Kulikuwa na Sababu ya Watoto wa Kikwete kuhudhuria sherehe za kuapishwa Mawaziri? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kulikuwa na Sababu ya Watoto wa Kikwete kuhudhuria sherehe za kuapishwa Mawaziri?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, May 8, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  May 8, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Marais toka awamu ya kwanza hadi ya Tatu hatuwaona watoto wao kwenye hizo sherehe za Mawaziri kuapishwa

  Ni Miaka Miwili na Nusu imebaki wataichukua ikulu hapo 2015?

  [​IMG]
  Ridhiwan Kikwete akizungumza na aliyekuwa rais wa Yanga Jamal Malinzi wakati wa hafla hiyo katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam leo.

  [​IMG]
  Miraji Kikwete akiwa na wadau wengine katika hafla hiyo
   
 2. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #2
  May 8, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Ndio wanaandaliwa kujifunza kuapisha na kuapishwa umesahau hii nchi ni ya usultani mkuu?
   
 3. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #3
  May 8, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Mh! Tusije fanya tena makosa 2015, huyu miraji si ndiyo alikuwa IT wa uchaguzi wa 2010 na inasemekana ali-master mind lile zoezi la wizi wa kura. Mimi ningekuwa mtoto nisingekuja hapo ikulu.
   
 4. NusuMutu

  NusuMutu JF-Expert Member

  #4
  May 8, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 423
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  nawewe naye huna dogo!, ulitaka wakauzie wp sura? Kwao ndo kule,na jana brassband ndo hiyo kiwanja cha nyumbani, juice ya kumwaga, sasa ulitaka miraj na riz1 waje tupigane nao vkumbo uswaz? Kwa taarifu tu na mwana**** naye alikuwepo!
   
 5. mpayukaji

  mpayukaji JF-Expert Member

  #5
  May 8, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kwa ufalme tulio nao sasa si kosa. Iwapo wanaweza kuwasukia watu dili hadi wakateuliwa uwaziri watashindwa uapishaji ambao ni matokeo ya dili zao? Nani mara hii kasahau tuhuma kuwa Lau Masha aliteuliwaje tokana na konnekisheni na RizOne? Wapo wanaokwenda mbali kudai eti wengine waliteuliwa kutokana na ukaribu na Bi Mkubwa rais wa WAMA. Ajabu wahusika hawakanushi tuhuma hizi. Waulize akina Mwanaidi Majaar waliulaje.
   
 6. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #6
  May 8, 2012
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,627
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280
  - Mkuu mleta mada kwani katiba ya Jamhuri inasemaje kuhusu Watoto wa The sitting President na Sherehe za Ikulu?

  - Halafu pia uweke wazi Katiba hiyo hiyo inasema nini kuusu hao wananchi wengine wa kwaida waliohudhuria huko jana, infact na mimi nilikuwepo pia, I mean ndio njia pekee ya kukata mzizi wa fitina, otherwise isije ikawa wivu na chuki binafsi bila hoja za msingi! au?

  William.
   
 7. Globu

  Globu JF-Expert Member

  #7
  May 8, 2012
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 7,975
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Wivu wa kike tu huo, ndio unaowasumbueni. Ungelikuwa wewe ndio Mkuu wa kaya, ungeliwafukuza wanao?
   
 8. H

  Huihui2 JF-Expert Member

  #8
  May 8, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 395
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  inabidi walio aapishwa wawajue kuwa wale ndiyo wadau wakubwa wa ikulu, ili watakapotaka michongo ya biashara wasijesema hawawajui
   
 9. S

  SURUMA JF-Expert Member

  #9
  May 8, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,908
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  Mfalme asipowashirikisha warithi wake katika day to day activities za ufalme watajifunzaje kazi wanazotakiwa kurithi? Haya ni mafunzo kwa vitendo jamani!
   
