Kulikuwa na Sababu ya Watoto wa Kikwete kuhudhuria sherehe za kuapishwa Mawaziri?

Mfalme asipowashirikisha warithi wake katika day to day activities za ufalme watajifunzaje kazi wanazotakiwa kurithi? Haya ni mafunzo kwa vitendo jamani!
Hii ndio point ya Muhimu!!
Hakuna jingine zaidi ya hilo!
 
Mkuu hiyo ndio tunaiita miiko ya uongozi, hapa kinachotia shaka ni conflict of interest,
hao watoto wana haki kabisa ya kuhudhuria hiyo sherehe, lakini swali ni kuwa wangeweza kuhudhuria kama Baba yao asingekuwa rais?

kuna makosa serikali ya JK inayafanya katika hili la miiko ya uongozi, tukiacha hili la JK na wanae, kuna hili la January Makamba na Dadaye, Kama utaratibu ungefuatwa vizuri (SIo Sheria bali Busara), January asingepewa unaibu (Mawasiliano) wa kwenda kuwa polisi wa dadake (Vodacom), busara ingekuwa ni kumpa wizara nyingine tu

Hapo kwenye MIIKO ya uongozi ndo panapofanya serikali ya JK ijae uozo mkuu! Nakuunga mkono mkuu!
 
Mbona Mwanaasha hayupo jamani au keshapelekwa tution Brazil?
 
Kwa lugha nyepesi unasema walijipendekeza kwenda kuuza sura?
Wengine ni umaarufu unawahangaisha Fidel80. Tunaowajadili hapa ni watoto wa Rais wetu. WJM naye akataka tujue naye alikuwepo. Mimi ningekuwa WJM, alipo JMK nisingepasogelea kwa kuwa hampendi kabisa Mzee wao.
 
- mkuu mleta mada kwani katiba ya jamhuri inasemaje kuhusu watoto wa the sitting president na sherehe za ikulu?

- halafu pia uweke wazi katiba hiyo hiyo inasema nini kuusu hao wananchi wengine wa kwaida waliohudhuria huko jana, infact na mimi nilikuwepo pia, i mean ndio njia pekee ya kukata mzizi wa fitina, otherwise isije ikawa wivu na chuki binafsi bila hoja za msingi! Au?

William.

sio kila kitu kinafanyika lazima kufuata katiba. Madhara yanayotokana na negative perception kutoka kwa wanajamii yanaweza kuwa mabaya zaidi kwa hawa watoto wa rais. Kwa kifupi tu mpaka sasa hawa watoto hawana picha zuri ndani ya mioyo ya baadhi ya watanzania wengi. Hii ina negative implications katika maisha yao ya baadaye.
 
- Mkuu mleta mada kwani katiba ya Jamhuri inasemaje kuhusu Watoto wa The sitting President na Sherehe za Ikulu?

- Halafu pia uweke wazi Katiba hiyo hiyo inasema nini kuusu hao wananchi wengine wa kwaida waliohudhuria huko jana, infact na mimi nilikuwepo pia, I mean ndio njia pekee ya kukata mzizi wa fitina, otherwise isije ikawa wivu na chuki binafsi bila hoja za msingi! au?

William.

@ William
Kwan wewe ungekuja na huo mwongozo wa katiba juu ya uwepo wa hao kina riz1 na hata hao watu wengine ungepungukiwa nn,,, Halafu umeambiwa na nani kuwa mtoa uzi yawezekana amesukumwa na wivu ndio maana amekuja na bandiko hilo.
Binafsi nilichoelewa ni yeye kuhoji uwepo wa hao vijana..
 
saif Al islam gadhaf, Muttasin Gadhaf, Khamis Gadhaf ??????? haya twendeni tu
 
- Mkuu mleta mada kwani katiba ya Jamhuri inasemaje kuhusu Watoto wa The sitting President na Sherehe za Ikulu?

- Halafu pia uweke wazi Katiba hiyo hiyo inasema nini kuusu hao wananchi wengine wa kwaida waliohudhuria huko jana, infact na mimi nilikuwepo pia, I mean ndio njia pekee ya kukata mzizi wa fitina, otherwise isije ikawa wivu na chuki binafsi bila hoja za msingi! au?

William.

Sherehe inafanyikia nyumbani kwa mzazi wa watoto hao, hivyo ni lazima wahudhurie hata kama ni ya malkia wa sheba lazima watoto wa Selemani walihudhuria.

