Kulikuwa na uhalali gani kwa Chief Mkwawa kutambulika kama 'Shujaa?

Hii ID yako ya infantry soldier haiakisi uelewa wako wa masuala ya kivita.

Yaani kitendo tu cha wajerumani kuondoka na fuvu lake hakikushitui. Kwao ni MTU aliyewatesa mno katika mapambano ya msituni.

Eti mtu anayejiua ni dhaifu. Mbona Hitler alijiua kwa kujitumbukiza kwenye acid.

Hata Gaddafi kwa taarifa yako alitaka kujimaliza na bastola yake dhahabu kabla hajawahiwa. Katazame video ya mauaji ya Gaddafi.

Alafu Mkwawa hakujiua kwa sababu ya hofu pekee ila ni kanuni ya kivita unapozidiwa na hakutaka kuwakatisha tamaa wanajeshi wake kwa sababu ikiwa wangemuua yeye kama kiongozi ingekuwa rahisi kuwamaliza wengine.

Alaf unafananishaje mazingira ya kifo cha mkwawa na cha Gaddafi, ikiwa mkwawa alipambana na bunduki kwa mishale kwa asilimia kubwa na tena akipambana na mojawapo ya mataifa makubwa yenye jeshi kubwa na teknojia ya kisasa huku yeye akiwa hata sio taiga bali empire iliyo ndani ya taifa, huku akiwa na teknolojia duni.
 
Mkuu, kwenye comment yako moja hapo nyuma ulisema kwamba, askari/kiongozi hujiua ili kuweza kutunza siri. Sasa ina maana Gadaffi na Saddam walikuwa hawana siri za kutunza?
Suala la siri ni muhimu sana katika mikakati ya kijeshi bila kujali adui ni inferior kiasi gani,kwa mtu mwenye elimu /historia nzuri kuhusu Ngome ya Yesu (Fort Jesus) ya Mombasa anaweza akatuongoza, kumbuka Gaddaf zilitumika pesa zake mwenyewe alizoficha Ulaya kumuua mwenye mali ambazo zilikuwa ni nyingi mno,adui walihitaji lazima afe ili wale kwa ulaini pesa waliyomuibia,pia lazima nchi iwe na vurugu ili waibe mafuta kiulaini,Mtwa Mkwawa ni shujaa zaidi ya hao unaowasifu kwa sababu nyingi sana ila kwa kuwa watu weusi hatutafiti,hatusomi na hatuandiki historia zetu wala kuweka record,machifu wengi tu walipigana na wazungu na wakashinda lakini kwa wakati huo alikuwa anaandika mzungu,sijui kama angethubutu kusema sisi wazungu tulishindwa vita mara kumi.
 
Mkuu upo sawa lakini kwa upande mwingine ataona alistahili kuitwa shujaa! Mhehe huyo alipambana na wajerumani kwa muda wa miaka minane akitumia magobole na silaha za jadi huku jamaa wakiwa na silaha nzuri! Aliwahenyesha mpaka msituni, Kuna mengi sana aliyafanya katika kupambana na wakoloni hao! Lait kama ingewezekana kuyarecord na kuyaonyesha matukio ya mapambano yake ilikuwa ni kama Filamu moja inaitwa "The Hard Way"!
Babu yetu huyo alipambana sio mchezo aisee! Alilazimika kujiua sababu alijua kuwa alikuwa ameshawaumiza na ameshawasumbua sana hivyo mateso ya kikatili ambayo wangempa yangekuwa si ya kawaida!
 
kwanza umeanza kwa kuharibu kudhani israel inaumaalumu wowote ,na sijui imetokeaje kwenye thread za kishujaa,anyway madini hayo yakuletewa,swala la kujiua useme siri nalielewa na mkwawa ni shujaa maana alipambana na wajerumani miaka minne (najua hujui) polini wakiwa wanamzidi technology mbali ,kukamatwa kwake yeye wangekutumia kuwavunja nguvu wahehe ya kimapinduzi maana wangeamua hata kuuburuza mwili wake kila mahali ili kuwakatisha moyo wahehe.
aidha wahehe waliendelea kuwa shida kuwatawala na hata wajerumani kadhaa waliandika kuwa watu wenye kiburi ,wavivu na hasira ,hata mashambani mwao wajerumani waliajiri wakinga na wabena sio wahehe .
Asante kwa ufafanuzi kuhusu wakinga na wabena
 
Kujiua ni uoga wa maisha mkuu na waoga kamwe hawatauona ufalme wa Mungu. Mzalendo hajiua hata siku moja.
Mkuu wewe ni muandishi wa hizi makala, na unajua kabisa Majasusi huwa wanakuwa na vidonge vya sumu midomo mwao ili wakikamatwa na kuteswa wajiue ili kulinda siri., unafikiri ni uoga huo??