 10. Nyangomboli

  Nyangomboli JF-Expert Member

  #10
  May 8, 2012
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 2,307
  Likes Received: 649
  Trophy Points: 280
  2015 watasononeka sana. Hawaoni Mubarack na wanae? Hata hivyo ndiyo wadau na ndiyo wapanga timu zote za uwaziri au ubalozi na kila kitu cha big house.
   
 11. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #11
  May 8, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,185
  Trophy Points: 280
  Eee ee jamani, mwanadamu hatosheki, hata ukimpa nini, milele hataridhika...

  Nyerere kawabana watoto wake mpaka leo kina Ganesh wamechanganyikiwa na maisha, tumemsema sana Nyerere. Mzee wa watu wanawe alikuwa hata haonani nao mpaka hela za madaftari wanapewa na Butiku. Tumemsema Nyerere mnoko.

  Kikwete katokea rais social, anawapa good time watoto, naye tunamsema.

  Tunataka nini hasa?
   
 12. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #12
  May 8, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  -Tunaongelea Facts wewe ni mtoto wa Mkubwa na Unamjua Makongoro Nyerere Wakati J.K. Nyerere alipokuwa anawaapisha Mawaziri Baba yako akiwa Mmoja wao sidhani ilikuwa faragha pia ya watoto kuvaranda Ikulu bila sababu yoyote ile na kuongea na Wageni Wakuu Waalikwa.

  Ni Sherehe Ngapi Umehudhuria za Mawaziri kuapishwa?

  - Katiba sio pana kiasi cha kusema kuhusu wageni watakao hudhuria kuapishwa kwa Mawaziri, Hakuna Fitina ni kuwa logistically kuna umaana gani ya hao watoto kwenda?

  - Kuhudhuria kwako sio kubaya ni vizuri na ni njia ya kujionyesha ili mbeleni ufanikiwe kugombea Ubunge, kwahiyo kuwepo kwako kulikuwa sio bila maana yoyote, ilikuwa baadaye itakulinda na kukujengea chakula kwa kuupata Ubunge au Ujumbe wa NEC.

  Tunampenda Rais wa nchi yetu, kwanini tuwe na chuki na amebakiza Miaka Miwili na Nusu kutawala nchi?
   
 13. Sema Chilo

  Sema Chilo JF-Expert Member

  #13
  May 8, 2012
  Joined: Mar 24, 2012
  Messages: 324
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi naona haina tabu kwani ndio wakati wao kwani si muda mrefu watakuwa hawna access tena na hilo jumba waaaacheni jamani
   
 14. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #14
  May 8, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Watakuwa walikuja home kwao mara moja, they ar too old kujifungia jamani. Wakianza kumsindikiza baba yao kwenye misiba ya kitaifa kama ule wa Kanumba, basi hapo ndo mseme.
   
 15. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #15
  May 8, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  ulaisi umepata laisi, shughuli imepata mshughulikaji.
   
 16. Maishamapya

  Maishamapya JF-Expert Member

  #16
  May 8, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,280
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  W. J. Malecela, naamini kuwepo kwao kusingeleta gumzo kama hayo mengine yaliyo nyuma ya pazia yasingekuwepo. Mengi yamezungumzwa kuhusu Riz1 na Miraji. Kwa kifupi kuwapo kwao ni news!
   
 17. Sniper

  Sniper JF-Expert Member

  #17
  May 8, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,944
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  2015 wataisoma namba
   
 18. Kiona

  Kiona JF-Expert Member

  #18
  May 8, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 936
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Mtoto wa nyoka ni nyoka siku zote hawezi kuwa jongoo
   
 19. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #19
  May 8, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,673
  Trophy Points: 280
  Mleta thread pale kwenye viwanja vya Ikulu tumeona sura nyingi ngeni kabisa lakini wewe umechambuwa wawili na kuwapiga picha na kuleta humu JF tufahamishe na wale wengine walikuwa na sababu gani kuwa Ikulu.
   
 20. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #20
  May 8, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  ni wageni waalikwa kama wageni wengine.
   
Loading...