salumselemani
Member
- Feb 17, 2015
- 53
- 10
Safiiiiiiiiiiii
Safi sana.... Hatuwezi kuwa na sheria then mtu anaamua yeye ndio anatoa maagizo kinyume na sheria
Safiiiiiiiiiiii
Chadema kwa kulalamika,angekuwa mke angeachika siku ya ndoa
Kesi itapangiwa muda wa kusikilizwa tarehe 26
Nice move,ila pia wafanye utaratibu wa kumlima Kikwete kwa wawakilishi wa nchi za Ulaya,International Observers na ICC kwa kitendo chake cha kuingilia NEC huku akipotosha idadi ya wapiga kura na kutoa vitisho vya kutumia mabavu/kuvunja amani!!!
Usichokijua ni kuwa sheria ya Uchaguzi inasema siku ya kupiga kura hakutakuwa na mikusanyiko ya kisiasa.Mikusanyiko yote ya kisiasa mwisho wake ni siku ya mwisho wa kampeni ambayo ni tarehe 24 octoba 2015.Ukikusanya watu wako siku hiyo ya uchaguzi wawe wana UKAWA au CCM wakajikusanya mahali ni kosa kisheria.
Pili kwa mujibu wa sheria zinazohusu mikusanyiko ni lazima kutoa taarifa polisi kuwa kutakuwa na mkusanyiko mahali fulani na kwa lengo gani. Hivyo kama kurtakuwa na watu wenye lengo la kukusanyika popote inabidi wawasilishe maombi yao polisi wakijieleza wao ni akina nani ili wapewe ulinzi wa polisi
Tatu kuna sheria ya ardhi.Unaposema utakusanyika hapo kwenye mita 200 hilo eneo ni mali ya baba yako au mama yako? Huyo mwenye miliki ya hiyo ardhi karidhia? Hivyo kama kuna watu watakaotaka kukusanyika ni lazima wapeleke kibali cha mwenye eneo kuwa karidhia eneo lake litumike kwa mikusanyiko.Na kwamba mikusanyiko hiyo haitakuwa kero wala bugudha kwa wakazi wa eneo husika,majirani n.k Maana kama watu watajiamulia kukusanyika hiyo mita mia 200 bila mwenye eneo lake kuridhia ina maana ni uvamizi wa ardhi ya mtu bila ridhaa yake.Na huo ni uvunjifu wa amani kwenye eneo la watu.Hivyo Mahakama lazima iangalie maslahi ya wenye maeneo maeneo yao yasije vamiwa SIKU YA KUPIGA KURA NA KUKALIWA KWA MABAVU na hao wanaojiita walinda kura.
Polisi kwa kuliona hilo kuwa kutakuwa na uvunjaji sheria kwa watu kuvamia maeneo ya watu na kujikusanya wakasema kila mtu aende kwake asubirie kwake.Sababu vituo vya kupigia kura haviko mbali na makazi ya watu.Kwa nini watu wakae kwenye viwanja vya watu? Mahakama iliangalie hilo
Kwangu sikubali mtu akusanyike WALA KUWEKA MAKALIO YAKE KWENYE ENEO LANGU NITAITA DEFENDER NA GARTI LA WASHA WASHA HARAKA WAJE NA MABOMU NA VIRUNGU WAONDOE WAVAMIZI KWENYE ENEO LANGU.
Hawa akina KIBATALA wanataka kuleta vurugu na ugomvi kati ya wenye maeneo na hao watu anaotaka wakusanyike hizo mita mia mbili sababu sio kwao ni kwa watu.
Eti bila haya lowasa na mbowe wanatoa amri mkimaliza kura kaeni mita 200.Hilo eneo wanaloamrisha watu wakae ni la baba yake au mama yake lowasa au mbowe.Sheria ya ardhi iheshimiwe majaji msimamie hilo kwa maslahi ya wenye maeneo yao.Mkiwakubalia mnawaweka wenye maeneo matatizoni.
