Kulikuwa na sababu gani za msingi, au kuna faida gani kwa wasaidizi wa Rais Magufuli kumpuuza Makamu wa Rais Samia Suluhu?

Huyu mama toka aseme askari wa ccm wanapiga risas sijui ngapi vile,hata boss wake mwenyewe kamshusha thamani
 
Tuna wapinzani wa hovyo sana ,

You can imagine hizi ndio hoja wanaleta tukae kuzijadili kama Taifa.
Sisiti kukuita mpumbavu! Yaani msemaji wa ofisi kuu ndani ya nchi anatoa taarifa ya uongo kama hiyo na wanao hoji unawaita wa hovyo! Jinga sana wewe! Eti wapinzani, kwa hiyo ukiwa CCM huwezi kuhoji ubwege wowote utakao toka serikalini hadi uwe mpinzani?
Nimetumia lugha kali nadhani ndio size yako
 
Kwani Makamu wa Rais anapokuwa anamuwakilisha Rais huko nje ( hasa Ulaya ) au hata katika nchi zingine hapa hapa Barani Afrika Kiitifaki huwa inatambulikaje?

Tuacheni Nongwa na tupunguze Kumsakama Rais au Taasisi yake ya Urais kwa Chuki zetu kila Uchao tu. Kiitifaki sijaona tatizo lolote lile ikisemwa ( ikitangazwa ) kuwa Rais ameshiriki Kikao hata kama aliyekihudhuria ni Makamu wake.

Hilo la Waziri Mwigulu Nchemba Kumtishia huyo Dada Maria kama ni kweli basi nadhani PhD yake haitumii vyema katika Kufikiri ( Kufikiria ) hivyo airejeshe tu huko Chuoni na aendelee kubakia na Upumbavu pamoja na Ushamba wake.

Alichotakiwa Kufanya Waziri Nchemba si Kumtishia Dada Maria ( kama ni kweli ) bali ni Kumuelekeza tu kwa Mtazamo wa Kiitifaki na Kidiplomasia juu ya hilo na wala hili Jambo lisingekuwa Kubwa hivi na la Kimjadala. Makamu wa Rais anafanya Kazi za Rais, ni Msaidizi wake na Muwakilishi wake Mkuu katika Matukio yote ya Kiitifaki hivyo akihudhuria Yeye ( Makamu ) na ikatangazwa Rais amehudhuria wala hakuna Kosa ( tatizo ) lolote hapo.
Hujaelewa hoja , HOJA NI KWANINI KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS (IKULU)ISEME UONGO KUWA Kwaya master alihudhulia kikao na kuweka picha ya kwaya master wala iso na bendera ya africa mashariki kama wenzie na hata mama samia aliiweka ,umeelewa sasa?
 
Hii kukwepa mikusanyiko ya marais wenzake inatugharimu sana Tanzania. Hakuna tena diplomasia, pia uhusiano na wenzake wa Afrika Mashariki uko chini. Hakuna rais wa Africa Mashariki anayehudhuria matukio Tanzania. Najua, mtasema twajitoshleza na hatuhitajii wengine!
Kwani kidagaa nae kamtema?
 
Kutoshiriki mikutano inayoshirikisha viongozi wenzake inaonyesha kuwadhalilisha.....kwamba hatoi uzito stahiki kwenye mikutano inayohusisha viongozi wakuu wa nchi nyingine, labda dharau au kiburi sijui....
 
Wale marais wenzake wanaongea English sasa Meko angeongea nini. Si ingekuwa mambo ya aibu.

You are off the point...

Mjadala uliopo ni kwanini Ikulu imedanganya umma kuwa Rais Magufuli kashiriki mkutano wa wakuu wa EAC huku ukweli ukiwa ni VP ndiye aliyeshiriki...?

Ikulu ilikuwa na maana gani kusema uongo mbaya na wa kijinga kama huu? Wana nia gani na VP? Ni kumdharau au ni kitu gani?

Kwa hiyo jadili hoja kwa kuwa ndani ya mantiki ya hoja. Ishu ya Magufuli kujua au kutojua Kiingereza haina nafasi hapa hata kama ni kweli ndivyo alivyo...
 
Back
Top Bottom