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Habari za wakati huu ndugu zangu wa humu jamiiforums.

Kulikuwa na uhalali gani wa Chief Mkwawa kutambulika kama "shujaa"? Kamwe hakuna askari anayeweza kuitwa shujaa kwa kuogopa adui kisha kujiua mwenyewe.

View attachment 1716322

Mbona Muamar Gadaffi wa Libya na Saddam Hussein wa Iraq hawakujiua kabla ya kukamatwa na wazungu? Mkwawa alikuwa shujaa ama askari muoga?

UOGA SIO SIFA NJEMA YA MWANAUME MPIGANAJI
=====
Uoga ni tabia ambayo hofu nyingi humzuia mtu kupambana na hatari au kukabiliana na adui. Uoga unaonyesha uwezo wa mtu kukosa tabia ya ujasiri wakati wa changamoto. Katika kanuni za kijeshi za nchi nyingi hapa duniani, uoga katika vita ni sawa sawa na uhalifu.

Vitendo vya uoga, kwa muda mrefu tangia vita ya kwanza ya dunia, vimeadhibiwa na sheria za kijeshi, ambazo inafafanua vema makosa yanayohesabika kama uoga, ikiwa pamoja na kumkimbia adui au kujisalimisha kwa adui pasipo kupata amri kutoka kwa wakubwa. Wale ambao walikamatwa walikuwa, mara kwa mara, wakipelekwa mahakamani na adhabu ya vitendo kama hivyo kwa kawaida huwa ni kali sana.

Siku zote ulimwengu umewaheshimu majasiri na kuwalaani waoga. Kuwa jasiri ni muhimu kwa mwanamume kama vile kuwa msafi kwa mwanamke, na muoga kati ya wanaume ana sifa mbaya kama kahaba kati ya wanawake.

Kujiua huitwa ni uoga kwa sababu inahitaji ujasiri wa hali ya juu sana ili uweze kuishi katika dunia iliyojaa kila aina ya changamoto, inahitaji mtu kuwa na mtazamo sahihi juu ya maisha na utulivu mkubwa wa akili. Pamoja na shinikizo na shida zote, vuta nikuvute za maisha ambavyo tunakabiliwa navyo, baadhi ya waoga huamua kuwa na mawazo hasi na kushindwa kupambana tena na badala yake kuchagua kufa.

KWA UFUPI SANA KUHUSU KIFO CHA CHIEF MKWAWA
=====
Kichwa cha mtemi kinasemekana kilikatwa na Wajerumani na kutumwa Berlin kilipohifadhiwa katika makumbusho, awali Berlin na baadaye Bremen. Waingereza waliochukua utawala wa koloni mwaka 1918 baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia walitaka kuonekana kama mabwana wema.

Mkuu wa serikali ya kikoloni ya Tanganyika alipendekeza kurudisha fuvu kwa sababu Wahehe walishirikiana na Waingereza wakati wa vita. Hivyo kuna kipengele 246 katika mkataba wa Versailles kinachosema: "Katika muda wa miezi 6 baada ya kuthebitishwa kwa mkataba huu. Ujerumani itakabidhi fuvu ya Sultani Mkwawa iliyohamishwa kutoka Afrika ya Mashariki ya Kijerumani na kupelekwa Ujerumani kwa serikali ya Mfalme wa Uingereza.

Wajerumani walikataa habari za fuvu hii na Waingereza waliamua ya kwamba ilishindikana kuikuta. Lakini baada ya vita kuu ya pili ambako Ujerumani penyewe ilivamiwa na wanajeshi wa Uingereza gavana Twining wa Tanganyika alikumbuka habari za fuvu akatembelea Ujerumani na kutazama mafuvu ya makumbusho ya Bremen.

