Kumbuka mawakili wa serikali/Tume lazima nao waandae utetezi na usishangae wakaomba muda kuandaa utetezi huo
Isitoshe kuna washitakiwa wawil ambao ni NEC na Raisi(serikali).Sasa hapo itategemea kama NEC itajitetea kivyake na serikali nayo itajitetea kivyake.
Tusubiri maana Mahakamani hakuna kesi rahisi hasa kukiwa na mawakili makini kwa pande zote mbili zinazohusika katika kesi.
Japo hii kesi tunaiona rahisi,lakini msishangae mambo yakawa tofauti.
Najua NEC na serikali watashindwa tu katika hii kesi ila ukweli huu hauzui ucheleweshaji wa maamuzi ya mahakama zetu.
Kwa Jaji anayeelewa /Jaji Mkuu lazima atachukua hatua ya hali ya Juu kuzitaka pande zote kuzingatia muda ilikusiwe na vikwazo na kama watashindwa kuzingatia time limit anaweza kutoa maamuzi on best interest of the Country and its people.