Tayari wakili jembe na nguli Peter Kibatala akiambatana na wanasheria nguli wa Ukawa Prof Safari, Mallya na Tundu Lissu asubuhi ya leo amefungua kesi mahakama kuu kuishitaki NEC kwa ukiukwaji wa sheria juu ya wananchi kukaa mita mia mbili na kulinda kura.
Kesi imefunguliwa under certificate of urgency nadhani kama sijakosea kwa kiswahili ni 'hati ya dharura' ili isikilizwe na tafsiri itoke kabla ya uchaguzi.Tayari jalada lishapelekwa kwa pilato na wanasheria nguli wa Ukawa wamejipanga kwa hoja za nguvu na ushahidi wa kutosha.
Pia jopo la wanasheria nguli wa UKAWA wameiomba mahakama kuu ya Tanzania kutoa tafsiri ya kisheria juu ya matamshi ya rais wa nchi kuwa alitumia mamlaka gani kuvaa kazi za tume.
Haisaidiii kitu...hatopata jibu mpaka uchaguzi uishe....umeshaambiwa ukishapiga kura nenda kalale nyimbani kwako....unataka nn sasa.???sheria sheria sheria...babake nani.????
Mnataka kuiba nini!? mbona mnang'ang'ania tuondoke!? Hatuondokiiijjjijjjjjjiiiiiijii.
Kwa hiyo shida ni kusema tunalinda KURA basi? Nawashauri CHADEMA/UKAWA wasiseme tunalinda KURA na wasiende kukaa umbali wa mita 200 tunatakiwa tusimame mita moja. Kila mwana UKAWA awahi kituoni mapema kwenye mstari lakini asipige KURA inapokaribia zamu yake arudi nyuma mpaka wana ccm wote, wazee na wanawake wamalize ndipo mafansi wa UKAWA wapige KURA cha kuzingaatia ni kuhakikisha kuwa kwenye foleni kabla ya muda wa kufunga vituo. Maana CCM wameandaa vurugu ili serikali ya 2015/20 iwe ya mseto na KWA KUMPA lOWASA UWAZIRI MKUU tuwe makini sana na hawa jamaa.
Ukae kwenye public road??? Ukikaa kwenye public road ina maana umefunga bara bara wakati inatakiwa kuwa wazi ili kuwezesha FFU na defender zao wapite kwa uhuru na watumiaji wengine wa barabara waitumie kwa uhuru.
Kukaa kwenye public road ni kujitangazia kiyama wewe mwenyewe mkaaji sababu polisi watakuja na mabomu na virungu kuvurumisha waliofunga baraba kwa kukaa ili kuhakikisha wanaifungua ili watumiaji wengine wa bara bara waendelee kuitumia.
Vita imenoga,man to man,kona to kona,mpaka wakubali ha ha ha
Ok, basi ngoja tusubiri hao polisi wasiofika elfu arobaini dhidi ya vituo vya kupigia kura elfu sitini na wapiga kura milion ishirini na ushee
Hata hao askari hawaipendi ccm, chukua hiyo. Hivi vi laki tatu mlivyowaongezea juzi wamegundua ni danganya toto. Ccm out. To hell ccm.Kwani hujui kuwa majeshi yote ya ulinzi na usalama yanakuwa kazini kipindi cha uchaguzi?
Wana ndege na helikopta na magari standby yenye spidi za kuua mtu.Kiasi kuwa likitokea jambo mahali pakizidiwa nguvu ni dakika tu magereza,jwtz,usalama wa taifa,JKT NK watakuwa wameshatua hapo tayari kutembeza kipigo cha mbwa mwizi.
Na makomandoo wengi watakuwa wamevaa kiraia wakisubiria raia anayetaka kukiinukisha wakiwa wamejichanganya na raia.Jaribu uone kama hawanyofoa hicho kinyeo chako kilicho katikati ya makalio.
washauri mkuu maana tunawaambia hawasikii.watavunjwa miguu bure...!!