nyingine.


“Mkataba wa Muungano ulitaka kuwapo kwa serikali tatu au mamlaka ambazo zingeundwa kiuunganishi ambazo katika waraka huo zilitajwa kuwa ni Tanganyika, Zanzibar na Jamhuri ya Muungano…”

Hiyo maana yake ni kuwa tangu awali zilipaswa kuwapo Serikali tatu, lakini kwa kuwa Zanzibar iliruhusu mambo ya Muungano yaendeshwe na Tanganyika, Mwalimu Julius Nyerere hakuona umuhimu wa kutenganisha shughuli za Tanganyika na zile za Muungano hasa kwa sababu yeye alikuwa ndiye Rais wa Tanganyika na ndiye Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Mwaka 2012 wakati wananchi walipokuwa wakitoa maoni yao mbele ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba walilizungumzia suala la muungano wanaoutaka kwa ufasaha kabisa.

Jaji Warioba anasema asilimia 61 ya wananchi waliotoa maoni kuhusu Muungano kwa upande wa Tanzania Bara walipendekeza muundo wa Serikali tatu, laiti Tume ya Jaji Warioba ingepata nafasi ya kuchapisha maoni yote ya wananchi, huenda tungepata mwanga zaidi wa kuona ni jinsi gani Watanzania Bara wanavyotamani kuwa na serikali yao.


Yafuatayo ni baadhi tu ya maoni yaliyojitokeza: “Watanganyika tumekosa fursa ya kuwa na Serikali tofauti na wenzetu Wazanzibari ambao wao wanayo Serikali. Kwa hiyo nataka kuona kuwa Katiba Mpya inairejesha Serikali ya Tanganyika ili kuleta uwiano sawa kati ya pande mbili za Muungano,” alisema Haji Juma mkazi wa Kata ya Jangwani jijini Dar es Salaam.

Thadeus Mangia alisema kuwa Muungano wa Serikali tatu utaondoa manung’uniko yaliyopo miongoni mwa wananchi kuwa upande fulani unaonewa na upande fulani wa Muungano ndiyo unaofaidika.

Wananchi kadhaa walilidadavua suala la Muungano na kusema kuwa katika Muungano huo walioathirika ni Watanganyika kwa kupoteza Serikali yao. Walisema Wazanzibari wana Rais na Serikali tangu mwanzo wa Muungano, lakini Watanganyika wamepoteza vyote, yaani Rais na Serikali.


Hayo ni baadhi tu ya maoni ya wananchi tena wa upande wa Tanzania Bara, lakini kwa upande wa Zanzibar nao walikuwa na yao wengi wao walihisi kukandamizwa na Tanzania Bara na walikuwa na mifano yao, hawa ndiyo waliotaka Zanzibar iwe na mamlaka yake kamili.

Hadidu za rejea ilizopewa Tume ya Jaji Warioba ni kuwa ihakikishe Muungano ambao ni tunu ya taifa unadumishwa; kwa kupendekeza muundo wa Muungano wa Serikali tatu, haina maana kuwa wanataka kuvunja Muungano, bali wanachotaka kwa dhati kabisa ni kuuboresha Muungano baada ya Muungano wa Serikali mbili kushindwa kutatua kero kwa nusu karne sasa.


Chanzo Mwananchi
 
Kuna argument Wa-Tanganyika wanapenda kuitumia sana kama ndio weapon yao ya kutaka Muungano kwa hali yoyote ile usivunjike sasa kwamba Muungano wa Zanzibar na Tanganyika una miaka 50, kwa hivyo, watu asilimia 85 wote wamezaliwa Tanzania, hivyo haiwezekani kiuhoji muungano na kuurekebisha kwa watu wake. Jee watu wenye argument hiyo watatwambiaje kuhusu Scotland ndani ya UK ambao muungano wao umekuwepo zaidi ya miaka 200 na sasa hakuna hata mtu mmoja aliyeiwahi Scotland independent na wanapigania kuifanya Scotland kuwa taifa huru.
Tathmini:

BONYEZA WEB
Scotland's Referendum 2014 | Scotland's Future – Your Guide to an Independent Scotland
 
Mimi nadhani issue ipo gharama, na hilo halikwepeki tukiingia kwenye serikali tatu. Na gharama zikishakuwa mzigo na kila mtu akawa mzalendo kwa taifa lake la asili zaidi ni wazi Muungano utavunjika.
 
Mimi nadhani issue ipo gharama, na hilo halikwepeki tukiingia kwenye serikali tatu. Na gharama zikishakuwa mzigo na kila mtu akawa mzalendo kwa taifa lake la asili zaidi ni wazi Muungano utavunjika.

Kama gharama basi nadhani serekali moja au kuvunja muungano ndio suluhusho la bei rahisi kabisa na wala sio mbili.

Kama hoja ni kulinda muungano, basi mbili ndio unahatarisha zaidi kuvunjika kwake.Ni bahati mbaya siwezi kusema moja kwasababu hoja hio haijadiliki kwa upande wa visiwani wala hakuna mfano duniani wa nchi iliopotea na kuwa mkoa.

Nimetoa maoni mwananchi na kutoa mfano kama Kenya iseme Tanzania/Tanganyika ifutwe na iwe mkoa kama mikoa mengine ya Kenya.Jee unahisi linajadilika ? Basi ni sawa kabisa na mzanzibari kumuelezea taifa lake lifutike na liwe mkoa.

Huo ni mfano haraka haraka tuu, lakini kiuhalisia kama Tanganyika itajiona ina nguvu za kijeshi na kujaribu hilo.Basi sina shaka Zanzibar itaingia kwenye vugu-vugu la kupigania uhuru na nadhani hio amani nayo itakuwa iko mashakani!
 
Back
Top Bottom