Katika mkusanyiko wa fuvu 2000 zilikuwa 84 zenye namba zilizoonyesha zilitoka kiasili katika Afrika ya Mashariki ya Kijerumani. Hapa alizipanga kufuatana na ukubwa na kutazama zile zilizokuwa na vipimo vya karibu na ndugu za Mkwawa aliowahi kupima kabla ya safari yake. Hapa aliteua fuvu yenye shimo kwa sababu taarifa ya kale ilisema Mkwawa alijiua kwa kujipigia risasi kichwani.

Kulikuwa na uhalali gani kwa askari aliyejiua kutambulika kama "shujaa"?

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
kwani siku ya mshujaa wanakumbukwa walio hai au wale waliokufa
 
Ni shujaa kwa sababu ni bora kujiua kuliko kukamatwa na adui akakutesa kiasi cha kukufanya kutoa siri za kuangamiza wenzako wengi.

Lakini pia kuuwawa na adui kwa kiongozi mkubwa ni ishara ya udhaifu wa mifumo ya kupambana na adui.

Hii mojawapo ya nguzo muhimu ya kuwakunbusha wakoloni kuwa kipindi kile hawakutundea haki wanazodai leo tuzifanywe.
Hapa kwenye upande wa haki ninakuunga mkono kwa maana ukoloni uliacha madhila makubwa sana kwetu sisi waafrika kwa ujumla.
 
Habari za wakati huu ndugu zangu wa humu jamiiforums.

Kulikuwa na uhalali gani wa Chief Mkwawa kutambulika kama "shujaa"? Kamwe hakuna askari anayeweza kuitwa shujaa kwa kuogopa adui kisha kujiua mwenyewe.

View attachment 1716322

Mbona Muamar Gadaffi wa Libya na Saddam Hussein wa Iraq hawakujiua kabla ya kukamatwa na wazungu? Mkwawa alikuwa shujaa ama askari muoga?

UOGA SIO SIFA NJEMA YA MWANAUME MPIGANAJI
=====
Uoga ni tabia ambayo hofu nyingi humzuia mtu kupambana na hatari au kukabiliana na adui. Uoga unaonyesha uwezo wa mtu kukosa tabia ya ujasiri wakati wa changamoto. Katika kanuni za kijeshi za nchi nyingi hapa duniani, uoga katika vita ni sawa sawa na uhalifu.

Vitendo vya uoga, kwa muda mrefu tangia vita ya kwanza ya dunia, vimeadhibiwa na sheria za kijeshi, ambazo inafafanua vema makosa yanayohesabika kama uoga, ikiwa pamoja na kumkimbia adui au kujisalimisha kwa adui pasipo kupata amri kutoka kwa wakubwa. Wale ambao walikamatwa walikuwa, mara kwa mara, wakipelekwa mahakamani na adhabu ya vitendo kama hivyo kwa kawaida huwa ni kali sana.

Siku zote ulimwengu umewaheshimu majasiri na kuwalaani waoga. Kuwa jasiri ni muhimu kwa mwanamume kama vile kuwa msafi kwa mwanamke, na muoga kati ya wanaume ana sifa mbaya kama kahaba kati ya wanawake.

Kujiua huitwa ni uoga kwa sababu inahitaji ujasiri wa hali ya juu sana ili uweze kuishi katika dunia iliyojaa kila aina ya changamoto, inahitaji mtu kuwa na mtazamo sahihi juu ya maisha na utulivu mkubwa wa akili. Pamoja na shinikizo na shida zote, vuta nikuvute za maisha ambavyo tunakabiliwa navyo, baadhi ya waoga huamua kuwa na mawazo hasi na kushindwa kupambana tena na badala yake kuchagua kufa.

KWA UFUPI SANA KUHUSU KIFO CHA CHIEF MKWAWA
=====
Kichwa cha mtemi kinasemekana kilikatwa na Wajerumani na kutumwa Berlin kilipohifadhiwa katika makumbusho, awali Berlin na baadaye Bremen. Waingereza waliochukua utawala wa koloni mwaka 1918 baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia walitaka kuonekana kama mabwana wema.