Lakini je wewe William ulienda kama nani? Hii tu ilinishangaza?
 
Pengine baadhi ya wateule wa Rais wetu ni chaguo la hawa wanae?

Hii kitu Heche aliitamka Arusha juzi kwenye rally ya CDM na nikasikia police wanamuhoji!!

Pamoja na kwamba alitumia lugha kali na jazba lakini alikuwa na point ya msingi kabisa!!

Kuna mawaziri wamewekwa pale kwa interests za kibiashara za hii familia as long as ni family business ni lazima king makers wawepo kwani hua kuna makubaliano maalumu!!

Le Mutuz nadhani ni katika kuendelea kutafuta na kutengeneza cartel za mnuso wa keki ya Taifa ndio maana alihudhuria sherehe hizo, sidhani kama kuna kitu chochote cha maana kilicho mpeleka!
 
Iwe itakavyokuwa; kama ni wivu/wivu wa kike au la. Bazazi hajali. Kuna taarifa kuwa Mhe Che-Nkapa aliwapika marufuku waanaye kwenda Ikulu kwa shughulu iwayo yote, na walipokuwa na shida naye basi aliwafuata pale Sea View. Labda alifanya hivyo kurudisha heshima ya Ikulu baada ya kuwa na wageni wa kila aina. Au alitaka kuifanya Ikulu iogopeke kama sehemu takatifu (ritual site). Kwanini JK ameruhusu hii? Tutakafari na tukuchue hatua
 
mimi nadhani sasa tuwe na jukwaa la solid politics na jukwaa la light politics. Ishu kama hii kuijadili kama political issue per se ni kujivunjia heshima.
 
naomba kukuuliza mtoa mada,kwa mfano kwenu kuna uwanja wa wazi ambao sherehe zinafanywa hapo bure bila malipo,je mratibu wa sherehe anaweza kualika watu wengine na familia zao akaacha kuwaalika familia ya mwenye mji? au mfano mwingine,baba yako na rafiki zake pamoja na familia zao na watoto wanafanya sherehe kwenye eneo la nyumba yenu,je nyie hamtaalikwa?jiweke wewe kwenye nafasi ya riz 1 then jijibu mwenyewe !siajabu ungetaka kukaa high table!
 
Tatizo kubwa ni show business kwenye series issues JK amegeuza Ikulu ni Kama Theatre, kwa Bahati Mbaya zaidi inatughalimu walipa kodi sana. Jaribu kuangalia nchi za zetu tukio la jana ni low key affair ila Kwa Msani wetu Ni sherehe so tusiwalaumu watoto lawama kwa Mkuu wa Kaya
 
Naomba niwakumbushe,katika baraza hili jipya yumo rafiki wa kufa na kupona wa ridhiwani kikwete nae ni.
Steven masele (mb) shinyanga-naibu waziri wa nishati na madini
mwaka juzi alichakachua kura akisaidiwa na ridhiwani hadi akashinda kwa kura moja
kesi ya kupinga ushindi wake akasiadiwa na ridhiwani kikwete,ushahidi upo kabla ya hukumu kusomwa ridhiwani alienda shinyanga na walikutana hotelini tunajua kila kitu.
 
Ah! mambo mengine yanchekesha sana, nani kakwambia JK anawatayarisha watoto wake kuwa wafalme? hivi inaigia akilini kwamba siku ya sherehe JK awe anawafungia wanawe chumbani wasionekane wakichanganyikana na raia/mawaziri hili asije kueleweka vibaya, tusiwe na mawazo potofu jamani.

Mkuu utacheka sana usipokuwa makini,, mtoa mada ameuliza kulikuwa na umuhimu wa akina riz1 kwenye hizo sherehe?
Hakuna mantiki yeyote JK kuwafungia vijana wake siku ya sherehe, swala ni kwamba upo umuhimu wa wao kuwepo? Na je kama haupo wamehudhuria kama nani na kwa nafasi gani waliyo nayo kiutendaji na kiutawala Serikalini..
Na fahamu kuwa wageni waalikwa hawapo pale kuchanganyikana wako specifically kuhudhuria hizo sherehe..Asa unaposema eti wasiruhusiwe kuchanganyikana na raia/mawaziri, inatia ukakasi kidogo, hata hivyo si kila tukio lafaa wao kijichanganya ni busara wapime uzito wa tukio, vinginevyo waende sehemu zinazowahusu..
 
Back
Top Bottom