Mkuu wa serikali ya kikoloni ya Tanganyika alipendekeza kurudisha fuvu kwa sababu Wahehe walishirikiana na Waingereza wakati wa vita. Hivyo kuna kipengele 246 katika mkataba wa Versailles kinachosema: "Katika muda wa miezi 6 baada ya kuthebitishwa kwa mkataba huu. Ujerumani itakabidhi fuvu ya Sultani Mkwawa iliyohamishwa kutoka Afrika ya Mashariki ya Kijerumani na kupelekwa Ujerumani kwa serikali ya Mfalme wa Uingereza.

Wajerumani walikataa habari za fuvu hii na Waingereza waliamua ya kwamba ilishindikana kuikuta. Lakini baada ya vita kuu ya pili ambako Ujerumani penyewe ilivamiwa na wanajeshi wa Uingereza gavana Twining wa Tanganyika alikumbuka habari za fuvu akatembelea Ujerumani na kutazama mafuvu ya makumbusho ya Bremen.

Katika mkusanyiko wa fuvu 2000 zilikuwa 84 zenye namba zilizoonyesha zilitoka kiasili katika Afrika ya Mashariki ya Kijerumani. Hapa alizipanga kufuatana na ukubwa na kutazama zile zilizokuwa na vipimo vya karibu na ndugu za Mkwawa aliowahi kupima kabla ya safari yake. Hapa aliteua fuvu yenye shimo kwa sababu taarifa ya kale ilisema Mkwawa alijiua kwa kujipigia risasi kichwani.

Kulikuwa na uhalali gani kwa askari aliyejiua kutambulika kama "shujaa"?
Naona udhaifu katika swali lako:
1. Mifano iko mingi ambako watu walijiua katika hali za mapigano wakiona hawawezi kushinda, wakiona umuhimu wa kutokamatwa, na bado wengi waliwatazama au wanawatazama kama mashujaa.

Mifano kadhaa inahusu watu wanaojua wanatunza siri fulani ambayo inapaswa kutunzwa - basi walijiua ili wasikamatwe na kulazimishwa kufichua siri (mbinu zilikuwa nyingi tangu kale, kuanzia mateso hadi ulevi na madawa..)

Mfano mashuhuri zaidi labda ni watetezi wa ngome ya Masada nchini Israeli miaka 1948 iliyopita. Katika vita ya Wayahudi dhidi ya Waroma mwaka 73/74 walizingirwa na jeshi la Waroma waliofaulu kuvunja ukuta. Katika usiku kabla ya shambulio la mwisho watetezi waliamua kujiua wote. Kuna taarifa juu ya hotuba ya kamanda Myahudi Eleasar ben Jaʾir aliyetaja sababu: Wake wetu waliopo watabakwa na kuuawa baadaye, watoto wetu watauzwa kama watumwa, na Waroma watapora mali yetu. Hivyo waliteua wanaume 10 waliopewa kazi ya kuchinja wengine, na hatimaye kujiua wenyewe. Kabla ya mauaji walichoma mali yao yote yenye thamani. Waroma waliposhambulia, walikuta maiti tu, na wanawake 2 pamoja na watoto 5, waliofaulu kujificha. - Hao watetezi wa Masada wanatazamiwa kama mashujaa katika Israel ya leo. Katika miaka ya 1956 - 1991 jeshi la Israel lilipeleka askari wapya wote huko kwenye maghofu ya Masada ili wale kiapo cha mwanajeshi kwenye mahali ambako hao watetezi wa zamani walikufa.
Kwa hiyo kujiua hakusemi kitu chochote kuhusu swali la shujaa.

2. Sababu yangu ya pili: huleti ufafanuzi je shujaa machoni pako ni nini au nani.
 
Naona udhaifu katika swali lako:
1. Mifano iko mingi ambako watu walijiua katika hali za mapigano wakiona hawawezi kushinda, wakiona umuhimu wa kutokamatwa, na bado wengi waliwatazama au wanawatazama kama mashujaa. Mifano kadhaa inahusu watu wanaojua wanatunza siri fulani ambayo inapaswa kutunzwa - basi walijiua ili kutofika hali ambako watalazimishwa kumwambia adui (mbinu zilikuwa nyingi tangu kale, mateso hadi ulevi...)
Mfano mashuhuri zaidi labda ni watetezi wa ngome ya Masada nchini Israeli miaka 1948 iliyopita. Katika vita ya Wayahudi dhidi ya Waroma mwaka 73/74 walizingirwa na jeshi la Waroma waliofaulu kuvunja ukuta. Katika usiku kabla ya shambulio la mwisho watetezi waliamua kujiua wote. Kuna taarifa juu ya hotuba ya kamanda Myahudi Eleasar ben Jaʾir aliyetaja sababu: Wake wetu waliopo watabakwa na kuuawa baadaye, watoto wetu watauzwa kama watumwa, na Waroma watapora mali yetu. Hivyo waliteua wanaume 10 waliopewa kazi ya kuchinja wengine, na hatimaye kujiua wenyewe. Kabla ya mauaji walichoma mali yao yote yenye thamani. Waroma waliposhambulia, walikuta maiti tu, na wanawake 2 pamoja na watoto 5, waliofaulu kujificha. - Hao watetezi wa Masada wanatazamiwa kama mashujaa katika Israel ya leo. Jeshi la Israel ilipeleka askari wapya wote huko ili wale kiapo cha mwanajeshi kwenye mahali ambako hao watetezi wa zamani walipokufa.
Kwa hiyo kujiua hakusemi kitu chochote kuhusu swali la shujaa.
Mkuu, ninaona umeandika maelezo meeeengi na kujaribu kujitetea askari wanaojiua kwa kuogopa mapambano na kisha kujaribu kutumia mfano wa Wayahudi kama ndio justifications bora.

Askari anayejiua kwa kuogopa kupambana, awe muafrika, mwaarabu, mchina au mzungu, huyo kwangu mimi sio shujaa hata kidogo ukilinganisha na yule aliyekamatwa na kisha kuuwawa...
 
Mkuu, ni siri gani ambazo mhehe angeweza kuzificha mfumo wa taarifa wa taifa kubwa kama Ujerumani aliyetawala takribani 90% ya Ulaya nzima kabla ya WWII?...
Kwa mfano hupendi kutoa majina ya hao waliokusaidia?
Menginevyo tafadhali jipatie kitabu cha historia yenye ramani. Ujerumani haikutawala %90 za Ulaya kabla ya Vita Kuu ya Pili.
Tena Mkwawa alikufa miaka mingi kabla ya Vita Kuu ya Kwanza.
 
Mkuu, ninaona umeandika maelezo meeeengi na kujaribu kujitetea askari wanaojiua kwa kuogopa mapambano na kisha kujaribu kutumia mfano wa Wayahudi kama ndio justifications bora.

Askari anayejiua kwa kuogopa kupambana, awe muafrika, mwaarabu, mchina au mzungu, huyo kwangu mimi sio shujaa hata kidogo ukilinganisha na yule aliyekamatwa na kisha kuuwawa...
Sina ya kujitetea hapa hata kidogo. Kaka tafadhali jaribu kusoma historia ya Mkwawa. Siku zake za mwisho alikuwa mgonjwa. Hakuweza kukimbia tena. Hakuwa na sababu kuogopa mapambano maana hakuwa na uwezo wa kupigana. Nahisi alichoka na hakutaka kukamatwa, katika hali yake uwzekano mkubwa wangemkamata hai. Katika gobori lake alikuwa na risasi 1 tu. Waliomfuata walikuwa kundi dogo.
Kama angekamatwa aliweza kuwaza wangemrudisha Iringa kama mfungwa na kumnyonga pale hadharani.
Na labda kumpiga hadi anatoa majina yote ya hao waliomsaidia katika miaka yake ya vita ya msituni.

Menginevyo, ukiona maelezo yangu kuhusu mfano wa watetezi wa Masada yalikuwa mengi - heri usiandike kuhusu historia. Maana kwa somo la historia unahitaji kusoma. Mengi! Sana!

Nimekupa mfano wa hao watetezi waliojiua na leo wanakumbukwa kama mashujaa wa kitaifa. Pinga tu, ukiweza kutaja sababu.
 
Alafu Mkwawa hakujiua kwa sababu ya hofu pekee ila ni kanuni ya kivita unapozidiwa na hakutaka kuwakatisha tamaa wanajeshi
Mbona Saddam Hussein hakujiua? Ina maana himaya ya wahehe ya miaka hiyo ya zamani ilikuwa na siri nzito kuzidi Iraq ya mwaka 2003?...
 
Back
Top Bottom